Msanii mkubwa wa kimataifa kutoka Tanzania Diamond Platnumz usiku wa Jana alifanikiwa kuchukua tuzo ya Philanthropic Endeavour community action kutokana na mchango mkubwa anatoa kwa jamii.Tuzo hizo zinahusisha wachezaji maarufu pamoja na watu mashuuri wanaofanya vizuri.
Tuzo hizo ziliudhuriwa pia na mchezaji wa zamani wa man United Rio Ferdinand ukiachana na Diamond lakini pia mchezaji maarufu wa Chelsea na team ya ufaransa N'golo Kante pamoja na Wilfred Zaha walipata pia tuzo na wengine baadhi.
Lakini pia msanii wetu Diamond alipata fursa pia ya kuhojiwa na kituo kikubwa Cha uingereza sky sport.
NB: naona kijana azidi kututoa kimasomaso.
-----
Wengine walioshinda kwenye Tuzo hizo zilizotolewa Jijini London, Uingereza. Ni Fuse ODG, Wilfried Zaha, Mosamba, N’golo Kanté, Stormyz, Pia tuzo hizo zilihudhuriwa na watu mbalimbali maarufu akiwemo mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand.
Tuzo za BOA zinafanyika mwaka huu kwa mwaka wa 8 mfululizo, Na huwa zinawaleta pamoja watu mbalimbali ambao wanaunga mkono na kushiriki kwenye maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika bara la Afrika, pamoja na kuwapa Tuzo washindi wa vipengele mbalimbali.
Tuzo za Best of Africa huwa zinawahusisha zaidi wanasoka pamoja na watu mashuhuri ambao wanafanya vizuri kutoka Afrika.