NALIA NGWENA
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 11,297
- 14,588
Diamond Platnumz, msanii namba moja wa muziki Afrika Mashariki na mwanzilishi wa lebo ya WCB Wasafi, amethibitisha mara nyingi kuwa ana "jicho la kipekee" linapokuja kwenye kugundua na kukuza vipaji vipya. Si tu kwamba ana uwezo wa kutengeneza muziki bora, bali pia ana kipawa cha ajabu cha kutambua wasanii wenye uwezo wa kung'aa kimataifa hata kabla hawajapewa jukwaa.
Kupitia lebo ya WCB, Diamond ameweza kuwatambulisha wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Mbosso na wengine waliogeuka kuwa mastaa wakubwa wa Afrika. Kila msanii aliyeshika mkono wake amekuwa gumzo si kwa sababu ya jina la Diamond pekee, bali kwa sababu walikuja na kitu cha kipekee alichokiona mapema kabla ya wengine.
WCB ilikuwa ya moto sana hasa katika kipindi cha dhahabu kilichojumuisha mastaa kama Rayvanny, Harmonize, Rich Mavoko (aliyeitwa Messi wa Bongo Fleva), Mbosso, Queen Darleen na wengine. Hii timu ilijua kutuburudisha sana kila mwezi kulikuwa na ngoma mpya, video kali, na ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Walileta radha mpya kwenye muziki wa Bongo Fleva na kuifanya WCB kuwa daraja la mafanikio kwa wasanii chipukizi.
Hata hivyo, siku hizi kumekuwa na changamoto katika uteuzi wa vipaji vipya. Mfano wa wazi ni D Voice, ambaye wengi wanadai hana ubora wa kuwa ndani ya WCB. Uwezo wake ni wa kawaida mno, na hana ule utofauti unaohitajika kuvutia soko la muziki linalozidi kuwa na ushindani mkubwa.
Za ndani zinaeleza kuwa kuna sajili mpya inakuja ndani ya WCB, jambo ambalo linawafanya mashabiki wengi kuwa na hamu kubwa ya kuona ladha mpya. Lakini kabla ya hatua hiyo kuchukuliwa, nachukua nafasi hii kumshauri Diamond Platnumz mwenyewe kuingia mbele kabisa kwenye jukumu la kusaka na kusimamia vipaji. Mashabiki wa WCB wanatamani kurudishiwa radha ya zamani, ubunifu wa kweli, na burudani isiyo na mfano vitu ambavyo yeye binafsi aliwahi kusimamia kwa mafanikio makubwa.
Kwa kifupi, Diamond si tu msanii, bali ni injini ya vipaji. Ili WCB irudishe heshima yake kama chuo kikuu cha muziki Afrika Mashariki, ni muhimu Diamond mwenyewe ashike tena usukani wa kusaka vipaji. Jicho lake linaona mbali linaona kile ambacho wengine hawawezi kuona.