Diamond Platnumz kutumbuiza kwenye tamasha la BET EXPERIENCE 2015

Diamond Platnumz kutumbuiza kwenye tamasha la BET EXPERIENCE 2015

Kidingi

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2012
Posts
1,872
Reaction score
1,832
Lile tamasha kubwa la BET Experience ambalo hufanyika L.A, Marekani wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo za BET, linatarajiwa kufanyika Afrika kwa mara ya kwanza mwaka huu na kuitwa BET Experience Africa.

Tofauti na diamond wasanii wengine waliotajwa tayari ni Tamar Braxton, Maxwell, na Flavour na wengine kuendelea kutajwa hivi karibuni

Tamasha la BET Experience Africa ambalo litajumuisha burudani za aina mbalimbali ikiwemo muziki, comedy, mitindo, na mambo mengine mengi limepagwa kufanyika Desemba 12, 2015 jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

“VIMN Africa and BET are proud to introduce this incredibly successful BET franchise to African audiences for the first time, celebrating so many rich and varied faces of the urban lifestyle experience under one roof.” Alisema makamu wa Rais na mkurugenzi mtendaji wa Viacom International Media Networks ( VIMN) Afrika, Alex Okosi.

Kwa Marekani mwaka huu (2015) tamasha hilo lilifanyika kwa siku 4 kuanzia June 25 hadi siku yenyewe ya tuzo June 28 ikiwa ni mara yake ya 3 kufanyika. BET Experience 2016 ya Marekani imepangwa kufanyika June 23-26, 2016.
 
Kidingi kwa nn kaondoa tiffas dady kwa bio yake ku fair usichague habari lete habari zote zinazomuhusu hivi itakuwa sio fair
 
Last edited by a moderator:
Kidingi kwa nn kaondoa tiffas dady kwa bio yake ku fair usichague habari lete habari zote zinazomuhusu hivi itakuwa sio fair

Unapoandika maneno kwenye bio kuna limit ya idadi ya maneno, mwanzoni aliweka Tiffah's daddy ila kukawa na tatizo kwa wale waliokuwa wanahitaji kuwasiliananae kuto kuwajibu emails kwa wakati, ndiomaana akaamua aongeze na email ya Manager wake Salaam pale ili kurahisisha mambo..


KING OF AFROPOP

We keep reigning
 
Last edited by a moderator:
Ndo uzuri wa kuwa wa kimataifa hausibirii shoo za msaada wa tigo
 
Back
Top Bottom