Diamond Platnumz kufa kimziki baada ya miaka 6

Sijui MTU kama mtoa mada uwa kichwani kwake uwa anaifadhi wadudu gani?acha jiroho.
 
Siku zote huwa naombea kijana mwezangu apate mafanikio zaidi ili nijifunze kwake japo sipendi mziki wa bongo fleva hata robo
Umeongea vema! Yeye kama ame-copy na ku-paste si kitu.Cha muhimu ni kutengeneza pesa tu. Duniani leo watu wanaofanikiwa ni Innovators. Hawa ni watu wanaobolesha juhudi zilizoanzishwa na creators(wavumbuzi ).Basi wengine wafanye hivyo pia.Hata hao wa majuu huchukua mambo yetu na kwenda kuyaboresha.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] acha waisome namba kidogo
diamond mbele kwa mbele
 
Diamond platnumz ni super star Mkubwa kuliko yyt hapa tz na ea kwa ujumla na ndio maana kila anachokifanya lzm wakichungumzie na wafungue thread, Kuna mtu hapa hapa Tanzania kakopi SAME GIRL ya R KELLY FT USHER hata kumzungumzia hawajamzungumzia, ila mondi mpaka makala wamemuandikia.
 
Hakuna kipya. Moja kati ya njia za kuthibitisha Google neno lolote. Ukipata jibu lake ujue hakuna copying na pasting. All are original
 
Hata aliyeunganisha mabati kule mbeya nae alijitangaza amegundua helkopta wakati ulishagunduliwa siki nyingi.
 
Watanzania sijui ni nani ametuloga!!
Huyu kijana anaelekea kupotea,hivyo ni vyema tukawa tuna mshauri kuliko kumshangilia..
Huwezi kwenda kushindana na watu wa majuu kama una-copy hovyo kazi zao,kwa mwenendo huo usishangae kila tuzo akawa anaangukia pua..
Ni kheri upigwe Kofi kuliko kupigwa busu kinafiki..
Angalizo:sina timu,nawapenda wote,King na Daimond..
 
6 years mbele mingi sana kiba atakua kazeeka
Pombe alishatoka madarakani ikulu imeshamia Dodoma du
 
Duniani jamani hakuna kitu kipya kwa sasa, zaid unachukua idea za wenzio unaziboresha unatoa chako

Kizuri huigwa mimi sioni tatizo hapo

MSANII MAARUFU NCHINI, DIAMOND
Na Saleh Ally
GAZETI la Championi lilianza kujulikana kabla ya ujio wa Nasibu Abdul ‘Diamond’. Ninaamini litaendelea kubaki nikiwa ninamaanisha hivi, ataliacha likiendelea kusikika kwa miaka mingine mingi.
Championi litaendelea kusikika kwa kuwa linaundwa na watu wengi makini wanaotaka liendelee kufanikiwa. Zaidi linajengwa na timu, ndiyo maana litakuwa na nafasi ya kufanya vema zaidi kwa kuwa iko makini.
Diamond Platnumz, anaweza kuendelea kudumu kama Championi kama angekuwa ametanguliza umakini na ikiwezekana angependa kuumiza akili yake zaidi na mwisho, asianze kuamini Watanzania wengi ni wajinga na hawajui kabisa.

GARI; DIAMOND

GARI LIL WAYNE
Juhudi za Diamond ambaye alikulia katika maisha ya shida kutoka katika Kitongoji cha Tandale katika Jiji la Dar es Salaam, zinapaswa kupewa sifa na kuthaminiwa kwa kuwa zinasaidia vijana wengi kutaka kukua zaidi.
Lakini kadiri siku zinavyosonga mbele, inaonekana hivi; Diamond amekwama kiakili, timu inayomuongoza imekwama pia na inawezekana ina watu walioridhika, wanaoamini wamefika au wanafikiri, hakuna anayeweza kumfikia tena Diamond kwa kuwa hakuna kama yeye.
Wanawaza hivyo kwa kuwa wamesahau mengi yaliyopita, kwamba hakuna shoo zilizokuwa zinajaza kama za 2 Proud au Mr II au Sugu. Baadaye ikawa hakuna kama Profesa Jay, Juma Nature, Lady Jaydee na wengine kama makundi ya East Coast, Wanaume TMK na kadhalika lakini sasa wanaonekana ni wa kawaida kabisa.
Huenda wale wana makosa yao, lakini kosa kubwa la Diamond linataka kulingana kabisa na vifo vya bendi za dansi ambazo zilikubaliana na kuamua kuiga kila kitu cha bendi za DR Congo na baada ya hapo zikataka kushindana sokoni na Wakongo.

ANARUKA DIAMOND...

ANARUKA LIL WAYNE
Leo unamuona Koffi Olomide ambaye Muumini Mwinjuma alimkuta sokoni, amemuacha na Mwinjuma kuinuka inaonekana ni hadithi itakayokuwa haina mhadithiaji.
Kwa nini inakuwa hivyo, ni kwa kuwa aliyeanza chake, mara zote anakuwa bora zaidi kuliko anayeiga na tabia ya watu ni kupenda vilivyo bora hasa kwa vile vinavyokuwa vimeanzishwa.
Mafanikio ya kibiashara ni ubunifu mpya kwa kuwa macho na masikio ya mwanadamu huvutiwa na kuona au kusikia mambo mapya na si kurudia na hasa inapozungumziwa ubunifu.

DIAMOND AMETUPA FEDHA, WASIOCHANA WALIOKUWA KANDO YA BARABARA WANAGOMBEA

LIL WAYNE AMETUPA FEDHA, WASIOCHANA WALIOKUWA KANDO YA BARABARA WANAGOMBEA
Kuona, kusikia na kuamini Diamond amekopi halafu akapesti na akarudia mara nyingine ndani ya mwaka mmoja zaidi ya mara tatu, ni kujinyonga kwa njia ya mkato na kutengeneza mwisho wake ingawa yeye anaamini haitatokea.
Diamond Platnumz alimshirikisha AKA wa Afrika Kusini katika Wimbo wa Make Me Sing, ulipotoka watu wengi badala ya kujadili ubora wa wimbo wenyewe, suala la kuiga Wimbo wa Got Money ya Lil Wayne ndiyo likawa mjadala kwa kuwa ilikuwa ni copy & paste bila ya aibu hata kidogo!
Wakati Diamond anatoa wimbo wake, tayari huo wa Lil Wayne ulikuwa umetazamwa na watu milioni 57. Wake ndani ya wiki chache ukawa umetazamwa na watu zaidi ya 600,000. Hapa utajifunza ubora wa usahihi, lakini jiulize hao milioni 57, wangapi waliingia katika 600,000 ya Diamond na wataweza vipi kukichukulia ni kitu kipya na wanapaswa kufurahia.

WANENGUAJI WA DIAMOND

WANENGUAJI WA TAYLOR SWIFT
Tena unaona Video ya Got Money ilitoka mwaka 2008, ya Diamond ni miaka zaidi ya mitano baadaye, huenda anadhani Watanzania ni mazumbukuku, hivyo hawawezi kuwa wang’amuzi.
Suala hilo la Diamond kukopi, liliandikwa na gazeti hili Februari 19, mwaka huu kwa kichwa cha habari, “Sare-sare maua”, mwandishi akiwa ni Hans Mloli. Diamond amekaa si zaidi ya mwaka, amerudia jambo kama hilo, ambalo nalo mjadala wake ni “copy & paste”.
Safari hii ‘kahamishiaa’ video kadhaa ndani ya video yake moja ya wimbo wa Kidogo ambao ameshirikiana na P Square. Wimbo ni mpya, mzuri na gumzo lakini video yake imerudi palepale, “ya kuiga”,
Kuiga bila ya kuboresha ni uzembe wa kufikiri, kutojiamini na ikiwezekana naweza kuiita udanganyifu au kuwapotezea watu muda kwa kuwa sina sababu ya kuangalia video ya msanii wa Marekani, halafu nikirejea kuangalia ya Diamond nayo iwe vilevile.

JASMINE V, KIPANDE CHAKE HIKI KIMEIGWA KWENYE WIMBO WA DIAMOND SEHEMU ALIYOIMBA PETER OKOYE WA P SQUARE, ANGALIA PICHA YA CHINI.

Au Diamond anaamini anavijua vitu vya Marekani yeye peke yake pamoja na meneja wake, Babu Tale, Said Fela, Sallam Sharaff maarufu kam SK, wengine wote hawajui au hawajawahi kuona, hivyo hawatang’amua hata kidogo!
Maana katika video ya Kidogo, ndani yake amechukua sehemu zinazofanana kabisa kwa utengenezaji na matukio katika video za wasanii Tyga na Jasmine V.
Ameiga mambo ya video ya Wimbo wa Right There ya Jasmine V, kafanya hivyo kwenye For The Road ya Tyga na kinachoshangaza hadi kukaa na mbwa mweupe, mavazi ya warembo ambayo ni rangi ya njano na bluu na hata mshono.
Hii unaona katika video yake ya Make Me Sing aliiga vitu kama mavazi, aina ya gari, aina ya uvamizi, fedha kutupwa barabarani na wanaogombea ni wasichana ili kuzuia gari la polisi. Unajiuliza, hivi Diamond na timu yake hawana uwezo hata kidogo tu wa kufikiria? Wamechoka au ndiyo wamefika mwisho? Au Diamond alifika hapo kwa nguvu zake na sasa alionao ni wasio na mawazo sahihi na hajui wanamtumbukiza shimoni?

DIAMOND AKIWA KWENYE MAVAZI MEUPE, MBWA MWEUPE ALIYE KULIA KWAKE KAMA ALIVYOFANYA TYGA KWENYE VIDEO YAKE, ANGALIA PICHA YA CHINI!

Mimi najiuliza, hata kama wale wanamtumbukiza shimoni, yeye mwenyewe haoni au hawezi kujiuliza kwamba mambo anayofanya yatamuangusha kwa kuwa kazi zake zinavuka mipaka hivyo itafikia siku moja anachaguliwa kwenye tuzo ya BET au nyinginezo halafu video yake iliyotazamwa na watu 600,000 inashindana na ile yenyewe iliyotazamwa mara milioni 57 na yeye akiwa ameiga.
Vipi Diamond wakati anaingia kimataifa zaidi ndiyo anashindwa kuwa mbunifu zaidi? Anaiga vya wale anaokwenda kushindana nao badala ya kutengeneza ladha mpya? Hata kama Watanzania hawajui kama anavyoamini, ataweza vipi kushindana kimataifa kwa “copy & paste”, tena ya waziwazi na inayoshangaza kama kweli walioamua walikuwa hawajachoka!
Kama watu wanaamini Diamond ndiye bora kuliko wasanii wote kutokana na mafanikio yake, je, wanaomfuatia wanaweza vipi kuiga anachofanya kama mfano au changamoto kama atakuwa anaiga video ya msanii mwingine akashindwa hata kubadili nguo, gari na aina ya kukaa?

MEMBA WA P SQUARE AKIWA KATIKA SEHEMU YA WIMBO WA DIAMOND AMBAO UMEKOPIWA KUTOKA KATIKA WIMBO WA MSANII TYGA HAPO CHINI!

Mfano huyu akiwa na mbwa mweupe, basi Diamond alishindwa hata kutafuta mbwa mweusi ili kuwa kitu tofauti! Jiulize hata ukaaji na upande alivyokuwa amekaa Tyga na Diamond alishindwa kubadili, jamani huyu ni Diamond yuleyule? Au amekubali kutengeneza kifo chake kimuziki, mapema kabisa!
Siku chache zilizopita, unamuona muigizaji maarufu wa Hollywood na duniani kote Terrance Howard akiwa amekaa na simba. Halafu siku chache zinazofuata, unamuona Diamond akiwa naye amekaa na simba kwa mkao uleule akionyesha uvivu wa kufikiri kwa kiwango cha juu tena ajabu zaidi, simba wakiwa wanatokea Afrika na kwenda kufanyiwa kazi Marekani kabla ya Tanzania na yule anayetokea kwenye simba wengi anakubali kuiga vilevile.
Nikajiuliza tena, hivi, kuliko Diamond kukaa kwani angemshika simba akiwa amesimama au anatembea, ugumu ungekuwa nini! Bado ingewezekana Diamond kutafuta mnyama mwingine ili kuepuka kuendelea kuonekana ni aliyechoka.
Inawezekana kabisa, mashabiki wa Diamond wameamua kuamini kila kitu chake ni bora bila ya kuchunguza. Watanzania wote hawawezi kuwa na akili zinazolingana na kwa utandawazi wa kiwango cha juu, dunia sasa ni kijiji. Taratibu ataanza kupoteza mashabiki mmoja baada ya mwingine.
Akiendelea hivi, Diamond lazima akumbuke ‘atajiua’ mwenyewe kwa kuwa wako wengine ‘walijiua’ na leo wanasuasua kurejea kileleni.

TERRANCE NA SIMBA, DIAMOND NAYE AKAKOPI VILEVILE AKIWA NA SIMBA...!!

Kwanza ni lazima abadilike na kama ataendelea hivi, hakuna ubishi, atakwisha na kumalizika kabisa kisanii na mwisho, itabaki stori. Inawezekana anaona sawa kwa kuwa wengi waliopaswa kumkumbusha hasa wanaohusika na sanaa kwenye vyombo vya habari hasa redio na runinga mbalimbali, wamegeuka kuwa wapambe kwake na wanachofanya ni kufurahia kila anachofanya na kusifia ili kuepuka kupoteza urafiki naye!

Mwisho, Diamond anapaswa kukumbuka, miaka sita iliyopita, hakuwa maarufu alivyo sasa na kuna wengine walikuwa wakitamba. Akiendelea hivi, miaka sita ijayo Mwenyezi Mungu akimjaalia uzima, atakuwepo lakini wengine watakuwa wakitamba zaidi yake kwa kuwa watapita katika mashimo ya udhaifu wake wa kuamini Watanzania hawajui lolote, kumbe kuna wengi kwa wingi wanajua mengi zaidi yake kuhusiana na muziki wa ndani na nje ulikotoka na unapokwenda.
 
Je utanipendaga inaelezea kila kitu
 
Wakati Mond akipiga mzigo wewe unajifanya mtafiti wa kumtafiti kipaji chake kitakoma lini...endelea kutafiti,ingia na show zake zote ulipe kiingilio kabisa ili akifa kimziki uwe umemchangia mtaji!
 
Diamond platnumz ni super star Mkubwa kuliko yyt hapa tz na ea kwa ujumla na ndio maana kila anachokifanya lzm wakichungumzie na wafungue thread, Kuna mtu hapa hapa Tanzania kakopi SAME GIRL ya R KELLY FT USHER hata kumzungumzia hawajamzungumzia, ila mondi mpaka makala wamemuandikia.
Kwani siwezi kukupa like miliom at once??? UMEMALIZAAAAAAAAAA!
 
Na hiyo miaka sita yako ndio yapotee yote..huna hata aibu
 
Duh! We jamaa si tu kwamba unatia huruma bali unatia aibu endapo dada zako wangefahamu kwamba hizi ndizo tabia zako!! Nakumbuka ulishawahi kufunga kanga kiuononi wewe kusherehekea Vodacom kuondoa mabango ya Vodacom Ongea Deilee kwa kile ulichoamini hilo ni rungu kwa Diamond!! Mbona huelekei kwamba jamaa ni level zako? Kama hisia zangu ni sahii; hivi huoni you're wasting your time dealing with someone ambae si ajabu hata kukufahamu hakufahamu; si ajabu hata kukaa nae sehemu moja, hujawahi kukaa nae sehemu moja! Kaita wimbo wake Nana, mkasema ameiga; yaani hata aibu hamuoni ingawaje wengi wenu mnaoleta haya mambo ni wanaume!

Look, hata maana ya ku-copy hujui pamoja na kutumia muda wote huo kuandika ki-post lireeeeeeefu!! Yaani kv Diamond ametengeneza video akiwa na simba pembeni yake hiyo nayo inaitwa ame-copy na ame-copy kwa Terrence Howard? Serious? Hivi kuna creative work iliyofanywa na Terrence Howard hapo hadi kila atakayefanya hivyo aonekane ame-copy kwake? Hivi kabisa unaamini kwamba hakuna mtu yeyote duniani ambae amepata kupiga picha na Simba except Terrence Howard to the point mtu mwingine yeyote akifanya hivyo aonekane ame-copy? By the way, hivi unafahamu kiwango kinachokubalika kwenye kazi sanaa kwa mtu mmoja kutumia kazi ya mtu mwingine? Majambazi hata hapa Dar ukiwaotea huwa wanamwaga pesa ili kuwa-keep watu busy lakini kwako wewe hiyo ni ku-copy!!!

Dada zetu siku hizi sijui watakuwa wanafanya mambo gani sijui manake yale yanayowapendeza wao hivi sasa hufanywa na kaka zao!!
 
Back
Top Bottom