Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto na Nandy wahojiwa na Polisi kwa kusambaza video za faragha, wapewa dhamana...

Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto na Nandy wahojiwa na Polisi kwa kusambaza video za faragha, wapewa dhamana...

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mwakyembe amesema kuna baadhi ya wasanii ambao walianza kufanya uhuni ndani ya mitandao akiwemo mwanamuziki nyota wa muziki, Diamond ambae tayari amekamatwa na Jeshi la Polisi na anahojiwa kutokana na picha alizozungusha.

Pia Mwakyembe amesema pia imebidi binti Nandy naye akamatwe kisha kuhojiwa na wanaangalia namna ya kuwapeleka mahakamani.

Mwakyembe ametoa wito kwa vijana kuwa mitandao sio kokoro la kupeleka uchafu wote ambao umezuiwa na sheria zingine na nchi ina utamaduni wake ambapo inahitajika kulindwa kizazi cha sasa na cha kesho cha Taifa hili.

Akiuliza swali, mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alitaka kujua kauli ya Serikali juu kukithiri kwa ushoga na kutukana matusi mithili ya bomu la nyuklia ambayo sio maadili ya mtanzania na team za matusi ikiwemo za Wema, Zari, Diamond na Shilole.

Mwakyembe amesema sheria ya EPOCA ilitungwa mwaka 2010 lakini zilikosekana kanuni za kubana maudhui hasa upande wa mitandao. Amesema kanuni zimeshatungwa na zimeanza kufanya kazi.

 
Wadau kwema?

Asubuhi hii nimemsikia Waziri Dkt Mwakyembe akisema kua jana wamempeleka Msanii Diamond Polisi sababu ya kukiuka sheria za Mitandao, kuna mwenye more details about this issue?
 
Kwa mujibu wake Waziri Mwakyembe sasa hivi akijibu swali la Nyongeza la Mbunge Mlingwa huko Bungeni Dodoma.

Kwa kauli yake mwenyewe Waziri husika Dr. Mwakyembe amesikika akisema kwamba tokea jana Msanii Diamond pamoja na mwenzeke Nandy wamekamatwa na kwenda Polisi kwa Mahojiano zaidi kutokana na Video zao ambazo hazina ' maudhui ' ya Kimaadili kwa Watanzania.

Kazi ipo mwaka huu hakyanani.

Nawasilisha.
 
Domo naye kazidi kujitoa akili..acha wamshikishe adabu
 
unawezaje kumkamata mtu ambaye ana sauti kuliko wewe mwenye zamana... ana bishana na mawaziri kila leo... ana tokelezea ktk mikutano ya uzinduzi ya mh. yupo pamoja na DAB... una wezaje kumkamata huyo mtu kirahisi... kama sio kamchezo furani ni nini
 
Waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe, amesema msanii Diamond Platnumz alikamatwa jana kwa makosa ya kusambaza picha zilizokosa maadili mitandaoni na sasa anahojiwa na polisi.
Akizungumza bungeni leo Aprili 17, Waziri Mwakyembe amesema serikali imeshatunga sheria inayowabana wasanii na kudhibiti maudhui yasiyo na maadili mitandaoni.


Mbali na hilo Mwakyembe ameagiza msanii mwingine Nandi kusakwa na polisi akisisitiza kauli yake kuwa Tanzania siyo kokoro la uchafu.
Ametoa kauli hiyo wakati anajibu swali la nyongeza la mbunge wa Ulanga Godluck Mlinga aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani kukomesha tabia za baadhi ya watu wanaotumia mitandao vibaya ikiwemo kuhamasisha masuala ya ushoga.


Awali serikali ilitaja changamoto kubwa inayolikabili taifa ni athari ya utamaduni wa nje katika maadili, mila na desturi za Mtanzania kutokana na kuwepo na muingiliano mkubwa wa watu duniani.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Juliana Shonza wakati akijibu swali la mbunge, Nuru Awadh Bafadhili.


Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mkakati gani madhubuti wa kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanasimamia maadili.


Hata hivyo Shonza amesema kinacholeta shida hadi nyimbo kuwa hazina maadili ni tabia ya wasanii kutopeleka nyimbo zao kuhaririwa katika baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
 
Back
Top Bottom