Diamond Platnumz badili mwenendo before it’s too late!

So what is your point?

Diamond anatumia madawa ya kulevya kwa sababu ya mazingira ya kazi?
 
Nisingeweza kusema zaidi, asante Mkuu Kiranga
 
Kwa msanii husasani hawa wa bongo kwanza wote wanatumia vilevi eg pombe kali sbb kubwa ni makundi na kupata ujasiri kwenye kazi.

Kupanda kwenye jukwaa kwa zaidi ya saa 1 na watu wakushangilie tu sio kazi rahisi
Sawa sawa ,wengine kuiga tu, uzuri nimeishi hayo mazingira ya uuzaji na uvutaji ngada , hawa wasanii wengine wafuata mkumbo

Sasa kama Diamond anakula unadhani chawa wake itakuaje? Si watafuata mkumbo
 
Hilo lilitakiwa kukufanya uwe na empathy/sympathy zaidi kwa hawa watu.

Nashangaa unavyosema huna hurumankwa hawa watu wakati kwako hili si jambo abstract una mifano ya watu wa karibu.

Watu waliosoma kwa undani haya matatizo wanasema uraibu ni ugonjwa.

Inawezekana tusiuone kuwa ni ugonjwa kwa sababu ninugonjwa wa kisaikolojia zaidi.

Sasa unachofanya hapa ni kusema kwamba huna hurumankwa mgonjwa.

Ni sawa na kusema kwamba humuonei huruma mtu anayeumwa Malaria.
 
Dah! Ile heshima yote niliyokupa nimeiondosha!

Yani kwamba Elon Musk ana mazingira rahisi ya kazi kuliko Diamond? Hivi unajua unamuongelea tajiri namba 1 wa Dunia nzima?
Mtu mpaka kufikia kuwa tajiri namba moja awe na mazingira rahisi ya kazi? Acha tu huko kumfananisha na Diamond.

Basi, mjadala wetu umekwisha.
 
Tukikuita uthibitishe haya uliyoyaandika utaweza kuthibisha?
 
Sasa ww nikuulize swali mazingira ya kazi ya Elon unayafaninisha na ya Diamond? Kumbuka Tz ni nchi inayoendelea ila huyo Elon nchi yake ilishaendelea, je?

Katika utendaji kazi wa kila siku bwana Elon ana vitu wezeshi vingi tena vyenye teknolojia kubwa kuliko ata Diamond mfano ishu ya bandari na Dp, watu wa Dp worldwide wanadai wana mifumo wezeshi kuliko ss wa Tz so ata wakifanya kazi nyingi kwa siku energy wanayotumia inakuwa tofauti na mamlaka husika za bandari wangefanya the applied to Diamond na Elon.

Siwezi kumfaninisha Elon na Diamond maana Elon ni safari nyingine na ndio maana nasema majukumu ya ki ukurugenzi na msanii ndio vinamfanya tumuone Diamond km mnavyodai nyie
 
Fatilia mtiririko wa hoja usidakie vitu kwa juu
Mtiririko wa hoja kutoka wapi? Wewe ndiye uliyeshindwa kuonesha post hii ilitoa hoja hii.

Mpaka sasa unaonekana kama mtu unayesema uongo kwamba kuna hoja ulitoa wakati hujatoa.

Ndiyo maana huwezi hata kuweka ushahidi wa link au post namba kwamba post hii nilitoa hoja hii.

Nitafuatiliaje mtiririko wa hoja hapo sasa?

Siamini kama una mtiririko wowote wa hoja, thibitisha hilo kwanza kwa kutoa posts na namba zake na links.
 
Kabisa kabisa
Sasa inakuwaje unakosa huruma kwa mgonjwa?

Unasema umewaonya na hawakusikilizi, unajuaje unapowaonya wana will power ya kukusikiliza na kushinda huo ugonjwa wa akili?

Unajuaje kuwaonya tu kunatosha?

Ukikutana na mtu ana homa ya Malaria unaweza kusema huna huruma kwa mtu mwenye ugonjwa wa Malaria?

Ukikutana na kichaa anaokota makopo uchi, unaweza kusema kuwa huna huruma na mtu mwenye ugonjwa wa kichaa?
 
Mkuu basi endelea kudakia vitu kwa juu
 
Kusafiri mara mbili kwa mwezi kwenda Marekani ni mazingira magumu? Unajua Elon anasafiri mara ngapi kwa mwezi?

Kwani Chid Benz, TID au Lord Eyez walikuwa wanatumbuiza kwa muda wa saa ngapi jukwaani? Huku wakitumia dawa za kulevya?

Ondoka kwenye fikra za kutafsiri uwezo wa kutumbuiza muda mrefu, kuwa siyo utumiaji dawa za kulevya. Iko tofauti.

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…