Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Bahati mbaya huwa sisikilizi!
But for this,no way!
Najua basata wamesikia na watalifanyia kazi!

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Mkuu achana nae huyo haelewi chochote!
Yesu ni Mungu!

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Unajua kuwa alichookiimba Rose hakukitoa hewani?
Read the bible!
Wakristo sio wajinga!
Rose hajukurupuka huo ni mstari upo kwenye biblia!

Ney kwenye winbo wake hajamtaja Yesu,kamtaja mungu!
Sasa ni mungu gani anajua yeye coz kuna mungu wengi tu waliojifunua kwa namna tofauti na wanaabudiwa na biblia IPO wazi!
,ila Mungu in mmoja tu!
Ila angekua specific ni mungu yupi tungeelewa!

Sio kila anaetaja mungu,anamaanisha Mungu(Jehova) there s a big difference!

JESUS IS LORD[emoji120]
 
Ninyi mnaolalamika sio Wakristo wa kweli. Sisi Wakristu hatuhukumu mtu. Yeyote mwenye makosa atahukumiwa siku ya mwisho.
 
Wewe unajua kusoma?
Siku 40 kabla ya kupaa kwake mwaka gani?

Unaelewa kwamba kurudi kunakozungumziwa hapa ni kwa mara ya pili baada ya huko "kupaa"?

Unaweza kuthibitisha alipaa, na kwamba habari za kupaa kwake si hadithi za uongo tu?
 
Unaweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo?Msipende kuingilia imani za watu!Waache waamini wanavyoamini!
 
Mimi mwenyewe leo nitapaa mbinguni, nyinyi endeleeni kukaa hapo na ubwege wenu mnisubiri, mimi nitakuja kuwaokoa tu nyau nyie, okay?
 
Kama kiranga yupo basi nasogea benchi la mbele kushuhudia mechi
 
Unaweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo?Msipende kuingilia imani za watu!Waache waamini wanavyoamini!
Wewe unayeuliza uthibitisho wa uwepo wa Mungu hujaingilia imani za watu?

Mbona unaweka sheria unayoivunja mwenyewe?

Unaelewa hata unachoandika wewe mwenyewe maana yake ni nini?
 
Wewe unayeuliza uthibitisho wa uwepo wa Mungu hujaingilia imani za watu?

Mbona unaweka sheria unayoivunja mwenyewe?

Unaelewa hata unachoandika wewe mwenyewe maana yake ni nini?
Hujaelewa,kumwambia mtu athibitishe kuwa Yesu sijui alifanya nini sio sawa!Ndio maana nikamuhoji na yeye kama anaweza kuthibitisha kama Mungu yupo!
Hapa namweleza kuwa mambo ya imani waachie wenye imani hiyo!
Hilo nalo ni gumu kuelewa?
 
Sasa kama Diamond imani yake inamruhusu kumfananisha mpenzi wake na Yesu, akisema hilo, wanaomsakama watakuwa hawajaingilia imani yake?

Ukimsakama Mkristo kwa kula nguruwe, wakati imani yake haijamkataza kula nguruwe, hapo hujamuingilia imani yake?
 
Kwanin yule aliyeikashifu quran alifukuzwa kazi na serikali?Vp kama imani yake inamwelekeza hivyo?Kumfananisha Yesu(ambapo kuna imani wanaamini ni Mungu wao) na demu wake ni kuwakosea heshima!
Kesho nao wanaweza kuamka na kuimba "maumbile yako ndiyo Mohamad SAW wangu"!
Huoni hapa ni kutafuta uvunjifu wa amani?Tena narudia,wakristo ni watu wastaarabu sana!Hayo maneno yangegeuzwa kwa imani ile na mungu wao akafananishwa na tupu ya mwanamke,ingekuwa balaa sasa hivi!
 
Kwani huyo aliyefukuzwa kazi alifukuzwa na Diamond?

Mbona unachanganya madawa?

Serikali yetu yenyewe haijielewi, inajisema haina dini, lakini Bunge linafunguliwa kwa dua.

Contradiction tupu.

Sasa hiyo ndiyo ya kuiangalia kama dira?
 
Hapa nilipo namsikiliza Ariana Grande anaimba God is a woman. Kawimbo katamu sana.
 
Kwani huyo aliyefukuzwa kazi alifukuzwa na Diamond?

Mbona unachanganya madawa?

Serikali yetu yenyewe haijielewi, inajisema haina dini, lakini Bunge linafunguliwa kwa dua.

Contradiction tupu.

Sasa hiyo ndiyo ya kuiangalia kama dira?
Sio sawa kukashifu imani ya watu wengine!Katika vitu ambavyo si vya kuchezea ni imani za watu,ni rahisi sana amani kutoweka!
Diamond amekosea kukashifu imani ya wakristo wanaoamini kuwa Yesu ni Mungu kisha yeye akamfananisha na Mwanamke wake!
Mtu anaweza kujibu kwa mtindo huo huo na kumfananisha Mohamad SAW na vitu vyao halafu ikaleta shida!
Yaani Diamond kakosa mistari ya kumfananisha na Demu wake mpaka amataje Yesu?Shenzi kabisa!
 
Kukashifu ni nini?

Na kama mimi imani yangu ni kukashifu ujinga, na imani yako ni ujinga, ukiniambia mimi niache kukashifu imani za watu wengine, wakati mimi imani yangu ni kukashifu imani za kijinga, hapo na wewe hujaikashifu imani yangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…