Apewe PhD 7 kama za msukuma pia sanamu lake lijengwe mikoa yote tz hadi mlima kilimanjaro juu.
Kama hutaki nenda burundi mipaka iko wazi
Jacko kwa uweusi wake Wamarekani wangemtosa asijulikane asilani, lakini kwa akili za Mzungu walimpaisha kwa kigezo tu cha kuwa Mmarekani hadi akaongoza dunia kwenye tasnia ya muziki na kulipa kodi kubwa serikalini. Ana tuzo 100 ikiwemo ya Grammy hadi anaaga dunia.
South Africa, Lucky Dube, Miriam Makeba, Brenda Fassie, Hugh Masekela, Nasty C, Yvone Chakachaka, Amanda, Mafikizolo nk wameinuliwa na nchi yao.
DR Congo, Abeti Masikini, African Fiesta, Avelino, Awilo Longomba, Bimi Ombale, Bisso Na Bisso, Bouro Mpela, Bozi Boziana, Cindy Le Coeur, Dadju, Damso, Dany Engobo, Evoloko Jocker, Diblo Dibala, Dindo Yogo, Fabregas, Fally Ipupa, Ferré Gola, Gaz Mawete, Geo Bilongo, Gibson Butukondolo, Grand Kalle, Pepe Kale, Luambo Luanzo Makiadi, Papa Wemba, M'bilia Bel, Koffi Olomide, nk wamepaishwa na taifa lao na kuwatangaza nje ya Afrika. Wenzao waliokuja Tz kama Remmy Ongara, Makasi, Babu Seya wamefifishwa na roho wa kufisha sekta ya muziki Tz.
Uganda kama mataifa mengine haikuwa nyuma kuinua wanamuziki wake kwa viwango vya kimataifa, Bobi Wine, Dr. Jose Chameleon, Bebe Cool, Ragaa Dee, Grace Nakimera, Ronald Mayinja, Mesaech Ssemakula, Geoferey Lutaaya, Eddy Kenzo, Hajji Haruna Mubiru.
Babu Seya ndiye aliyeghani wimbo maarufu wa "Chama chetu cha Mapinduzi chajenga nchi....." mwaka 1977 wakati TANU na ASP vikiungana kuzaa CCM, alipewa masaa 7 kughani wimbo huo kwa dharura lakini nyota ya muziki Tz haing'aagi. Na ndiyo maana mzee Nnauye na Capt. Komba wamekufa masikini kwa kutumbuizia siasa.
Diamond (kama alivyokuwa Capt. Komba na mzee Nnauye) amechangia kuiweka serikali Ikulu kwenye chaguzi za 2015 na 2020 lakini mafanikio yake hayana mkono wa serikali hata kwa senti 5, ni bidii zake mwenyewe.
Huko DR Congo, zaidi ya 50% ya wanamuziki maarufu ni graduates wa fani ya muziki ndiyo maana wanauza sana kwenye soko la Ulaya na Marekani ambako muziki ni taaluma pia licha ya kuwa kipaji.