Diamond Platnumz hili la kumfananisha demu (msichana) wako na Yesu (Mungu) utuombe radhi wakristo na utubu au wimbo wake ufungiwe na BASATA

Hoja hapa ni kumfananisha Yesu na GF wako,hayo mengine kuna nyuzi zipo kuhusu Yesu ni Mungu au vipi!
Tusipoteze focus ya uzi,Diamond aombe radhi na aufute wimbo huo!
Vipi kuhusu alie uwonja utamu wa Yesu
 
Nimeusikiliza wimbo mpya wa Diamond Platnumz uitwao ongeza kiukweli anatakiwa atafute mhariri wa mashairi na mistari yake. Kwenye ngoma ya ongeza anasema "we ndo wangu yesu mkombozi sa mbona unaniacha mwenyewe" anamuongelea mwanamke/ msichana/demu wake.

Kwa hili Diamond hapana umeenda mbali mno na umetukosea Wakristo. Hivi mkristo aimbe wimbo amljnganishe demu wake na Mtume Mohammad au Allah atakuwa sawa?

Kwetu Wakristo Yesu ni Mungu kweli, mtu kweli Yohana Mtakatifu 1:1-10. Yesu ni Mungu mwana katika nafsi tatu za Mungu zinazofanya Utatu Mtakatifu.

Yesu aliacha kiti chake cha enzi kule mbinguni akauvaa mwili akashuka duniani ili atufie na kutukomboa sisi na dhambi zetu. Alisulubiwa akafa, akazikwa siku ya tatu akafufuka na sasa ameketi mkono wa kuume wa Mungu Baba na hapa tulipo tunasubiri arudi aje awahukumu walio hai na wafu. Maana ameahidi anakwenda kwa Baba kutuandalia makao na atakuja kutuchukua ili alipo nasi tuwepo. Je ni Yesu huyu wa kumlinganisha na demu wake kweli Diamond Platnumz?

Yesu huyu ambaye alikuwepo kabla ya ulimwengu kuumbwa ambaye maandiko yanasema vitu vyote viliumbwa kwa jina lake na pasipo yeye hakuna kilichoumbwa? Huyu ndiyo wa kumlinganisha na demu.

Ni kweli sanaa inahitaji ubunifu lakini siyo kwa kiwango hiki Diamond aombe radhi kwa kweli au wimbo wake ufungiwe na BASATA.
Huyo msichana atakufa kama meko.

Tena kifo kibaya.
Binadamu akifananishwa na Mungu atakufa kifo kibaya
 
Social experiment kama kawaida
 
Wakristo wenyewe wameshajidharau na kumfanya Yesu wao adharaulike. Ndio maana Diamond anaweza kutunga mashairi ya kumkejeli Yesu. Tena Diamond ameiga tu, aliyeanza kutoa hizo dharau ni Kangi Lugola alipomfananisha Magufuli na Yesu, na viongozi wakubwa wa dini ya kikristo wakakaa kimya huku wakimshangilia Magufuli na kumsifia ovyo ovyo. Sasa tuwaache wakristo wavune walichopanda. Yote haya ni mafanikio ya uongozi wa awamu ya tano!

Heshima ya Yesu italetwa na wale wanaomwamini, na itapotezwa na hao hao wanaomwamini.

CCM oyeee!
Magufuli oyeee!
Diamond oyeee!
Dah kumbe walijikoroga wao wenyiwao
 
Back
Top Bottom