Diamond Platnumz adaiwa kodi Sh. Milioni 400 na TRA

cosa nostra

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2010
Posts
1,773
Reaction score
1,805
IMG_6402.PNG

Ni miezi mbili tu iliyopita ambapo Diamond alienda kwa makao makuu ya Mamlaka ya Mapato TRA baada ya kuitwa ili alelezee namna anavyopata mapato yake na namna gani analipa kodi ya serikali.

Diamond alipewa cheti na TRA kama dhibitisho kuwa analipa kodi ya serikali kama inavyohitajika na sheria ya Tanzania.

IMG_6401.JPG

Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia hata hivyo aliluambia Bunge kuwa Diamond anadaiwa na Mamlaka ya Mapato zaidi ya shilingi milioni 400.

Mheshimiwa Mtulia alidai kuwa hit maker huyo wa ‘Marry You’ alimwambia kwa sasa anadaiwa kodi ya zaidi ya shilingi milioni 400 na TRA.

Mbunge huyo aliyasema hayo wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ulipokuwa ukijadiliwa bungeni.
 
ana miliki nini na nini mpaka iwe ml 400
 
Sio lazima umiliki vitu ndio udaiwe kodi. Kodi inatokana na kipato unachopata. Wataalamu wa kodi wanaweza kuwa wamekusanya malipo yote aliyolipwa na makampuni mbalimbali, wakamtaka ajaze fomu mbali mbali za kutoa taarifa mapato yake. Wakayalinganisha, wakakokotoa ndio wakafikia hapo. Na pia inawezekana sio kwa mwaka mmoja.
 
perfume moja ya Chibu sh 105,000 akiuza perfume elfu kumi anakua ina pato la sh bilioni 1.05

Anauza nyimbo wasafi.com sh 300 akiuza nyimbo 1,000,000 anakua na pato la sh 300,000,000

anafanya biashara za matangazo na Vodacom,cocacola,GSM etc

Bado unauliza inakuaje anadaiwa deni hilo

Pia kikubwa kijana yuko Legit vitu vyake vyote vinajulikana kisheria sio kama wabongo fleva wengine wanakwepa kilipa kodi
 
Correct asante
 
Inawezekana coz ana magari ya bei sana kwahy kodi zake lazma nikubwa na pia makampun yanayomtumia lazma yalipie nk [emoji6][emoji6]
 
perfume moja ya Chibu sh 105,000 akiuza perfume elfu kumi anakua ina pato la sh bilioni 1.05

Anauza nyimbo wasafi.com sh 300 akiuza nyimbo 1,000,000 anakua na pato la sh 300,000,000

anafanya biashara za matangazo na Vodacom,cocacola,GSM etc

Bado unauliza inakuaje anadaiwa deni hilo

Pia kikubwa kijana yuko Legit vitu vyake vyote vinajulikana kisheria sio kama wabongo fleva wengine wanakwepa kilipa kodi
Sawia kabisa.
Kijana anajitahidi sana kujihangaisha na kusaka kipato, sitashangaa kama TRA wanamdai pesa hio!
 
perfume moja ya Chibu sh 105,000 akiuza perfume elfu kumi anakua ina pato la sh bilioni 1.05

Anauza nyimbo wasafi.com sh 300 akiuza nyimbo 1,000,000 anakua na pato la sh 300,000,000

anafanya biashara za matangazo na Vodacom,cocacola,GSM etc

Bado unauliza inakuaje anadaiwa deni hilo

Pia kikubwa kijana yuko Legit vitu vyake vyote vinajulikana kisheria sio kama wabongo fleva wengine wanakwepa kilipa kodi

!
!
Kijana ana hela aisee inabidi tu umpende vinginevyo unaweza kukonda sana
 
Diamond hata kama anadaiwa billion moja bado siyo issue.
 
Diamond anachitakiwa kuwa nacho ni kuwa na mshauri wa kodi. Atamsaidia mengi badala ya kulalamika. Ukijipanga vema kodi inalipika.
 
Back
Top Bottom