Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Wakristo wenyewe wameshajidharau na kumfanya Yesu wao adharaulike. Ndio maana Diamond anaweza kutunga mashairi ya kumkejeli Yesu. Tena Diamond ameiga tu, aliyeanza kutoa hizo dharau ni Kangi Lugola alipomfananisha Magufuli na Yesu, na viongozi wakubwa wa dini ya kikristo wakakaa kimya huku wakimshangilia Magufuli na kumsifia ovyo ovyo. Sasa tuwaache wakristo wavune walichopanda. Yote haya ni mafanikio ya uongozi wa awamu ya tano!

Heshima ya Yesu italetwa na wale wanaomwamini, na itapotezwa na hao hao wanaomwamini.

CCM oyeee!
Magufuli oyeee!
Diamond oyeee!
Umesahau Mungu oyeeeee!
 
Jamaa anakunywaga mvinyo kwenye kikombe cha shetani pia usisahau kulaani kitendo cha wasaka tonge kumfananisha joka letu yesu masia
 
Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.

Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?

Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.

Yesu aliacha kiti chake cha nzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?

Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.


Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
Kristo uwa anapigana vita mwenyewe hapiganiwi na wanadamu... Mungu aliye hai hupigana vita yake mwenyewe akitaka ukiona Mungu anapiganiwa vita jua ni fake hana hata uwezo wa kupambana mpaka apambaniwe....
So kama Yesu hajapenda atapambana tu.
 
Mtoa mada acha udini, umejaribu kuruka baadhi ya vitu ili kuleta udini!! Emu rudia kusikiliza mashairi hayo nahisi utaelewa zaidi, kukurupuka sio kuzuri!!
Usitake kuleta mambo ya facebook , huku ni jamii forum
 
Nimeonja Utamu Wa Yesu
Ya Rose Muhando imekubaliwa na Wakristo kisa ni msanii wa Injili
Ila hii ya Leo imekataliwa na wakristo kisa ni Diamond

Mungu yuko wapi ya Ney imekubaliwa sikuona aliyeibuka kuipinga wala kusema haitakiwi
Ma Niggas huwa wanaimba nyimbo za kukejeli kule Marekani na za kuhusisha Freemasons kuipinga Imani ya Kristo hamkuibuka kupinga.

Wakati fulani niliwahi kumtongoza msichana akaniambia sikati kuolewa mwanaume pekee na rafiki yangu ni Yesu tu

Acha Nikae Kimya[emoji850][emoji850]
See now
 
Back
Top Bottom