Diamond Platnumz jihadhari na washauri wako

Diamond Platnumz jihadhari na washauri wako

TinyMonster

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
242
Reaction score
154
Kwa wiki nzima hii ukifuatilia kinachoongelewa katika mitandao ya kijamii na kwenye vipindi vya burudani ni ugomvi unaowahusisha Diamond na Alikiba, yote ikianza baada ya wimbo wa Fid Q aliowashirikisha Diamond na Rayvanny kutoka na kusikika mashairi yaliyoonekana kama yanamlenga Alikiba.

Mara baada ya wimbo ule kutoka Alikiba alimjibu kwa kebehi Diamond na kumfananisha na Malkia wa Nguvu huku Ommy Dimpoz ambaye yuko menejimenti moja na Kiba alijaribu kumtetea swahiba wake akaishia kuchanwa katika wimbo mwingine ambao Diamond aliutoa kama kujibu mapigo ambapo Ommy alienda mbali zaidi kwa kumjibu kupitia Instagram katika picha aliyopozi na mama yake Diamond, Bi Sandra kitu ambacho kilionyesha kuchochea zaidi ugomvi huku mashabiki wakigawika pande mbili.

Siku 3 baadae Alikiba alitoa wimbo wake mpya alioupa jina la Seduce Me ambapo saa moja baadae Diamond kupitia instagram yake alipost picha ya mtu anaecheka kwa kebehi ikatafsiriwa kama vile ameudharau wimbo wenye, jioni yake Diamond nae akawatangazia mashabiki wake kuhusu kuachia wimbo mpya aliowashirikisha wasanii wote walio chini ya label ya Wasafi uliopewa jina la Zilipendwa na kilichofuatia hapo ni ushindani mkubwa wa mashabiki ambao wamekuwa wakitupiana maneno.

Hata hivyo suala la Diamond kutoa wimbo ni kama vile halijapokelewa vizuri na wasanii wengine ambao wanaona lengo lake ni kujaribu kuuzima wimbo wa Alikiba na wengi ukifuatilia utagundua wamechagua upande wa Seduce Me badala ya Zilipendwa.

Yameibuka maneno zaidi kuhusu namna ambavyo label ya Wasafi imekuwa na tabia ya kutoa nyimbo siku msanii yeyote mkubwa akiachia wake, kana kwamba wanataka wao tu ndio wasikike msanii mwingine asiwe juu yao.

Ninavyomfahamu mimi Diamond ni mtu ambaye yuko humble sana ukiongea nae, na nyuma ya pazia huwasaidia wasanii wengi tu wanapokuwa na matatizo. Hili suala la ugomvi wa kujaribu kuwabania wasanii wengine wasisisike inajulikana wazi ni management yake imekuwa ikilisukuma.

Ushauri wangu kwake ni kuwa ajihadhari na hii tabia na kubali kwamba ushindani ni mzuri kwenye muziki lakini isifikie hatua ya kutaka kumharibia msanii mwenzake. Asiruhusu mameneja wake Babu Tale na Sallam kumuingiza kwenye ugomvi na wasanii wengine ambao asilimia kubwa Diamond anawaheshimu kama kaka zake, atambue nguvu ya umma iliyotumika kumtetea Alikiba inaweza kuhamia kwenye kazi zake nyingine na kumshusha kabisa.

Ni hayo tu.
 
Kwakweli huo ni ukweli mchungu inabidi aunywe na auzingatie.
Ila pia namshauri akamwone manecky atupe radha ya mziki wake ule uliokuwa unaishi maana nikisikiliza ngoma ya jux manecky kwakweli mchawi wa beats za hisia kuna hilo guiter kali balaa
 
Ugomvi kaanza mwenyewe Leo yupo Mitandaoni analia lia kuonewa
 
8f067795e8a187ed19fa91834cc87f50.jpg
 
Mkuu umeongea kweli, kwa mara ya kwanza nimeshangaa diamond kupata upinzani mkubwa hv, yaani nguvu ya umma ilikuwa nyuma ya Alikiba, naamini kama Diamond angetulia hata wiki moja halafu ndo aachie zilipendwa hii ngoma ingefanya vizuri na ingepokelewa vizuri sn, diamond kwa upande mwingine ndo amesababisha seduce me ya kiba kuipa chat sana, kwa maana hio seduce me haina umaarufu huo kama ilivyopokelewa ila kwa kua ila kwa kua Diamond alikua na nia ovu kwa mwenzie ndo maana watu wakahamia kwa kiba,
 
Mkuu umeongea kweli, kwa mara ya kwanza nimeshangaa diamond kupata upinzani mkubwa hv, yaani nguvu ya umma ilikuwa nyuma ya Alikiba, naamini kama Diamond angetulia hata wiki moja halafu ndo aachie zilipendwa hii ngoma ingefanya vizuri na ingepokelewa vizuri sn, diamond kwa upande mwingine ndo amesababisha seduce me ya kiba kuipa chat sana, kwa maana hio seduce me haina umaarufu huo kama ilivyopokelewa ila kwa kua ila kwa kua Diamond alikua na nia ovu kwa mwenzie ndo maana watu wakahamia kwa kiba,
tatizo la dai lilianza kama utani kwa mabeto likahamia kwa dimpoz halafu kina mange wakalipigia punyeto kama utani jamaa kampiga dai KO KAMA MYWEATHER
 
Diamond na Kiba hawana ugomvi.
Wako kwenye biashara. Waamuzi ni mashabiki..... Nani anaingiza mkwanja mrefu kwa single zilizotoka kwa mpigo hilo hasa ndiko lengo la usanii.

Super star kuna gharama zake mojawapo ni kukubaliana katika kutokubaliana.

Mshindi wa haya ni Diamond na AliKiba kwani ndio wanaingiza ngawira.

Hapo sio ajabu kila kitu kilipangwa na team zote kuwa tutoe nyimbo tarehe husika....tupishane masaa.....nani aanze nk nk nk.

Tutafuteni pesa....hawa wanajuana.
 
Uzuri mmoja Diamond kazungukwa na kundi kubwa la watu la washauri wasiona na elimu kichwani ndiyo tatizo...... Kama mshauri mkuu mwandamizi wa Diamond mwenye elimu kubwa ni Petity Man mwenye bachelor ya mapishi hapo kuna nini tena.......????
 
Uzuri mmoja Diamond kazungukwa na kundi kubwa la watu la washauri wasiona na elimu kichwani ndiyo tatizo...... Kama mshauri mkuu mwandamizi wa Diamond mwenye elimu kubwa ni Petity Man mwenye bachelor ya mapishi hapo kuna nini tena.......????
Mkuu usiandike vitu kwa sababu umeandika Petit na Domo wapi na wapi au kwa sababu shemeji yake ukahisi wapo karibu? Seduce me ni kweli amepewa umaarufu na WCB wenyewe kwa blunders zao wangepotezea hata mwezi hivi ungepotea kama Lupela
 
Back
Top Bottom