Diamond Platnumz na Nandy, waambieni wanaowatumia kamwe dunia haitarudi nyuma!

Diamond Platnumz na Nandy, waambieni wanaowatumia kamwe dunia haitarudi nyuma!

Wanajamvi

Nianze kwa kuweka msimamo wangu kwamba mimi sio mpenzi kabisa wa bongo flavor wala bongo movies. Naamini wengi walio kwenye hilo kundi kwa maana ya wasanii ni watu wa hovyo na mfano ni Wema Sepetu na Lulu. Hawa kwangu naamini ni viumbe wa hovyo kabisa kabisa.

Msanii Diamond na Nandy sijui wameanza kutumiwa na huyu anayejiita mwenye Mkoa wa Dar? Nitaeleza.

Nandi alijirekodi akifanya ujinga. Nauita ujinga kwasababu mtu mwenye akili na utashi hawezi kurekodi mambo ya faragha na kuyarusha kwenye mitandao. Ukifanya hivyo hata kwa kutumwa na Bashite kama alivyofanya huyo Nandy humuumizi yeyote ila unajiumiza mwenyewe bila kujua.

Hatimaye jana uliibukia TCRA kuomba radhi na kuonesha kwamba mitandao ni kitu kibaya; la hasha. Muulize Bashite ile clip ya kumtukana Lowassa iliyomkweza daraja au ile picha ya kumfunga kamba za viatu Ridhiwani au ile clip ya kumpiga mzee Warioba zingewafikiaje mabwana zake kama sio mitandao? Leo anakwambia wewe uikosoe mitandao? Umejiua mwenyewe.

DIAMOND: Kwa mkakati uliopangwa kipuuzi na kitoto kama ilivyo mingine uliwekwa ndani kisha ukaibukia TCRA ati unaenda kuomba msamaha? Yaani badala ya kuomba msamaha unadai ati VIJANA TUWE MAKINI NA MITANDAO? Bila mitandao wewe ungekuwa hapo ulipo? Umeimba kitu gani wewe hadi uwe maarufu hivyo? Nani hajui biashara unazofanya? Nani hajui?

Kimkakati bwana Diamond alionekana wakati wa kupokea kandege/panga boy pale JNIA akiteta jambo na malaika. Ati leo anatumika kudiscourage matumizi ya mitandao.

Ushauri: Diamond wanaokutuma na kutumia waambie dunia haiwezi rudi nyuma kusubiri frastrations zao. Yani watu wanafikiria namna ya kuwasiliana kwa urahisi kupitia mitandaoni! ( tabia ya utandawazi) wewe umetoka Kolomije juzi na vyeti vya kuiba uturudishe nyuma? Hiyo haiwezekani. Utarudi wwe na Diamond wako sie tunasonga.
Hii ndio shida ya kila mtu kujua kufungua ID jf na kupost....atakayeelewa hili andiko aniTAG tafadhali
 
Mbona hueleweki?
Unasonga na nani kwenda wapi?

Kwani kudiscourage matumizi ya mitandao lazima ifanyike kwa kurekodi picha za aibu? Tena kwa kushawishiwa?
Mbona hata haiingii akilini?
 
Back
Top Bottom