Diamond platnumz, baba ni baba tu, rudi kwa baba yako

Diamond platnumz, baba ni baba tu, rudi kwa baba yako

Lakini hata kama wazazi mnaachana, jaribu kuwa karibu na watoto wako, msaidie mwanao, kwa sababu watoto wanaona na ingawa pain.mimi kwa upande wangu mpaka Leo,najaribu kuwa na upendo kwa babaangu ila nashindwa, hata kama walikuwa na matatizo wenyewe wazazi,watoto hawastahili kuadhibiwa, hasa ukiangalia baba ana uwezo,matokeo yake ukikua mapenzi yote unayahamisha kwa mama

Nikweli ila kinachowaumiza wamama wengi wanaachana ila baba hajumuiki kwenye kuchangia huduma zozote za mtoto mpaka unakua unashindwa kupata elimu bora kisa baba na unajua ana uwezo fika wa kukusaidia kikubwa wababa hata wakitengana na wamama wasiache kutekeleza majukumu yao kama baba ili watoto nao wajue umuhimu wa baba
 
Uko sawa mtani huyu baba diamond alikuwa amelewa sana hata kujieleza ni shida.clouds inabidi wawe na mipaka ya hizo interview zao maana kama nia yao ilikuwa ni kumuhoji wangesubiri akiwa sawa. Vinginevyo ni kutaka sifa za kijinga zisizo na maana.
Hakuna siku walio nikera Clouds kama jana na walio kuwa wana muhoji walikuwa wanajua kabisa Baba Diamond kalewa halafu walionekana kabisa wanamfanya kama Toy kwakweli walimdharirisha sana maana maneno aliyo kuwa ana ongea kwakweli ina shangaza!

Halafu walinishangaza kumuuliza mahusiano yake na Mama Diamond wakati walijua huyu mtu kalewa lazima aseme vitu visivyo faa...mara aka anza kusema sijui mama Diamond alikuwa na bwana nje..kwakweli Clouds walikihuka sheria ya faragha kabisa!

Na mtu mwenyewe alikuwa ana jichanganya sana mara aseme wako poa na Diamond na ana msaidia mara aseme Diamond hampigii simu...!

Ifike wakati Media ziwe na mipaka maana kufanya vile ni uchonganishi na sijui wao wana faidika nini? Nina hakika Baba Diamond akienda kuhojiwa sasa hivi hawezi kuongea alivyo ongea kwenye TV...huu ulikuwa ni udhalilishaji kwa Diamond,Baba Diamond na Mama Diamond.
 
Diamond mwisho wake mbaya sana atakuja juta amzarauye babaye maisha yake ni kama tone la maji huwezi kujua mapenzi ya baba yako na mama yako yaliingia dosari gani kwa mwanaume mwenye akili hayo mambo usiyaingilie unatakiwa uyakwepe usukubali kujumuishwa humo inahitaji akili sana sababu ni rahisi sana kwa mama kumwaminisha mtoto mabaya ya baba yake kuliko baba kumwaminisha mtoto
Msipende kuwa wepesi wa kutoa lawama kwa vitu msivyovijua. Hakun hata siku moja Diamond amewahi kueleza kwa undani chanzo cha yeye kutokuwa karibu na baba yake. Ile uweze kusuluhisha mambo ya familia ni sharti uwe na taarifa sahihi kutoka pande zote mbili. Na kwa sababu mambo ya familia ni masuala ambayo ni personal na private ndio maana Diamond hataki kuyaongelea hadharani. Ni kwa mantiki hiyo hiyo hata huyo baba yake Diamond anakosea kuyaongelea kwenye media. Na anapaswa ajue kwamba kama siyo umaarufu wa Diamond basi hata hizo airtime anazopata kwenye media zisingekuwepo. Kuongelea ishu za kifamilia kwenye media kuna madhara makubwa hasa kwa mtu kama Diamond. Ni vyema badala ya kukaa na kumponda Diamond au badala y kumuonea huruma huyu baba, tumshauri aache kupeleka mambo ya familia kwenye media, badala yake atafute wasuluhishi wakakae pande zote mbili na kila mtu alitoe lililopo moyoni mwake.
 
Tena Diamond ana huruma sana!!

Huyu mzee angetakiwa awe jela kaolewa na nyapara flan amazing atulie kabisa!!
Yaani umfanyie hivyo mtu aliyejipinda usiku kucha ili wewe utokee?!! Kama unasoma vitabu vya Mungu, fanya hivyo uisikilizie LAANA yake. Pumbavu!
 
TATIZO La WATANZANIA Kupenda Kuweka Mbele Chuki Zetu BINAFSI Ktk Issue Sensitive!! KWANI Wkt Huyo Mzee Anakula Raha Na Kushindwa KUWAPATIA Msaada Walau Wa Yale Mahitaji Muhimu Kwa BINADAMU, Alizuiwa Na Nani!!?? HIVI Angekuwa Amekubali Kuwa Yeye Ndiye Baba Mzazi Wa Diamond Na KUKUBALI Kumtunza Mtt Wake, Hata Kama Walikosana Na Mzazi MWENZAKE, NANI Angemzuia Kutoa Matunzo Kwa Mtt Wake!!! LKN Yeye Alikwepa Majukumu Ya Kumtunza Mzazi Akiwa Mjamzito Na Hatimaye Mtt!! AKAENDELEA Kula Bata Tu, Na Nilivyomuona Na Kumsikia Ni MHUNI Wa Mjini Tu!! Maneno Ya KISELA Tu!!! So Ameleta USELA MAVI!!! PIA Kama Diamond Angekuwa Hana AKILI Za KUONA Na KUFAHAMU, Kuwa Babake Yupo Hai Na UWEZO Kiuchumi Tu!! MBAYA Zaidi Ni Pale Mtt Anaposhindwa Kupata Hata VIFAA Vya Shule Na Chakula!!! HUKU Ukiambiwa Babako Yuko Hai Tu Na Ana Kauwezo!! ILA Waliwakataa Tokea Mimba Hadi Leo Hii!! Mtt / Wtt Wanaona Mama Yao Anavyotaabika Kuwalea!! LEO Baada Ya Mtt KUPATA MAFANIKIO KWA UWEZO WAKE MUNGU, ETI Baba Ndio ANAJITOKEZA Na Kusema Mi Ndiye Babake!!! PUMBAVUU!!!! WKT Ule Life Taiti Ulikuwa Mbali, Ila Kipindi Cha Neema Unajitokeza!!!!! ALAFU Unataka Upatiwe Huduma, Ambazo Ww Ulizikimbia Kuzitoa!!! ALAFU WATANZANIA Kwa CHUKI BINAFSI Tu, Wanamuona Mtt Ndiye Mshenzi!!!! MTAKUWA Hamtendei Haki Diamond Na Wtt Wooote Waliokataliwa Na Baba Zao Tokea MIMBA, Hadi Walipopata Mafanikio!!!! UZURI Yule MSELA AMEKIRI Mwenyewe, Kuwa Ktk Issue Za Kuwasiliana Na Kumpatia PESA Halina Tatizo, Diamond Analifanya!!!! JE Ww Ulitaka Diamond Afanye Lipi Zaidi!!!!?? ACHENI CHUKI ZENU BINAFSI, KTK ISSUE SENSITIVE!! WATU Wengi Wanafanya Huo UJINGA Alafu Wanakuja KUOMBA MISAADA KWAO!!!!

Daaahh kunywa pepsi barrriiidiiiii nakuja kulipa! Umeongea ukweli mtupu.

Hawa wababa wanaotelekeza watoto na wawajibike kwa matendo yao maana hakuna namna. Iwe fundisho na kwa wengine!
 
Hili la kusamehe ni la mtu na mtu ingawa tunaambiwa forgiveness is easy for the people who are ready to forgive huwezi jua na pia maelezo yana changanya mara wapo uzuri mara kuna figisufigisu sijui lipi sahihi?
 
Mleta mada na wadau wengine mliochangia hadi hapa,hivi baba yake Diamond anaitwa Mzee Platnumz?
Clouds ndo walimtamtambulisha hivyo, hadi ktk screen waliandika interview na mzee platnumz. Sio sisi.
 
Msipende kuwa wepesi wa kutoa lawama kwa vitu msivyovijua. Hakun hata siku moja Diamond amewahi kueleza kwa undani chanzo cha yeye kutokuwa karibu na baba yake. Ile uweze kusuluhisha mambo ya familia ni sharti uwe na taarifa sahihi kutoka pande zote mbili. Na kwa sababu mambo ya familia ni masuala ambayo ni personal na private ndio maana Diamond hataki kuyaongelea hadharani. Ni kwa mantiki hiyo hiyo hata huyo baba yake Diamond anakosea kuyaongelea kwenye media. Na anapaswa ajue kwamba kama siyo umaarufu wa Diamond basi hata hizo airtime anazopata kwenye media zisingekuwepo. Kuongelea ishu za kifamilia kwenye media kuna madhara makubwa hasa kwa mtu kama Diamond. Ni vyema badala ya kukaa na kumponda Diamond au badala y kumuonea huruma huyu baba, tumshauri aache kupeleka mambo ya familia kwenye media, badala yake atafute wasuluhishi wakakae pande zote mbili na kila mtu alitoe lililopo moyoni mwake.
Umeongea ukweli mtupu na mimi nafikiri kama kweli watu walikuwa wana nia njema wasinge kwenda kumrekodi mtu tena aliye lewa aongee mambo ya ndani ya familia!

Baba Diamond ukimsikiliza utagundua ana matatizo yake lakini Baba ni Baba japo swala la kupeleka mambo kwenye vyombo vya habari yana haribu zaidi!

Kama Diaomond na wengine waliangalia lazima mambo yatakuwa yameharibika zaidi!
Na mimi hapa ndipo na walaumu Clouds maana ni wazi wao ndio walimtafuta na walijua alikuwa amelewa!
 
kwani kusamehe ni hiari au lazma? kma ambavyo huyo baba hakulazimishwa kumlea akafanya yake sasa amuache mondi afanye yake akijisikia atamsamehe asipojisikia basi akitulize kma mwanae alivyokituliza alipo telekezwa asimsumbue kbsa mxiewww sipendi watu opportunists mimi wakiona hela ndio wanakumbuka msamaha yaan sku zote hzo asiombe msamaha asubiri kafanikiwa ndio ajue alikosea kwendaaa
 
Kwenye U Heard Soudy Brown yuko na Baba yake Diamond Platnumz Abdul Juma akielezea mkasa mzima uliosababisha akaikimbia familia yake kipindi wanaishi wote.

Baada ya kuulizwa kwanini aliikimbia familia Baba Dimond anasema “niliondoka kwao kama saa tisa usiku, ogopa sana mboga yako umeipika alafu hujui nani kakuwekea chumvi..lakini ukija kujua mtu aliyekuwekea ni hasira”

Jambo gani ambalo limewahikuongelewa kwa Diamond na likamchukiza? “Watu wanaposema kuwa Diamond hanisaidii.. wakati mimi ananisaidia, sasa hivi nikitembea watu wananinyooshea vidole kuwa natembea pekupeku.. mimi najisikia simple “

U HEARD FEB 5
 
Ni wanawake wangapi wanatelekeza, kujiuwa au kuwauwa watoto baada ya maisha kuwa magumu kutokana na baba kukimbia?

Mzee Abdul inasemekana hakumlea Naseeb kabisa! Muda huo hakuwa na Bi radhia, alikuwa na kambi nyingine nadhani ni kwa mama wa Queen darlin. Si kwamba hakuwa na uwezo, alikuwanao ila ni ujinga wa wanaume wengi kupuuza majukumu yao. Diamond alisema hata baada ya kukua kidogo, alijaribu hata kumfuata baba yake kumuomba pesa ya shule lakini alitimuliwa.

Wakati huo maisha yalikuwa magumu nyumbani, na msaada pekee aliokuwanao ni Mama, licha ya magumu yote huyu mama alihakikisha kwa kila awezalo mwanae aishi maisha ya kawaida apate hata kusoma, walidiriki wote kulala chumba kimoja, ili kingine wapangishe ipatikane pesa ya shule.

Leo hii moja ya vitu anavyopondwa sana diamond ni kutokuwa na shule ya kutosha, na kiukweli angekuwa nayo ingempa advantage zaidi, yote haya akikumbuka kuwa mzee alikuwa na uwezo ila hakutaka kumsaidia kama mwanae inamuuma sana.

Huyu mzee alikuwa akifahamu diamond anaishi tandale miaka yote hiyoo, ila hakumtafuta amekuja kufanya maamuzi hayo baada ya maisha take kukaa vibaya afu diamond amekuwa star mkubwa Tanzania, yani hapo ni full drama ni sawa na demu aliokuwa anakukataa afu umepata mkwanja anakushobokea unakuwa na mawazo mawili (ametambua unamfaa we we kama wewe, au pesa ulizonazo)

ILA AMEFIKIA HATUA YA KUMSAMEHE, YEYE ALILIONGEA HILO NA BABA AMELITAMKA HILO NA NI KITU KIZURI...

Kinachokuja kutokea ni kwa kiasi kipi mzazi atakuwa karibu na mwanae, tumuachie mwanae Naseeb afanye maamuzi yake ila tu itakuwa poa kma watazidi kuwa karibu zaidi na kuonana Mara kwa Mara.

Na uzuri wa hii hali, ni kuwa inatoa fundisho kwa wanaume suruali, tabia zao za kojo kojo kama jogoo afu unamuachia tetea alee pekeyake, UJINGA MTUPU..!!
 
Diamond mwisho wake mbaya sana atakuja juta amzarauye babaye maisha yake ni kama tone la maji huwezi kujua mapenzi ya baba yako na mama yako yaliingia dosari gani kwa mwanaume mwenye akili hayo mambo usiyaingilie unatakiwa uyakwepe usukubali kujumuishwa humo inahitaji akili sana sababu ni rahisi sana kwa mama kumwaminisha mtoto mabaya ya baba yake kuliko baba kumwaminisha mtoto
That is a point!! Mama hawezi kusema yeye ndo chanzo cha mzozo..
 
clouds TV mafala wamekosa vipindi.Huyu muandaaji wa kipindi next time afanye interview na baba/mama yake mzazi tujue kuwa hasumbuliwi na wivu/njaa....!
 
TATIZO La WATANZANIA Kupenda Kuweka Mbele Chuki Zetu BINAFSI Ktk Issue Sensitive!! KWANI Wkt Huyo Mzee Anakula Raha Na Kushindwa KUWAPATIA Msaada Walau Wa Yale Mahitaji Muhimu Kwa BINADAMU, Alizuiwa Na Nani!!?? HIVI Angekuwa Amekubali Kuwa Yeye Ndiye Baba Mzazi Wa Diamond Na KUKUBALI Kumtunza Mtt Wake, Hata Kama Walikosana Na Mzazi MWENZAKE, NANI Angemzuia Kutoa Matunzo Kwa Mtt Wake!!! LKN Yeye Alikwepa Majukumu Ya Kumtunza Mzazi Akiwa Mjamzito Na Hatimaye Mtt!! AKAENDELEA Kula Bata Tu, Na Nilivyomuona Na Kumsikia Ni MHUNI Wa Mjini Tu!! Maneno Ya KISELA Tu!!! So Ameleta USELA MAVI!!! PIA Kama Diamond Angekuwa Hana AKILI Za KUONA Na KUFAHAMU, Kuwa Babake Yupo Hai Na UWEZO Kiuchumi Tu!! MBAYA Zaidi Ni Pale Mtt Anaposhindwa Kupata Hata VIFAA Vya Shule Na Chakula!!! HUKU Ukiambiwa Babako Yuko Hai Tu Na Ana Kauwezo!! ILA Waliwakataa Tokea Mimba Hadi Leo Hii!! Mtt / Wtt Wanaona Mama Yao Anavyotaabika Kuwalea!! LEO Baada Ya Mtt KUPATA MAFANIKIO KWA UWEZO WAKE MUNGU, ETI Baba Ndio ANAJITOKEZA Na Kusema Mi Ndiye Babake!!! PUMBAVUU!!!! WKT Ule Life Taiti Ulikuwa Mbali, Ila Kipindi Cha Neema Unajitokeza!!!!! ALAFU Unataka Upatiwe Huduma, Ambazo Ww Ulizikimbia Kuzitoa!!! ALAFU WATANZANIA Kwa CHUKI BINAFSI Tu, Wanamuona Mtt Ndiye Mshenzi!!!! MTAKUWA Hamtendei Haki Diamond Na Wtt Wooote Waliokataliwa Na Baba Zao Tokea MIMBA, Hadi Walipopata Mafanikio!!!! UZURI Yule MSELA AMEKIRI Mwenyewe, Kuwa Ktk Issue Za Kuwasiliana Na Kumpatia PESA Halina Tatizo, Diamond Analifanya!!!! JE Ww Ulitaka Diamond Afanye Lipi Zaidi!!!!?? ACHENI CHUKI ZENU BINAFSI, KTK ISSUE SENSITIVE!! WATU Wengi Wanafanya Huo UJINGA Alafu Wanakuja KUOMBA MISAADA KWAO!!!!
Wewe una uhakika gani baba yake alimkataa? Msipende kuingiza hisia kwenye mambo ya ndani
 
Yaani umfanyie hivyo mtu aliyejipinda usiku kucha ili wewe utokee?!! Kama unasoma vitabu vya Mungu, fanya hivyo uisikilizie LAANA yake. Pumbavu!
KWELI Ww Mgonjwa!! KITABU Gani, Cha DINI Ipi Na MUNGU Yupi Huyo!!! AMBAYE Anatoa Au Anabariki LAANA Kwa Mtt Amekataliwa Na Kutekelezwa Mzazi Ambaye AMEKIMBIA Majukumu Yake!! MUNGU Anayemuabudu Mi, Najua Malezi, Matunzo Na Mahitaji Mengine Ni JUKUMU Na WAJIBU Wa Mzazi, Wala Si Hisani!! SIO Kuweka Mbegu Tu Na Kukimbia!!! HATA Shamba Ukilima Na Kupanda Mbegu, Lazima Upalilie, Uweke Viuatilifu, Umwagilie Maji N.k .Ndipo Uje Kuvuna MAZAO Yako!! KAMA Utashindwa Kufanya Hivyo, Umeishia Kupanda Tu, Ukalitelekeza Shamba. MATOKEO Yake Mazao Yamekuwa Kwa SHIDA!! MATOKEO Uje Kudai MUNGU Akulipe Fidia Ya Mbegu Ulizopanda!!! HAKUNA MUNGU Wa Aina Hiyo!! NA UPAMBAVUU MKUBWA KUDHANI, MUNGU ANABARIKI LAANA ZA KIJINGA HIVYO!!!! KAMA Haujui Hilo, Jaribu Kuwauliza WATU Wakubwa Zaidi, JE, LAANA Ya Mzazi Wa Aina Hiyo MUNGU Anaibariki!?
 
Back
Top Bottom