We jamaa inaelekea sio mfuatiliaji wa game! Ina maana umeshasahau au hufahamu Wasanii wa Kenya walivyolalamika kwenye show ya Mombasa baada ya Media za Kenya kufichua Mondi alilipwa KSH 5M wakati wasanii wa Kenya hakuna hata mmoja aliyekuwa amelipwa angalau nusu ya hiyo 5M. And man, hiyo ni 5M ya 🇰🇪 kwahiyo piga mwenyewe hesabu kwa pesa za madafu! Hadi Bodi ya Filamu ya Kenya na wenyewe wakaanza figisu kwamba Diamond analipwa pesa nyingi sana Kenya lakini hailipi kodi! Back in the days, huko huko Kenya ikatolewa orodha ya wasanii wanaolipwa mkwanja mrefu zaidi kupitia "COSOTA" ya Kenya! Hapo napo Diamond alikuwa at the top of everyone else including Kenyan Musicians! Na sio tu alikuwa on top of everyone bali pia aliwaacha mbali!
Ile kampeni yao Kenya ya last year ya PLAY KENYA na kuzuia Bongo Flavor iliwalenga akina Diamond kwa sababu wanapiga pesa ndefu Kenya kuliko Wakenya wenyewe!
Hata hapa Bongo, hivi ulishawahi kujiuliza kwanini alikuwa hapigi shows za ndani hadi ilipokuja Wasafi Festival?! In short, Promoters wa Bongo walikuwa hawafikii dau lake! Muulize Erick Shigongo atakueleza vizuri hili! Ungekuwa mfuatiliaji wa game, ungefahamu ama 2017 au 2016 Shigongo na Tale waliparuana sana! Kisa?! Malalamiko ya Shigongo kwamba Diamond anatoza pesa kubwa mno bila kujali kwamba hawatendei haki mashabiki wake wa TZ waliofanya afike hapo alipo! Malalamiko ya Shigongo yalikuja baada ya kumtaka Diamond kwenye show yake pale Dar Live, alipotajiwa price akakimbilia Instagram kulia lia! Kwa unafiki tu Shigongo akataka kuwatumia mashabiki kumbe lengo lake ni la mfanyabiasha yeyote yule!! Amlipe pesa ndogo msanii ili yeye avune maradufu!!