Diamond Platinumz na Zuchu waonyesha sura ya binti yao Sandrah (Sanura)

Diamond Platinumz na Zuchu waonyesha sura ya binti yao Sandrah (Sanura)

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Wasanii Diamond Platnumz na Zuchu, wamezidi kuvuta hisia za mashabiki wao kufuatia hatua yao ya hivi karibuni ya kuchapisha picha mpya za mtoto wao wa kike, Sandrah Nasibu Issac.

Tofauti na awali ambapo walikuwa wakitumia emoji kuficha kabisa sura yake kwenye mitandao ya kijamii, picha za hivi karibuni zimeweka wazi muonekano wa mtoto huyo na kutoa fursa kwa umma kushuhudia muunganiko wa kifamilia wa wasanii hao.

Taarifa za uwepo wa mtoto huyo zilianza kushika kasi wakati wa sherehe za kifahari za arobaini zilizohudhuriwa na familia na ndugu wa karibu.

Katika sherehe hizo, mama mzazi wa Zuchu, Bi. Khadija Kopa, alitangaza rasmi jina la mjukuu wake kuwa ni Sandrah, huku pia akipewa jina la pili la Sanura kwa heshima ya bibi yake, Mama Dangote.
1789246538101.jpeg
 
Back
Top Bottom