Responded Diamond Platnumz amjibu memba wa JamiiForums, amwambia "Mkataba wangu na Warner ni Sh Bilioni 13"

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Kuna uzi nilianzisha humu kuhusu wasanii wa Tanzania kutosainiwa na lebo za kimataifa

Hoja ya Mdau iko hapa ~ Ayra Starr amesainiwa Roc Nation. Tanzania tunafeli wapi wasanii wetu kusainiwa na lebo za kimataifa?

Naona msanii wenu kajibu kwa haraka sana akisema kuwa hiyo hoja yeye haimuhusu maana ana international brands nyingi anazofanya kazi

Haya ndo mahela aliyoyataja!

photo_2025-07-21_11-29-05.jpg

Screenshot 2025-07-21 115823.jpg
 
Rocnation ya JIGA Jay Z?
Ndio dokta ..

Kwangu Mimi naona hii mikataba ni ya kinyonyaji na zaidi ukishaingia spiritually Kuna vitu inabid ukubaliane navyo unaweza kuishia kua mateka tu wakakutumia na kukuacha ama wakapata faida kubwa wewe kiduchu. ...huyo jay z kutoa Dola laki 2.5 naona ilikua ni dharau, hata mwakinyo alikataa mkataba aliopewa na Mayweather ya boxing...Hawa watu Wana pesa nyingi badala watumie platform zao kusaidia wengine wao ndio kwanza Wana offer mikataba ya kishenzi tu ...wanaowaweza Hawa ni wanaijeria ...wanaijeria kwenye kutafuta pesa ni wajanja mno, ndio mana huyo ayra star aliesaini roc nation pesa nyingi imetoka ila lebo inayommiliki Bado Wana makubaliano ya production etc ..roc nation. Wako kwa ajili ya kupush tu...
 
Kuhusu mambo ya kiroho ni nadharia tu mkuu

Hawa watu wa USA Kama Jay Z wanasimamia Sana Malengo na kujinyima mambo mengi mpaka wakanuwa well successful.

Kwahiyo hakuna uchawi hapo Mkuu Jay Z amekuwa Star tangu akiwa na miaka 26 na sasa Ana 55 yrs na bado anaendelea kusikika .

Kwahiyo yeye kuwa bilionea ni kitu ambacho kinawezekana.

Wapo very smart .

kuhusu unyonyaji hata Diamond anawanyonya walio chini yake ni mifumo ya kibepari
 
Kaka mjadala wako ni mzuri sana na umeibua mengi, naona kuna umuhimu wa kuelewa kwamba mikataba ya wasanii na lebo za kimataifa huwa hazifanani kuna aina tofauti za deals, na kila moja ina faida na hasara zake. Hapa chini ni breakdown fupi ya aina kuu za mikataba:

🔹 1. Full Record Deal (Exclusive Recording Contract)
Hii ni ile ambapo msanii anasainiwa kabisa lebo inasimamia kila kitu: recording, distribution, marketing, publishing, tour support, n.k. Msanii anakuwa chini yao full time, wanapewa advance kubwa lakini lebo inachukua asilimia kubwa ya mapato.

Mfano: Burna Boy alisaini full record deal na Atlantic Records (Warner) mwaka 2017. Baada ya hapo, alitoka kwenye Spaceship kama lebo yake ya kwanza, na kujiunga fully na Atlantic kwa global reach. Hii ndio deal iliyomsukuma hadi kushinda Grammy, kujaza London na Tottenham hospers Stadium back to back, top 20 album chart kwenye Billboard 200 na number 1 album kwenye UK album's chart.

🔹 2. Distribution Deal
Hapa msanii au lebo yake binafsi (independent label) inaendelea kumiliki content, lakini inawapa kampuni kubwa kazi ya kuisambaza (distribution) kwenye market kubwa, hasa Marekani na Ulaya. Msanii ana uhuru zaidi, mapato pia ni mazuri.

Mfano: Deal la Ayra Starr na Roc Nation kwa mujibu wa taarifa, ni distribution/management deal ya kumpush Amerika na Ulaya, lakini bado yupo chini ya Mavin Records Afrika. Don Jazzy bado anasimamia production na distribution ya ndani.

🔹 3. Licensing Deal
Hapa msanii au lebo yake inatengeneza muziki, kisha inaipa lebo kubwa haki ya kuuza au kusambaza kwenye maeneo fulani tu (kwa muda fulani). Msanii hubaki na haki zaidi, hulipwa kwa asilimia.

Mfano: Mikataba mingi ya wasanii wa Amapiano waliopata virality kama Uncle Waffles huwa ni licensing ambapo wanaendelea kuwa independent lakini lebo kubwa inapewa haki ya kusambaza content zao kwenye market fulani.

🔹 4. 360 Deal
Hii ni deal ambayo lebo inahusika na kila kipato cha msanii: muziki, shows, brand endorsements, merch n.k. Msanii anapewa support kubwa (mara nyingi na advance kubwa), lakini kampuni inachukua asilimia ya mapato yote ya msanii. Ni nzuri kwa msanii anayetaka kupenya haraka, lakini inaweza kuwa ya “kinyonyaji” kama msanii hana bargaining power.

Mfano: Deal ya Tyla na Epic Records (Sony) inaelezwa kuwa ni aina ya 360 deal kwa maana kwamba label inacontrol hadi upande wa performances, endorsement deals n.k. Lakini kwa kuwa alikuwa ameshasaini na Fax Records (ya Afrika Kusini), label hiyo ilihusika kwenye negotiations pia, na amekuwa na benefit kubwa since “Water” kuhit.

Kwa kifupi:

Wasanii wa Nigeria na Afrika Kusini wameweza kuingia kwenye deals mbalimbali kwa sababu wana teams zenye kuelewa game ya kimataifa.

Siyo lazima msanii asaini full deal ndiyo awe na mafanikio. Hata distribution au licensing ya kimkakati inaweza kumfikisha mbali.

Tanzania bado tunahangaika na uelewa wa aina hizi za mikataba, na wengi wetu tunafikiri "kusainiwa tu" ni mafanikio, bila kujua impact yake kwenye career.

Kama kuna anayejua zaidi kuhusu deal la Diamond na Universal na Warner, ni vizuri pia tukajua ilikuwa ya aina gani maana ye mwenyewe hajataja, kwa Afrika very few have full major deals like Burna.
 
Wakati wamarekani wenyewe wanapambana kuwa independent artists wamatumbi mnataka muwe signed under. Mmerogwa?

Ali Kiba, Ommy Dimpoz, V Mdee, Lunya walisainiwa waliishiwa wapi? For the most part ilikua ndo mwanzo wa mwisho wao. D'banj wa Nigeria alikua under Good Music ya Kanye for a hot minute aliishia wapi? Naye anguko lake lilianza hapo. Lunya bado yupo under Sony nani anamsikia tena Lunya siku hizi?

Hii mikataba sio hisani. Hakuna free money kila mtu anawaza kukupiga. Nani anampa Mondi offer ya 250k kama sio ujuha? If anything, ningesema wakae nayo mbali.
 
Kaka mjadala wako ni mzuri sana na umeibua mengi, naona kuna umuhimu wa kuelewa kwamba mikataba ya wasanii na lebo za kimataifa huwa hazifanani kuna aina tofauti za deals, na kila moja ina faida na hasara zake. Hapa chini ni breakdown fupi ya aina kuu za mikataba:

🔹 1. Full Record Deal (Exclusive Recording Contract)
Hii ni ile ambapo msanii anasainiwa kabisa lebo inasimamia kila kitu: recording, distribution, marketing, publishing, tour support, n.k. Msanii anakuwa chini yao full time, wanapewa advance kubwa lakini lebo inachukua asilimia kubwa ya mapato.

🔹 2. Distribution Deal
Hapa msanii au lebo yake binafsi (independent label) inaendelea kumiliki content, lakini inawapa kampuni kubwa kazi ya kuisambaza (distribution) kwenye market kubwa, hasa Marekani na Ulaya. Msanii ana uhuru zaidi, mapato pia ni mazuri.

🔹 3. Licensing Deal
Hapa msanii au lebo yake inatengeneza muziki, kisha inaipa lebo kubwa haki ya kuuza au kusambaza kwenye maeneo fulani tu (kwa muda fulani). Msanii hubaki na haki zaidi, hulipwa kwa asilimia.

🔹 4. 360 Deal
Hii ni deal ambayo lebo inahusika na kila kipato cha msanii: muziki, shows, brand endorsements, merch n.k. Msanii anapewa support kubwa (mara nyingi na advance kubwa), lakini kampuni inachukua asilimia ya mapato yote ya msanii. Ni nzuri kwa msanii anayetaka kupenya haraka, lakini inaweza kuwa ya “kinyonyaji” kama msanii hana bargaining power.

Kwa kifupi:

Wasanii wa Nigeria na Afrika Kusini wameweza kuingia kwenye deals mbalimbali kwa sababu wana teams zenye kuelewa game ya kimataifa.

Siyo lazima msanii asaini full deal ndiyo awe na mafanikio. Hata distribution au licensing ya kimkakati inaweza kumfikisha mbali.

Tanzania bado tunahangaika na uelewa wa aina hizi za mikataba, na wengi wetu tunafikiri "kusainiwa tu" ni mafanikio, bila kujua impact yake kwenye career.

Kama kuna anayejua zaidi kuhusu deal la Diamond na Universal na Warner, ni vizuri pia tukajua ilikuwa ya aina gani maana ye mwenyewe hajataja, kwa Afrika very few have full major deals like Burna.
Burna yeye ukoje mkataba wake mkuu?
 
Back
Top Bottom