sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Hii ni summary ya interview aliyofanya na Dizzim online radio.
Nazindulia A boy from tandale album nchini Kenya sababu mimi ni msanii wa east africa sio wa Tanzania pekee.
Rick Ross alinishangaa baada ya kuniona wakati tunafanya video,alisema ''you're a star'' ..alinipa siku mbili akijitoa tufanye video sababu alinikubali.
Lazima wasanii tuwe na njia mbadala, ndio maana WCB nyimbo azipigwi kwenye vyombo ila zinahit mtaani.
Ramani ya Wasafi tv na radio nilianza kuichora miaka mitano iliyopita.
Naamini watoto wa uswazi wana akili nyingi kuliko wakishua.
Mimi siwezi kufeli, anaefikiri anaweza nifelisha anajidanganya. Nitafeli siku Mungu akiamua.
Mimi ni kama mzee Bakhresa, uwezi kulala bila kunitaja.
Wanaonibania wanapoteza muda.
Angalia wote wanaoblock content za WCB wanapoteza mvuto na mashabiki.