Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

Usingemjibu huyo mpuuzi ukute Yuko shamba mkoani diamond amamuona kwenye tv.

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Hawa ni wafanyabiashara ya madawa ya kulevya halafu unamwita ''icon''? Karma is bitch, acha na yeye yamkute. Unadhani fedha yake ni matokeo ya muziki tu?
 
Kuna watu wengi wataona ni vigumu sana kufanya kitu sahihi hapa, ambacho ni kumhurumia Diamond kama mgonjwa/victim.

Kwa sababu jamii yetu inaangalia pesa kama kila kitu. Yani ukiweza kupata pesa tu, unaonekana mjanja.

Sasa watu wanamshangaa Diamond, imekuwaje amepata ujanja wa kupanda ngazi kwenye usanii wenye competition sana, halafu ashindwe kuji control kwenye madawa ya kulevya?

Ukiangalia hili jambo ni tatizo dunia nzima. Ni kama vile wasanii wanapata pressure sana kuwa creative na kubaki on top, wanapata pressure kuandikwa sana, tunawaingilia maisha yao binafsi sana kama tunawajua personally wakati hatuwajui kihivyo, mwishowe wanaji boost kwa madawa kama coping mechanism.

It is very hard to argue for sympathy for Diamond, kama mtu, kama mgonjwa, kwa sababu jamii yetu inaangalia umasikini wa fedha kama ndiyo tatizo kubwa, haiangalii umasikini wa akili na mambo yanayohusu afya ya akili kama tatizo.

Mimi nilikuwapo katika watu walioanzisha Bongoflava siku hizo, ila niliamua kutoendelea huko, kwa sababu niliona gharama ya u star kwenye kutokuwa na privacy.

Hili ni jambo kubwa sana ambalo watu wanalichukulia poa tu.
 
Kiuno bila mfumo



Huyu ni Ray sii

Sent from my Pixel 5 using JamiiForums mobile app
 
Kunae ndg yangu kwa upande wa baba mkubwa, ni muhanga wa hii kitu, uso kwa uso nimekutana nae mwaka huu mwanzoni, mazee nililia kwa uchungu kwao kuna kila kitu ila ndo hivyo akienda mama yake mzazi na deko zote anamtimua akalale nje anamuhofia asimuibie vitu vyake, na ndie firstborn, ilibidi niwapigie simu usiku huo kuwashukuru walionilea hata km ilikuwa kwa mateso na masimango ila kwa dhati niliwashukuru sana
 
Habari zinazo ongelewaga na upande mmoja tu na mostly ni wale wanao mchukia since day one wamekaa wanasubiri ashuke
ha ha ha haaa
Chanzo ''Dada Mange kasema"
 
Pole sana mkuu.

Natumaini hata nje mnamfuatilia na kumpa support dada yenu.

Mimi kwa kawaida ni mtu wa "live and let live". Basically "kila mtu mzima aubebe msalaba wake mwenyewe".

Na nilipoanza kusoma huu uzi nilipata hisia hizo, nikaona hii ni kama obsession na celebrities.

Ila, nilivyozidi kufikiri zaidi, nikapata picha ya tatizo kubwa zaidi kijamii. Kwamba Diamond anavuma kwa sababu ya umaarufu wake tu, lakini wako wengi.

Kuna namna za kulikabili hili tatizo kimkakati na kimfumo. Mfano, haya madawa yanaingiaje? Nani anahusika?

Kuna wafanyabiashara na watu wakubwa tu wanaoshiriki. Kwa nini hawadhibitiwi?

Unajua mambo mengine ni ya kimazingira tu, ukiwa katika mazingira ambayo pombe ipo nje nje kila siku, ni vigumu kukaa bila kunywa, madawa ya kulevya nayo ni hivyo hivyo.

Tukiweza kudhibiti biashara ya kuingiza madawa ya kulevya nchini, hapo tutakuwa tumepiga hatua kubwa.

Tukishindwa hapo, huku chini lazima kuwe na victims tu, na katika hao victims ndugu zetu na watu wanaotuhusu kwa njia moja au nyingine hawatakosa.
 
Wewe jamaa mbona unaonekana una akili zako tu?
Yani unataka kusema Diamond ana majukumu kuliko tajiri wa Dunia Elon Musk?
I rest my case!
Uwe muelewa basi, nani kasema ana majukumu mengi kuliko Elon? Nimesema mazingira ya kazi ya Diamond na Elon ni tofauti, Diamond ana mazingira magumu ya kazi kuliko Elon, katikati ya wasafi festival Diamond alisafiri kwenda Marekani kama sikosei mara 2 ndani mwezi mmoja. Sasa hapo unazijua changamoto za usafiri kati ya Elon na Diamond alaf bado arudi ajiandae wasafi festival?

Hao wasio tumia madawa ata kutumbuiza kwa masaa zaidi ya 2 kwenye stage na kwa nguvu km ya Diamond wanaweza?
 
Watu tofauti wana historia tofauti, uwezo tofauti kustahimili mambo, privileges tofauti, etc.

Hivyo si sawa kuwalinganisha.
 
Kwa hiyo ww ndiye mwenye akili sana kuliko wabia wa Diamond kibiashara eg Pepsi na airtel kuwa balozi wao ni teja ila wakae kimya.

Em jaribu na ww kuwa uraibu kwenye kazi zako alaf uone mambo yatanyooka km ya Diamond. Akili za kuambiwa changanya na zako na usiwe km dodoki unachota kila kitu ata kwenye maji taka.

Huyo chid aliyekuwa akitumia madawa ya kulevya au mtu mlevi km chilla vp kwenye stage walikuwa na nguvu km Diamond?
 
Asante.
 
Watu tofauti wana historia tofauti, uwezo tofauti kustahimili mambo, privileges tofauti, etc.

Hivyo si sawa kuwalinganisha.
Sijafananisha attitude au perception ya mtu, nimefaninisha mazingira ya kazi note that.

Kabla ya Diamond lini uliona mwanamuziki wa kibongo amekuwa nominated for BET? Ila kwa nigeria ata upcoming ni rahisi kwake kupata hiyo fursa eg tems na sbb kubwa ni mazingira ya kazi yao ya Sanaa yapo juu kuliko ya yetu ya bongo na ndio maana kwenye tuzo kila siku tunamsikia Diamond tu kwann
 
Mie mtu akila Ngada simuonei huruma, Madogo wanasnif sana tu siku hizi ,wala hawajifichi
Mkuu hata wewe ungekuwa katika mazingira fulani na una baiolojia fulani ungekula tu.

Wakati mwingine huwa tunajiona wajanja kuepuka mishale fulani, wakati kiukweli hatujaiepuka mishale, ni mambo ya bahati tu, umezaliwa na wazazi fulani, ukapita njia fulani, umefikia hapo ulipofikia.

Ungepitia njia tofauti, hata kwa ajali ya kuzaliwa tu, inawezekana sana tu na wewe ungekuwa muhanga wa ngada.

Yani kuna watu wana DNA zinazowafanya waweze kuwa wahanga wa ngada kuliko wengine. Yani ile kuzaliwa na hizo DNA tu ni tatizo. Sasa hapo unaweza kumlaumu huyo mtu kwa sababu yeye kala mgada na wewe ambaye huna hizo DNA hujala?

Kwa hiyo usijione kuwa wewe umeweza kushinda vita kwa nini wao hawajaweza.

Inawezekana ukawa unamlaumu mtu wa Gaza kwa nini kapigwa bomu hajakwepa, wakati wewe uko Dar kwenu hakuna mabomu.
 
Bro mie nimepoteza madogo zaidi ya watatu kwa Ngada, akiwemo Langa, D Roby na wengineo ,maeneo ya Msasani /oysterbay ,mikocheni

Uzuri nimekaa na wauza Ngada na wavutaji, kuna madogo waliingia ktk ngada ile kujifanya wanyamwezi ,wakishua ,wako juu , kumbe wanapotea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…