Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Kwa mtazamo wangu, watanzania tunakalili ila siku hizi kuna waigizaji kanumba haoni ndani.Jana nilicheki ile video yake ya Zuwena, Diamond Platnumz anaweza kiukweli sio kuimba tu Diamond ni muigizaji mzuri tu tena mbunifu saana.
Kama kuna watu ambao wako karibu naye wa mshauri afanye filamu ya huu wimbo wa Zuwena na amini anaweza pia kuamsha bongo movie na pia anaweza kupata pesa nyingi.
Na yeye sio kwamba ndio atakuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo 20% alifanya hivyo, Papa Wemba alifanya hivyo kwa wimbo wake La vie est belle.
Naomba afanye hivyo kwa faida ya Bongo movie pia
Mfano yule jamaa anaigiza juakali kama luka, ni moto wa kuotea mbali kuanzia kuigiza hadi facial expressions zake zinaendana na anachoigiza. Kuna Mimi Mars, yule binti nadhani ana kipaji kikubwa cha kuigiza kuliko hata kuimba. Yule binti ni moto wa kuotea mbali kabisa.
Kanumba alikuwa mzuri zama zake ila waigizaji wazuri wapo kwa sasa.na siku hizi naona watu wameinvest sana kwenye tamthlia naona tasnia inakua sana. Dstv wanamwaga pesa sana