Diamond Platnumz na Nandy, waambieni wanaowatumia kamwe dunia haitarudi nyuma!

Tairi bovu

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
3,063
Reaction score
2,985
Wanajamvi

Nianze kwa kuweka msimamo wangu kwamba mimi sio mpenzi kabisa wa bongo flavor wala bongo movies. Naamini wengi walio kwenye hilo kundi kwa maana ya wasanii ni watu wa hovyo na mfano ni Wema Sepetu na Lulu. Hawa kwangu naamini ni viumbe wa hovyo kabisa kabisa.

Msanii Diamond na Nandy sijui wameanza kutumiwa na huyu anayejiita mwenye Mkoa wa Dar? Nitaeleza.

Nandi alijirekodi akifanya ujinga. Nauita ujinga kwasababu mtu mwenye akili na utashi hawezi kurekodi mambo ya faragha na kuyarusha kwenye mitandao. Ukifanya hivyo hata kwa kutumwa na Bashite kama alivyofanya huyo Nandy humuumizi yeyote ila unajiumiza mwenyewe bila kujua.

Hatimaye jana uliibukia TCRA kuomba radhi na kuonesha kwamba mitandao ni kitu kibaya; la hasha. Muulize Bashite ile clip ya kumtukana Lowassa iliyomkweza daraja au ile picha ya kumfunga kamba za viatu Ridhiwani au ile clip ya kumpiga mzee Warioba zingewafikiaje mabwana zake kama sio mitandao? Leo anakwambia wewe uikosoe mitandao? Umejiua mwenyewe.

DIAMOND: Kwa mkakati uliopangwa kipuuzi na kitoto kama ilivyo mingine uliwekwa ndani kisha ukaibukia TCRA ati unaenda kuomba msamaha? Yaani badala ya kuomba msamaha unadai ati VIJANA TUWE MAKINI NA MITANDAO? Bila mitandao wewe ungekuwa hapo ulipo? Umeimba kitu gani wewe hadi uwe maarufu hivyo? Nani hajui biashara unazofanya? Nani hajui?

Kimkakati bwana Diamond alionekana wakati wa kupokea kandege/panga boy pale JNIA akiteta jambo na malaika. Ati leo anatumika kudiscourage matumizi ya mitandao.

Ushauri: Diamond wanaokutuma na kutumia waambie dunia haiwezi rudi nyuma kusubiri frastrations zao. Yani watu wanafikiria namna ya kuwasiliana kwa urahisi kupitia mitandaoni! ( tabia ya utandawazi) wewe umetoka Kolomije juzi na vyeti vya kuiba uturudishe nyuma? Hiyo haiwezekani. Utarudi wwe na Diamond wako sie tunasonga.
 
Tutasikia mengi tutaona mengi siku ikifika
 
Mkuu mbona hueleweki?
Wewe ndio mgeni kwa daimond
Kwa sisi wapenzi wa mziki tumeshamzoea kiki zake kwani hajaanza leo.
Hizo video ulizoziona na za kawaida kwake kwani zipo nyingi za hatari ambazo amezifanya na zari.

Mondi ni kawaida yake wala haihusiani na maandamano
 
Chagua moja kuwa mchumba wa Nyapala ua kuomba radhi......wewe ungefanyeje hapo
 
SIRI:Wasanïi fulani mapema tarehe 25-4-2018 watakwenda TCRA kuhojiwa,ili kupoteza watu maboya "waache kusaĺï na kujisomea" huku Chakubanga akibishana na CAG kule matamasha yakiendelea
 
Huna lolote umeanza vizuri kwa kutoa wosia mzuri kumbe kuna watu umewatarget kuwatolea nyongo. Wapigie cm unatujazia server upupu
 
Nianze kwa kuweka msimamo
wangu kwamba mimi sio
mpenzi kabisa wa bongo
flavor wala bongo movies.
Naamini wengi walio kwenye
hilo kundi kwa maana ya
wasanii ni watu wa hovyo na
mfano ni Wema Sepetu na
Lulu. Hawa kwangu naamini ni
viumbe wa hovyo kabisa
kabisa.

Uzi ulikua uishie hapa.
 
Hapa zahir shahiri akili ndipo zililpo ishia ndio uwezo wako wa kufikiria umegota uchafu wa watu wengne ufananishe na mambo mengne wew Fanya kile unachoona kinafaa na sio kuleta mada zenye law quality
 
Hawajasema mitandao ni mibaya! Kinachogomba hapa ni namna ya kuitumia! Usipotoshe maudhui ya kauli zao!
 
Reactions: UCD
Njaa + Ushamba... vilimfanya Diamond akutumiwa vibaya sana na CCM hasa kuanzia 2014 mpaka leo hii.

Yupo yupo tu...
 
Ila kwa mtu anayewaza vizuri,kwenye issue ya diamond lazima ujiulize..tukumbuke diamond alikuwa kwenye uzinduzi wa ndege wiki chache zilizopita huku akicheka na raisi...do you think,ni rahisi tu polisi na tcra wamwite kwa ile video?
 
Hahahaha Huwa mnanichekesha sana nyie wana harakati wa nyuma ya keyboard yani huwa mnadai demokrasia ila wenzenu wakifanya demokrasia mnawapinga na kuwaona wabaya....
Diamond na Nandy hawajafanya kosa lolote kuhimiza vijana kuwa makini na mitandao au kutumia vizuri mitandao...binafsi naona wametimiza wajibu wao kama vijana na kama wana demokrasia...
Swala la kutaka wenzenu wasioongee chochote kuhusu mitandao au kufanya lolote kwa kuwa ninyi mnakashughuli fulani kwa hofu katapotea basi ni wazi ninyi ndio madikteta watupu kwani mnatulazimisha tusimamishe shughuli zetu kisa mna shughuli yenu inayo wahusu....nyie wana harakati punguzeni udikteta waacheni wenzenu wafanye demokrasia......

Unasema wanatumika na Makonda na hujaonesha kosa gani wametenda kama kweli wana tumika na Makonda...Pia umesahau kutumika na mtu nayo huwa ni demokrasia hivyo kama ni kweli wanatumika basi wamechagua kufanya demorasia hivyo hawajatenda kosa maana hata ninyi wana harakati huwa mnatumika...

Uliposema huwa ufatilii mambo ya bongo fleva imebidi nikuhurumie tuu kwa kuwa unatulazimisha sisi tuwe kama wewe.....Sisi tunafatilia sana tena sana na ndio maana vyombo vya habari vyote vilikwenda kwenye press ya Diamond hadi Clouds..
Pole sana
 
ulimsikia raisi leo alichoongea juu ya mitandao? hamuipendi
 
bullshit kimambi shithole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…