Diamond Platnumz amuoa Zuchu. Ni mpango wa kuuzima moto wa Askofu Gwajima?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wakuu

Huu mbona kama ni mkakati hivi wa kutaka kututoa kwenye Reli?

Msanii wa Bongo Fleva, Nadeem Abdul maarufu kwa jina la Diamond Platnumz amemuoa mpenzi wake wa muda mrefu Zuhura Othman Soud maarufu Zuchu. Msanii wa lebo yake WCB Wasafi.

Ndoa hiyo imeibuka katikati mjadala mkali baada ya Mbunge wa Jimbo la Kawe, Askofu Josephat Gwajima, kulaani vikali vitendo vya utekaji vinavyoripotiwa kuendelea nchini Tanzania


Your browser is not able to display this video.
 
Yaani kama kweli ameoa na bado unaamini kafanya hivyo kumzima Gwajima basi utakuwa mtu wa ajibu sana! Hivi Watanzania ujinga ujinga mtaacha lini? Yaani mtu asipooa, oh Diamond anachezea watoto wa watu! Kama kweli ameoa, oh anataka kumzima Gwajima! Ingekuwa wiki moja iliyopita mngesema anataka kuzima issue ya akina Mungi! Ingekuwa wiki moja au mbili kabla ya hapo mngesema anataka kuzima issue ya Bunge la Ulaya! Kama kabla ya hapo mngesema issue ya Mdude! Kabla ya hapo mngesema issue ya Lissu! Na hapo katika kungekuwa na vilaza wengine wangesema kaona wivu harusi ya Jux ilivyo trend kwahiyo alitaka kuizima!

Acheni ujinga ujinga!
 

MAWAZO YA KIJINGA NA HOFU ZA KIPUMBAVU. UNAWEZA KUDHANI NAWE UMEWAZA KAMA GT. GWAJIMA NI MTU MKUBWA KWA SASA HUWEZI MFANANISHA NA HOJA ZA KIPUMBAVU KAMA HIZI
 
Mbona kama cha mkeka kisiri. Sirri
Itakuwa hujawahi kuishi kwenye jamii za kiislamu wewe. Ndoa zao ndo zinavyokuwa, zile taarabu taarabu zao unazoona zinakuja baada ya ndoa kuwa imeshafungwa, wakati mwingine kitambo sana, hata mwaka na zaidi. Hili nalifahamu kwa sababu baadhi ya ndugu zangu ni Waislam na wakati naingia mjini kwa mara ya kwanza niliishi nyumba ya baba wa kiislamu! Siku moja narudi job, nafika kwenye korido nakuta watu kama 6 wanapiga mpunga baada ya ndoa kupita wakati hakukuwa na dalili yoyote!
 
Wabongo tuna matatizo ya akili sana mkuu, yn hawataki watu waishi maisha yao kisa kuna trending ya jambo fulani.

Wabongo kwa kupangiana namna ya kuishi tupo vzr.
 
Hata simba kufungwa tatu lengo ni lilikuwa ni moja
 
Mimi habari za diamond nilishagaacha kufatilia hakuna unalojifunza ni ujinga tu
 
Ukisoma post ya diamond unasema amewai kuoa...hajaona hivi Sasa hiyo ndoa ni ya muda mrefu sio kwamba ameoa.

Na inaonesha wameshaachana
 
Na Gwajimanization inatumika kuzima kesi ya Lissu, no reforms no elections
 
Mimi habari za diamond nilishagaacha kufatilia hakuna unalojifunza ni ujinga tu
Kwanza muongo muongo halaf ndoa gani ile jaman mtoto wa watu hata kasherehe kadogo hakuna ndio maana zuchu hanaga raha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…