Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz afichua kuwa alilipwa dola 150k sawa na TSh. Miloni 374 (373,554,903) kutumbuiza nchini Kenya katika show iliyovurugika mwisho wa wiki.
Taarifa hii imekuja wakati akijibu madai kwamba alihusika katika kumzuia msanii wa Kenya, Willy Paul, kupanda jukwaani wakati wa tamasha la Furaha Festival.
Soma, Pia: Ujinga alioufanya msanii Willy Paul jana dhidi ya wasanii wa Tanzania ukemewe vikali
Diamond ameeleza kuwa hakuhusika na suala hilo, akisisitiza kuwa yeye alifuata ratiba yake ya kazi na hakukuwa na sababu ya kuzuia msanii mwingine kuonyesha kipaji chake. Madai haya yamezua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wakitoa maoni tofauti kuhusu tukio hilo.