Responded Diamond Platnumz amjibu memba wa JamiiForums, amwambia "Mkataba wangu na Warner ni Sh Bilioni 13"

Mambo ya ushirikina kwenye mziki na filamu Marekani sio nadharia tena man

Kanye West kipindi ametibuana na walimwengu wakapita na mikataba yake na kila kitu alifanya confession moja ambayo inakuonyesha kuna vitu nyuma ya pazia(ndio juhudi na maarifa pia vinachangia but namba nzuri inatumia njia za mkato).Alitaja watu kama Dr Dre(kifo cha mtoto wake kama sijakosea),Michael Jordan,yeye mwenyewe(kifo cha mama yake) na wengine kibao tu

China McClain(alikuwa muigizaji sijui kwa sasa anafanya nini) ali-confess pia mambo ya giza yanayofanyika kwenye tasnia ya filamu na mziki kwa ujumla.

So,haya mambo sio nadharia man.Watu wamefanya confession kibao na wanaojua wapo japo hawawezi kukueleza kila kitu publicly
 

Mkuu mambo ya kiroho yapo Ila success inahitaji Sacrifice wenzako hao hata kuoa na kuzaa watoto wanaanza wanapambana .

Sasa ikiwa Jayz amejitafuta miaka zaidi ya 30 je anashindeaje kuwa bilionea .


Sisi wabongo hatujitumi na hatuna ndoto kubwa za Ku-archive mambo Makubwa.
 
Burna yeye ukoje mkataba wake mkuu?
Burna Boy alisaini full record deal na Atlantic Records (Warner) mwaka 2017. Baada ya hapo, alitoka kwenye Spaceship kama lebo yake ya kwanza, na kujiunga fully na Atlantic kwa global reach. Hii ndio deal iliyomsukuma hadi kushinda Grammy, kujaza London na Tottenham hospers Stadium back to back, kuingia top 20 album kwenye chati ya Billboard 200 na kupata number 1 album kwenye UK album's chart.
 
Jay z kuwa bilionea ni sawa kwa maana amekaa kwenye tasnia ya mziki kitambo mpaka anaweza kumiliki wasanii wakubwa ujue sio kazi nyepesi.Sema tu ni vipi alifanikisha hilo ndio debate(ukisema kujituma na uvumilivu ni sawa wote tutakubali kwa maana ndicho kinachoonekana,japo utata unakuja watu ambao wako kwenye hiyo industry wakianza kufanya confession ndio unajua kuna vitu zaidi ya kujituma na mengineyo kwenye mafanikio yao)
 
Zaidi ya kazi zao (ambazo kwa kweli madogo wa sasa wanajitahidi na zipo vizuri) hayo ya kipato chao nadhani yanawafaa zaidi familia zao na wategemezi wao...; after all kama wamepigika ni sababu ya utamaduni wetu wa kutokununua kazi na kutegemea piracy...

Naweza kusema wanajitahidi sana, with very little support from the locals...; I Salute them..., Keep Up the Good Work..
 
Understandable kabisa kuwa baadhi ya deals zinawavuruga wasanii wetu na ni kweli 100% kwamba mikataba mingi ya kimataifa haina huruma. Lakini si kila kusainiwa ni ujinga wala kila deal ni ya 'kupigwa'. Kuna tofauti kubwa sana kati ya msanii anayekimbilia pesa ya haraka (cash grab) na msanii anayechagua deal kwa vision ya muda mrefu

Take Burna Boy for example alichagua kuingia kwenye full record deal na Atlantic si kwa sababu hakujua anachofanya, bali kwa sababu alijua anahitaji force ya kimataifa kusukuma brand yake nje ya Afrika. Sasa hivi yupo consistent kwenye Grammy shortlist, anapewa media push kila kona, na brand yake ni global. Hiyo haiji kwa kuingia YouTube na Boomplay pekee

Wamarekani wana luxury ya kuwa independent kwa sababu industry yao iko tayari. Sisi bado tunahitaji mifumo hiyo. Kama kila msanii wa Tanzania ataogopa kusaini kwa sababu wengine walifeli basi hakuna atakayevuka mlango huo. The game si kuwa signed au not signed ni kuelewa game, kuwa na team, na kusign kwa vision not for clout
 
Huyu Jamaa ana matatizo ya akili, ukitaka achafukwe mseme kuwa hana hela, hata kwa kinyume nyume jiwe likipitia karibu tu hata kama haliendi kwake yeye ana panic.
 
Diamond Platnumz kumiliki muziki wake mwenyewe mimi namuona winner. Huu ni utajiri watakuja kutumia mpaka wajukuu zake. Kuna wasanii wakubwa wenye majina, wanauza music na wanapiga show lakini nyuma ya pazia wanaishi kwa credits. Hizo lebel kubwa ndio kulikojaa unyonyaji mpaka wasanii wanadata
 

There's more to mafanikio ya wanigeria than kuwa under big labels. Burna alianza mziki wake UK kabla hajarudi Africa. Wanigeria waliopo nje (diaspora) ni wengi kuliko nchi yeyote ile Africa, in other words, mnigeria kusikika nje ni jambo rahisi sana sababu wanaowasikiliza ni watu wao pia. Msanii underground Nigeria anaweza hit airwaves za Canada au Europe sio sababu anasikilizwa sana na mizungu au kuwa chini ya label fulani bali wanigeria wenzake waliopo huko.

Hizi labels zimewaangusha wengi kuliko kuwasaidia that is a fact. Wamareknai wenyewe wanapambana kila siku kujitoa huko ila bongo watu wanapambana kujiingiza huko huko.

Inawezekana kuna faida chache zipo za kuwa under labels ila sio za maana kama miaka ya nyuma.
 
Huyu Jamaa ana matatizo ya akili, ukitaka achafukwe mseme kuwa hana hela, hata kwa kinyume nyume jiwe likipitia karibu tu hata kama haliendi kwake yeye ana panic.
😁😁😁
 
Ulitaka apewe kiasi gani na kwa kipi hasa anachoimba?

Tunaomba ushahidi wa picha ya mkataba sinza pazuri tusaidie kutufikishia ombi letu la nakala ya mkataba basi. πŸ˜‚πŸ˜‚
 
hajiulizi kwanini hata bro kajibu kwa hasira wakati huwa ana jeuri ya kuwakalia kimya ma haters kama amavyopenda kuwaitaπŸ˜…πŸ˜….

si kila mafanikio yanaamuliwa na juhudi peke yake hasa haya yanayohusisha umaarufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…