Diamond Platnumz aanza kutoa msaada wa kodi ya miezi 3 kwa kaya 500

Diamond Platnumz aanza kutoa msaada wa kodi ya miezi 3 kwa kaya 500

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
4752f03228bbbc7385950dcf503e1bb3

Mkurugenzi wa kampuni ya Wasafi, msanii Diamond Platnumz ametoa msaada wa kodi ya pango kwa watu 57 ambao ni wajane, walemavu pamoja na wasiojiweza.

Msaada huo ni awamu ya kwanza katika ile dhamira yake ya kusaidia kodi ya pango kwa kaya 500 nchini zilizoathirika kiuchumi na janga la mlipuko wa virusi vya Corona.

Diamond Platnumz ametoa msaada huo leo katika makao makuu ya ofisi za kampuni ya WasafiMedia baada ya watu zaidi ya 100 kujitokeza ofisini hapo ambapo familia 57 zimeweza kupata msaada huo.

Kufuatia jambo hilo, familia zilizobakia kwenye orodha ya kaya 500 ni 443 ambapo mchakato unaendelea kwa ajili ya kuzipata kaya za wajane, walemavu na wasiojeweza.

==============

Fuatilia Diamond alivyoahidi:

Msanii Diamond Platnumz kulipa kodi ya nyumba ya miezi 3 kwa familia 500 za hali ya chini - JamiiForums
 
hata kiba katoa ventilators kwa nchi ya marekani sema ndo vile tu hapendi kujitangaza
 
Niseme tu kwamba siku ya Jumatano nimeshuhudia msafara wa huyu mwamba ukielekea Kijitonyama na kweli ulitia nanga kwenye nyumba moja wanaishi walemavu wenye tatizo la kuona, kwa hicho nilichokiona, nashawishika huenda mchakato wa kuwatambua wahitaji umefanyika vizuri.

Yote kwa yote, tumpongeze kijana kwa anachokifanya, si lazima kukubaliana nae au kupendezwa na kila anachokifanya ila pale anapofanya vizuri, kumtia moyo ni uungwana.

Niwatakie mfungo mwema na kuwakumbusha kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.
 
Hongera diamond, nimeona unawasiliana na wanao pia... this is maturity.. Hongera sana
Si tu yeye kuwa mature lakini pia zari nae amekuwa mature kwa kukubali kuwa mwanaume siku zote atabaki kuwa mwanaume sio wakumvimbia au wa kushindana nae.
 
Si tu yeye kuwa mature lakini pia zari nae amekuwa mature kwa kukubali kuwa mwanaume siku zote atabaki kuwa mwanaume sio wakumvimbia au wa kushindana nae.
School fees haziingii,lazima awe mature ama alale njaa
 
bongo fleva bila mondi ingekua mtaloni maana jamaa kaichangamsha na kuwapa changamoto kweli kweli wenzako japo wanamchukia badala yakuzifanyia kazi changamoto anazowapa
 
Back
Top Bottom