Ndio dokta ..Rocnation ya JIGA Jay Z?
Ndio dokta ..
Kwangu Mimi naona hii mikataba ni ya kinyonyaji na zaidi ukishaingia spiritually Kuna vitu inabid ukubaliane navyo unaweza kuishia kua mateka tu wakakutumia na kukuacha ama wakapata faida kubwa wewe kiduchu. ...huyo jay z kutoa Dola laki 2.5 naona ilikua ni dharau, hata mwakinyo alikataa mkataba aliopewa na Mayweather ya boxing...Hawa watu Wana pesa nyingi badala watumie platform zao kusaidia wengine wao ndio kwanza Wana offer mikataba ya kishenzi tu ...wanaowaweza Hawa ni wanaijeria ...wanaijeria kwenye kutafuta pesa ni wajanja mno, ndio mana huyo ayra star aliesaini roc nation pesa nyingi imetoka ila lebo inayommiliki Bado Wana makubaliano ya production etc ..roc nation. Wako kwa ajili ya kupush tu...
Mfano: Burna Boy alisaini full record deal na Atlantic Records (Warner) mwaka 2017. Baada ya hapo, alitoka kwenye Spaceship kama lebo yake ya kwanza, na kujiunga fully na Atlantic kwa global reach. Hii ndio deal iliyomsukuma hadi kushinda Grammy, kujaza London na Tottenham hospers Stadium back to back, top 20 album chart kwenye Billboard 200 na number 1 album kwenye UK album's chart.
Mfano: Deal la Ayra Starr na Roc Nation kwa mujibu wa taarifa, ni distribution/management deal ya kumpush Amerika na Ulaya, lakini bado yupo chini ya Mavin Records Afrika. Don Jazzy bado anasimamia production na distribution ya ndani.
Mfano: Mikataba mingi ya wasanii wa Amapiano waliopata virality kama Uncle Waffles huwa ni licensing ambapo wanaendelea kuwa independent lakini lebo kubwa inapewa haki ya kusambaza content zao kwenye market fulani.
Mfano: Deal ya Tyla na Epic Records (Sony) inaelezwa kuwa ni aina ya 360 deal kwa maana kwamba label inacontrol hadi upande wa performances, endorsement deals n.k. Lakini kwa kuwa alikuwa ameshasaini na Fax Records (ya Afrika Kusini), label hiyo ilihusika kwenye negotiations pia, na amekuwa na benefit kubwa since “Water” kuhit.
Burna yeye ukoje mkataba wake mkuu?Kaka mjadala wako ni mzuri sana na umeibua mengi, naona kuna umuhimu wa kuelewa kwamba mikataba ya wasanii na lebo za kimataifa huwa hazifanani kuna aina tofauti za deals, na kila moja ina faida na hasara zake. Hapa chini ni breakdown fupi ya aina kuu za mikataba:
🔹 1. Full Record Deal (Exclusive Recording Contract)
Hii ni ile ambapo msanii anasainiwa kabisa lebo inasimamia kila kitu: recording, distribution, marketing, publishing, tour support, n.k. Msanii anakuwa chini yao full time, wanapewa advance kubwa lakini lebo inachukua asilimia kubwa ya mapato.
🔹 2. Distribution Deal
Hapa msanii au lebo yake binafsi (independent label) inaendelea kumiliki content, lakini inawapa kampuni kubwa kazi ya kuisambaza (distribution) kwenye market kubwa, hasa Marekani na Ulaya. Msanii ana uhuru zaidi, mapato pia ni mazuri.
🔹 3. Licensing Deal
Hapa msanii au lebo yake inatengeneza muziki, kisha inaipa lebo kubwa haki ya kuuza au kusambaza kwenye maeneo fulani tu (kwa muda fulani). Msanii hubaki na haki zaidi, hulipwa kwa asilimia.
🔹 4. 360 Deal
Hii ni deal ambayo lebo inahusika na kila kipato cha msanii: muziki, shows, brand endorsements, merch n.k. Msanii anapewa support kubwa (mara nyingi na advance kubwa), lakini kampuni inachukua asilimia ya mapato yote ya msanii. Ni nzuri kwa msanii anayetaka kupenya haraka, lakini inaweza kuwa ya “kinyonyaji” kama msanii hana bargaining power.
Kwa kifupi:
Wasanii wa Nigeria na Afrika Kusini wameweza kuingia kwenye deals mbalimbali kwa sababu wana teams zenye kuelewa game ya kimataifa.
Siyo lazima msanii asaini full deal ndiyo awe na mafanikio. Hata distribution au licensing ya kimkakati inaweza kumfikisha mbali.
Tanzania bado tunahangaika na uelewa wa aina hizi za mikataba, na wengi wetu tunafikiri "kusainiwa tu" ni mafanikio, bila kujua impact yake kwenye career.
Kama kuna anayejua zaidi kuhusu deal la Diamond na Universal na Warner, ni vizuri pia tukajua ilikuwa ya aina gani maana ye mwenyewe hajataja, kwa Afrika very few have full major deals like Burna.
Anasema mtu aliyeunga bando la mkopo la jeroHela ndogo sana kwa wasanii wanaoingia mikataba ya kuuza nafsi...
Sheria ya kodi mtu akiingiza pesa Marekani anatakiwa akatwe income tax hukohuko, upo hapo?TRA wanaemaje