Diamond Platnumz na Mbwana Samatta wanastahili kutunukiwa PhD ya heshima

Diamond Platnumz na Mbwana Samatta wanastahili kutunukiwa PhD ya heshima

Chinedu5

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2015
Posts
763
Reaction score
2,755
Niende kwenye mada moja kwa moja.

Kwa msanii kama Wizkid na Tiwa Savage kuja Tanzania, kualikwa na mtoto wa Tandale, mtoto alielelewa na single mother kwa maisha ya kubangaiza, mtoto ambaye hata Form 4 hajamaliza kama kamaliza basi kafeli) ni bonge la achievement.

KiukwelI Diamond kaleta mabadiliko makubwa mno na anastahili sanamu lake liwekwe pale mjini posta,na kumbukumbu zake ziwekwe makumbusho ya taifa, apewe hata PhD ya heshima akiwa hai tusisubiri afe ndo tuanze unafiki! Leo hii Diamond ameajiri watu zaidi ya 200, wenye elimu kumzidi na wasio na elimu. Watanzania tuweke unafiki na ushabiki pembeni, tuanze ku- appreciate vya kwetu.

Pia kuna mtu kama Samatta (SamaGoal), naye anastahili heshima ya PhD na sanamu lake liwekwe pale nje Uwanja wa Taifa.

Wapo wengi sana walioleta mabadiliko kwa nchi yetu tuwaenzi hawa ma living legends wetu tusisubiri wafe ndio tuanze UNAFIKI!!
 
Wewe kweli ni kilaza, kwani ni mara ya kwanza huyo Wizkid kuja bongo? Watu wamewaleta akina Jay Z, 50 cent na wengine kibao na hawajapewa hiyo Phd
Hata wewe unaweza kuwa kilaza hatuzungumzii wasanii wangapi waliowah kuja hapa Tanzania tunachozungumzia hapa ni msanii aliye na ushawishi na kukubalika na wasanii wakubwa.
 
Hata wewe unaweza kuwa kilaza hatuzungumzii wasanii wangapi waliowah kuja hapa Tanzania tunachozungumzia hapa ni msanii aliye na ushawishi na kukubalika na wasanii wakubwa
Hizi story tumezichoka nchi hii ina mambo mengi ya maana ya kufuatiliwa kipindi hiki ndo maana akili zinakuwa zimelala lala tu
 
Hizi story tumezichoka nchi hii ina mambo mengi ya maana ya kufuatiliwa kipindi hiki ndo maana akili zinakuwa zimelala lala tu
Hujalazimishwa kusoma kuna majukwaa yanayojadili hayo mambo unayoyataka kwanini usiende huko
 
Hii nchi tukianza wapa heshima watu kwa kuweka masanamu yao kila kona

Tutabadilishwa jina na majirani zetu watatuita Nchi ya Masanamu

Mwalimu sanamu
Askari sanamu
Magu sanamu
Samaki sanamu
Saa sanamu
D sanamu
Samatta sanamu

hii itakua nchi gani sasa...

Tufanye kinachofanyika kule Hollywood inatosha sana,Heshima zote ziwe under one roof
 
Tusubiri kwanza, Samatta namkubali ila hastaili kupewa tuzo yoyote. Hakuna mafanikio yoyote aliyotuletea.

Tusubiri huko mbeleni Taifa letu likichukua kombe la AFCON au likishiriki Kombe la Dunia.
Platnumz je
 
Acha kumleta Wizkid na Tiwa,ebu angalia background yake,alipotoka wote tunafahamu hadi hapa alipofika ni hardworking,kuna waimbaji wangapi wanasauti na mashairi zaidi yake??kawasaidia wangapi?Katoa ajira ngapi?

Alafu unatumia vigezo vipi kumuita mtu kilaza??nmetoa mawazo yangu,hukubaliani nayo toa yako au pita vile umeitwa u comment??

Kingine,unadhihirisha akili yako kwa maneno yako,logic yako ni dhaifu mno,"kwa sababu wengine wamefanya vizuri hawajakubalika,basi yeyote atakaefanya vizuri asipongezwe"hii ni logic dhaifu na ya kimasikini mno,ni sawa na ile ya (tukose ote)!!
Wewe kweli ni kilaza, kwani ni mara ya kwanza huyo Wizkid kuja bongo? Watu wamewaleta akina Jay Z, 50 cent na wengine kibao na hawajapewa hiyo Phd
 
Hii nchi tukianza wapa heshima watu kwa kuweka masanamu yao kila kona

Tutabadilishwa jina na majirani zetu watatuita Nchi ya Masanamu

Mwalimu sanamu
Askari sanamu
Magu sanamu
Samaki sanamu
Saa sanamu
D sanamu
Samatta sanamu

hii itakua nchi gani sasa...

Tufanye kinachofanyika kule Hollywood inatosha sana,Heshima zote ziwe under one roof
Kwa platnumz anastahili mkuu
 
Hata wewe unaweza kuwa kilaza hatuzungumzii wasanii wangapi waliowah kuja hapa Tanzania tunachozungumzia hapa ni msanii aliye na ushawishi na kukubalika na wasanii wakubwa.
Ushawishi bila pesa,. Hao Pesa ndo Imewaleta hapa.. Na Si Ushawishi wa Diamond Hao wanaweza kuletwa hata na Ebitoke kama pesa anayo..

Alilolifanya Diamond ni jambo la Kawaida watu Walishafanya sana.. Anayofanya ni Marudio
 
Back
Top Bottom