Themagufulianz
JF-Expert Member
- Apr 15, 2017
- 4,548
- 1,988
maisha yake hayakuhusu anyway... na hakuna sheria kwenye maisha binafsi ya mtu...Ushauri utakuja baadae ngoja kwanza tuwekane sawa. Wabongo hawatii sheria bila shuruti.
Jamaa kwanza kwenye uvaaji tu bado sana. Na tena afadhali ameacha kuvaa kofia za baridi wakati yuko Madale anatandikwa na jua kali, ilikuwa ni aibu.
Tuje kwenye uimbaji. Kila siku habari za mapenzi tena matusi. Hata kina Michael Jackson wameimba nyimbo za maisha kiujumla, yeye anataka kukaa kimya.
Tuje kwenye uchezaji. Diamond hajaweza kuwa na dance style yoyote iliyotrend Afrika. Kila siku anacopy style tena ambazo zimeshachoka.
Beyonce hakukosea. Bila nguvu za Makonda na CCM, Diamond ni kama Jux tu.
Inashangaza eti kuna mtu anamuweka level moja na Davido!!
Ningetoa ushauri ila sidhani kama utapokelewa kwa mikono miwili.
NYONGEZA: Sina chuki binafsi na Naseeb ila naona kipaji chake hajakitumia kikamilifu. Hana washauri wazuri. Washauri wenyewe nao sasa hivi wako busy wanagombania umaarufu huo huo.
Wewe si mzima hebu msome huyu msanii hapo Ed kapiga show 260 ndani ya miaka miwili na nusu na nimegundua nabishana na asiyejua mziki ,usiku mwema .
Tetesi: - Ed Sheeran Atangaza Kupumzika Muziki
MWANAMUZIKI maarufu duniani, Mwingereza, Edward Christopher Sheeran, maarufu kama Ed Sheeran ametangaza kuwa atapumzika kazi hiyo baada ya kuifanya kwa muda mrefu. Ametoa kauli hiyo alipokuwa anafanya hitimisho la ziara yake ya ‘Divide World Tour’ mjini Ipswich, Uingereza, baada ya miaka...www.jamiiforums.com
Kwa hiyo unamlinganisha Diamond na Ed Sheeran sasa? Ungezingatia yote niliyoyaandika kwenye uzi huu usingefanya hivyo kabisa.
Usisumbuane na huyu jamaa...We usiyedanganywa weka mkataba wa malip ya Diamond?
Tuambie sie tunaodanganywa.
Soma hiyo mchanganuo.NB 5mil Ksh ni zaidi ya milioni 100 za kibongo.
View attachment 1195959
"Show 90 wewe ni underground. Diamond kwa muda aliokaa kwenye game hakutakiwa kuwa mtu wa kukimbizana na show 90 bro. Siyo wivu au chuki ila ndiyo ukweli. "
Mziki hujui ww,msanii mkubwa lazima uwe na show nyingi kwa mwaka.
Mwalimu wako anatabu,imeandikwa wapi,ili uwe na tour ndefu lazima uwe umetoka kutoa album.Kawaida msanii anaenda kwenye tour ndefu akiwa ametoka kutoa album.
Kwa hiyo ukitoa ep na single moja hurusiwi kufanya tour?'Kawaida' umegeuza 'ili uwe'.
Ed Sheeran ametoa album 2017 na nyingine 2019, tour uliyoipost ilikuwa kusupport hizo album.
Basi nikutokana na definition yako ya ujanja na ushamba...Unaweza kuwa na hela ukawa mshamba vilevile.
Kwa hiyo ukitoa ep na single moja hurusiwi kufanya tour?
Kijana ukiona msanii anatoa single mbili au tatu alafu ana show zaidi ya 90 jua huyo sio wa kawaida,hizi tour hapangi yy ila mapromoto wanamuhitaji,sasa ww endelea kukalili,wenzako ndio wanapiga hela na hawana album.
USIKU MWEMA hii comment ya mwisho .
Kapumzike ndugu yang, huyu anabisha mpaka vinavyoonekana.Basi nikutokana na definition yako ya ujanja na ushamba...
Sasa mkuu unakuwaje mjanja halafu huna pesa... ujanja ni pesa.. ukiwa mjanja utapata njia ya kusaka hela..Unapingana na definition hiyo? Siku hizi tuna watu wengi mbona wa namna hiyo.