Diamond Platnumz atakuja kuwa kama Mr. Nice asipoangalia

holygrail

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2012
Posts
1,303
Reaction score
597
wasanii wetu yawapasa wawe makini sana. Hebu ona haya mambo kutoka kwa mr.nice. (kwa hisani ya le mutuz)

Katika hali isiiyokuwa ya kawaida mwanamuziki Lucas Mkenda maarufu kwa jina la Mr Nice ameibuka na kueleza sababu zilizomfanya kufirisika licha ya kuwahi kumiliki zaidi ya bilioni moja na nusu kwenye akaunti zake tofauti.

mwanamuziki huyo ambae kwa sasa yupo nchini kwa muda mfupi kabla ya kurudi tena nchini Kenya alikohamishia makazi na kufanyia shughuri zake za kimuziki huko. Akizungumza na mwandishi wetu kwenye ukumbi wa mpya wa burudani wa Full Stop uliopo Mwanamboka Kwa Manyanya Kinondoni Jijini Dar ambapo alisema kuwa dunia imemfanyia kitu kibaya na hafahamu nini kimetoka katika maisha yake.

Mr Nice alisema kuwa anashindwa kuelewa kwa nini maisha yamempiga kiasi hicho kwani pesa yote aliyokuwa anaipata alikuwa anaipata kwa jasho lake" Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu kwani sikuwahi kumdhurumu mtu wala kuiba cha mtu pesa yote nilikuwa naipata kwa hali naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu" Alisema mwanamuziki huyo

Aidha mwanamuziki huyo anasema" Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini pesa hizo zilitokana kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama Marekani, Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, Afrika Kusini na kwingineko na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana"

Alisema Hata hivyo Mr Nice nasema kuwa hizo ni nchi za mbali lakini bado shoo za alizokuwa anazifanya nchi za Kongo, Zambia, Uganda, Rwanda, Kenya na moja ya shoo ambayo akiikumbuka huwa inamtoa machozi ni ile ya nchini Rwanda ambayo siku anashuka Airport alikuta kitu cha kushangaza sana. Anasema alikuta umati mkubwa wa watu ukimsubiri pamoja na Waziri wa Michezo wa nchi hiyo pamoja maofisa wa ngazi za juu wa Polisi na Jeshi huku kukiwa na Red Capet kisha akapigiwa saluti huku akisindikizwa na mizinga ishirini na moja.

Hata hivyo mwanamuziki huyo anasema alifikia uamuzi wa kujiita the milonea Mr Nice baada ya kuingia mkataba na kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Safari alifanya shoo mikoa yote ishirini n tano kwa pesa ndefu na kufanya kuwa mwanamuziki mwenye pesa nyingi Afrika Masharki kuliko mwanamuziki yeyote.

Mambo mengine ya kushangaza aliyokuwa nayo mwanamuziki huyo kipindi akiwa na pesa ni juu ya msafara wake uliokuwa umejaa wapambe wengi na kulazimika kutumia magari zaid ya nane kwenye mizunguko yake huku yakiwa hayazimwi Ac masaa ishirini na nne hata kama hayana watu ndani.

Aidha Mr Nice alimaliza kusema kuwa anawashauri wanamuziki wa sasa kujifunza kwa waliopita ili nao yasijekuwakuta kama yaliyowakuta wao.
 
wadau mnasemaje kuhusiana na wasanii wetu.
 
bado ana kazi ngum sana ya kutengeneza watu wa kumlilia akiwa hai,

kijana ana akili sana ya kutengeneza pesa pamoja na kutengeneza jina ili ku-maintain status yake

jambo la msingi sasa kwa vile walishaona yaliyomtokea mr nice, basi ajifunze kutoka kwake,

la sivyo diamond atakuwa zaidi ya mr nice.
 
yaan pangetolewa fungate ya ban, ngekukimbusha wajibu wako kwa masingi, unaquote habari nzima kwa comment hyo, utatujazia nafasi kif@l* hvo, huna adabu...

Halaf jibu fupi kweliii lol hahhhhahhha
 
Pesa inahtaji nidhamu,kwa kila mtu mahala popote na si wasanii tu,just imagine leo mtu anafanya kazi sehemu fulani lakini hajui umuhimu wa kutunza akiba(saving)japo hata 10% of his/her paycheck,siku akipunguzwa au akifukuzwa kazi anaishia kuwa omba omba,so ni muhimu kuwa na saving na ku-invest in the wise investment,haitakiwi tuwe na matumizi mabaya ya pesa kama pesa haiwezi kujizungusha,alafu tusipende kumsingizia mungu kila kitu we must take 100% for our life,kama hatutabadilika tutaishia kulalamika sana!
 
Akili ni nywele 2mwache aendelee kupaka bleach
 
Hatutaki mambo ya nilikuwa hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…