Diamond Platnumz bado ni mshamba sana

Kwamba hata Akina Michael Jackson waliimba nyimbo za maisha? Kwann Michael na siyo Kiba au davido?

Hata Akina Beyonce? Kwann Beyonce na siyo shilole na ruby?

Ndo ujue Mondi yuko anga zingine kabsa
 
Kwanini unayoona makosa kwa Diamond usifanye wewe au Diamond ndio Binadamu wewe Funza.
 

Bro, soma hoja zangu za kwanza, wapi nimeongelea kipato? Nilikujibu vile baada ya wewe kuanza kulazimisha mada ibadilike.

Hili suala la kipato naliacha na sitaliongelea tena kwa sababu kipato cha msanii siyo alama ya umahiri wake na ni suala binafsi.
 
Mbona hoja zako Nishazijibu au kuna nyingine?

Hayo mawazo yako na chuki zako binafsi.Kwani wasanii wote waliotamba wana dance zao binafsi?

Hebu nitajie dance binafsi ya Burnaboy,Patoranking,2 face Idibia?

Eti,msanii hana jipya,hana jipya kwako,msanii na show zaidi ya 90 karibia kila mwaka,hebu nitajie wasanii watano tu Africa wenye utitiri wa show kama Diamond.

Makonda ana mchango gani katika kupeleka mziki wa Diamond mbele?

Mbona Steve Nyerere na Bongo movie kila siku wapo na Makonda lkn hamna hata mmoja aliyefikia level za Kanumba
.

Maswali yangi ww hata moja hujanijibu na nimekuuliza kutoka na ulivyo changia ktk huu uzi.

Kutumika vibaya kivipi ?
Kwani anaiba au anakula kwenu?
We mwenye maono alimsaidia msanii gani kufikia level ya Diamond?

Watu sahihi wataje?
Wamevumbua vipaji vingapi?
Je na hivyo vipaji vilifika level gani?
 
Kwamba hata Akina Michael Jackson waliimba nyimbo za maisha? Kwann Michael na siyo Kiba au davido?

Hata Akina Beyonce? Kwann Beyonce na siyo shilole na ruby?

Ndo ujue Mondi yuko anga zingine kabsa

Shilole yule mpishi? Hapa tunaongelea muziki bro. Davido nimemsema. Davido toka day 1 amemuacha Diamond mbali sana.

Asipoangalia atatokea dogo mmoja atampiga kikumbo labda wamfanyie fitna tu.

Diamond ana album ngapi mpaka sasa? Au mnadhani kwa kuwa soko lenu hili la Kariakoo lisioeleweka ndiyo na nje ni hivyo hivyo?
 

Show 90 wewe ni underground. Diamond kwa muda aliokaa kwenye game hakutakiwa kuwa mtu wa kukimbizana na show 90 bro. Siyo wivu au chuki ila ndiyo ukweli.

Najua hautanielewa ninachotaka kusema kwa kuwa wewe unaleta ushabiki.

Ila kama unavyosema kila mtu na life yake, au siyo?
 

Makundi ni kweli yanavunjikaga ila siyo haraka kama ilivyotokea kwa Yamoto. Makundi yanavunjika baada ya kufika kwenye peak na wanaaza kushuka.
 
Burna boy Dola 50000 per perfomance....Nimeanza na huyo embu nambie Diamond anacost sh ngapi?
Hiyo hela anayolipwa Burnboy sasa hivi Mondi alikuwa akilipwa 2017 .Kasome post namba 30 na 40 na nimeweka na reference.
 
Mimi na ww nani nani shabiki,nimekuwekea na Reference,ww hujaweka chochote zaidi ya maneno.

Wewe HATER.
 
Reactions: Qwy
Hiyo hela anayolipwa Burnboy sasa hivi Mondi alikuwa akilipwa 2017 .Kasome post namba 30 na 40 na nimeweka na reference.

We jamaa umekazania hela. Hivi unadhani kwa nini nimemtaja Makonda na CCM? Nionyeshe akifanya show Marekani au hii ya Ujerumani analipwa kiasi gani? Haya majadiliano ya mfuko wa mtu siyapendi ni basi tu. Tubaki kwenye sanaa.
 
Ungeweza kuandika kama ushauri ungekuwa umefanya kitu cha maana sana..
Lakini kumponda mtu ambaye ana mind business zake na hata hakujuwi na ikizingatia maisha yako ni magumu .. umeonekana bwabwa mbele za wanaume... Unaitwa mbeya na mwenye chuki.

Bado mawazo yako can be constructive kama utayatoa kama ushauri na si kijembe cha kike
 
Umleta Uzi matak* yako

Unamkataje raia mwenye doors mingi kama mond
 
We jamaa umekazania hela. Hivi unadhani kwa nini nimemtaja Makonda na CCM? Nionyeshe akifanya show Marekani au hii ya Ujerumani analipwa kiasi gani?
Haya sasa nipe sababu ya kumtaja Makonda na CCM na reference ya hicho unachokiongea.

Za US na Germany sijui,sababu sina reference,ila kwa mujibu wa Diamond sasa hivi anafanya show kwa dola 75000.

Maswali yangu hujayajibu.

Kutumika vibaya kivipi ?
Kwani anaiba au anakula kwenu?
We mwenye maono alimsaidia msanii gani kufikia level ya Diamond?

Watu sahihi wataje?
Wamevumbua vipaji vingapi?
Je na hivyo vipaji vilifika level gani?
 

Ushauri utakuja baadae ngoja kwanza tuwekane sawa. Wabongo hawatii sheria bila shuruti.
 
Wewe si mzima hebu msome huyu msanii hapo Ed kapiga show 260 ndani ya miaka miwili na nusu na nimegundua nabishana na asiyejua mziki ,usiku mwema .
 
Reactions: Qwy

Jiongeze bro. Kama unataka kujua utajua ila ukitaka ubaki na ubishi wako pia sawa. Diamond hawezi kulipwa hela hiyo nje ya ukanda huu. Show moja ya hapa na pale inaweza kutokea ila siyo wastani.

Kuhusu maswali yako ni kwamba mada yangu siyo mashambulizi binafsi. Dogo yuko vizuri na anajitahidi sana ukizingatia mazingira ya sanaa zetu yalivyo. Mimi ninaiangalia kwa level ambayo angeweza kuwa kama kasoro fulani zisingekuwepo.

Unajua wabongo huwa tunajipaisha sana na kujitia upofu halafu tukishindwa tunashindwa kujua wapi tumeharibu kwa sababu tulishajiona tuko juu sana.

Rudi issue ya The Lion King kwa mfano. Sikuifuatilia sana ila ningeshangaa sana kama wangetumia muziki wa Diamond. Sitashangaa kukuta BASATA huko wakawawekea fitna wasanii wengine wasitumike kwa sababu tu wahusika hawakutaka kumtumia D.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…