Msanii wa kimataifa kutoka Tanzania Diamond Platnumz ajinyakulia tuzo ya Afrimma katika kipengeke cha Msanii bora wa kiume Afrika Masharika.
Diamond Platnumz amenyakua tuzo hiyo na kuwapiga chini wasanii wawili kutoka Tanzania Darassa pamoja na Ali Kiba ambao nao walikua katika kinyang’anyiro hicho ambacho Diamond ameibuka kinara.
Tuzo za Afrimma mwaka huu zimetolewa mjini Dallas, Texas nchini Marekani huku zikipambwa na wasanii mbalimbali ambao walipanda jukwaani kwa ajiri ya kufanya ‘show.’akiwemo Diamond na Rayvanny kutoka Tanzania.
PianDiamond amewashinda wasanii kadhaa wakubwa wa Afrika kama Davido na Wizkid ambao walikuwa wakiwania tuzo hiyo katika kipengele kimoja kama inayonekana hapa chini;