Diamond Platnumz na Nandy Wazoa Bilioni 3 huko Mombasa kwenye harusi ya Zakir, Mwana wa Bilionea Imran Kholsa. Rais wa Kenya Miongoni mwa Wageni

Diamond Platnumz na Nandy Wazoa Bilioni 3 huko Mombasa kwenye harusi ya Zakir, Mwana wa Bilionea Imran Kholsa. Rais wa Kenya Miongoni mwa Wageni

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Super bilionea toka Mombasa, Imran Kholsa, ameendelea kuthibitisha kuwa pesa kwake si tatizo, akigeuza harusi ya mtoto wake kuwa tukio la mwaka

Ni baada ya kutenga kiasi cha dola 1,350,000 (sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 3) kwajili ya Diamond Platnumz na Nandy kutoa burudani kwenye harusi ya kifahari ya mtoto wake, Zakir. Hafla hiyo ilifanyika jijini Mombasa na kuhudhuriwa na viongozi mashuhuri, akiwemo Rais wa Kenya na Gavana wa Mombasa.

Nandy - Dola 350,000 ( Shilingi milioni 826)

Diamond - Dola 1,000,000 (Shilingi Bilioni 2.3 )

1734832143502.png






 
Sisi chadema tunapinga, haiwezekani serikali iangalie tu
 
hivi huwa munaamini vipi hizo takataka? Dunia wajinga hawawezikwisha kwa kweli
 
Super bilionea toka Mombasa, Imran Kholsa, ameendelea kuthibitisha kuwa pesa kwake si tatizo, akigeuza harusi ya mtoto wake kuwa tukio la mwaka

baada ya kutenga kiasi cha dola 1,350,000 (sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 3) kwajili ya Diamond Platnumz na Nandy kutoa burudani kwenye harusi ya kifahari ya mtoto wake, Zakir. Hafla hiyo ilifanyika jijini Mombasa na kuhudhuriwa na viongozi mashuhuri, akiwemo Rais wa Kenya na Gavana wa Mombasa.

Nandy - Dola 350,000 ( Shilingi milioni 826)

Diamond - Dola 1,000,000 (Shilingi Biliobi 2.3 )

View attachment 3182106



View attachment 3182116

View attachment 3182113
Wakenya watameza viwembe safari hii.
 
Ajabu sasa japo siwaonei kijicho chochote unakuta ndoa kama hii inafungwa baada ya siku chache inasambaratika.Nimeshawahi ona harusi moja Dar miaka30 iliyopita watoto wa vigogo wawili walioana nawahifadhi majina yao.

Pamoja na bia za Breweries zilikuja bia za Steller artois kwa meli maalum.Barabara zilifungwa mitaa miwili.

Ile ndoa ilidumu kwa miezi mitatu.
Hata mimi ningekuwa na ukwasi ningefanya hivi ila sababu mungu hajanipa ukwasi huo kanipa ya ugali na kusumbua mtaani kidogo nikifanya nafanya kwa urefu wa kamba yangu kikubwa kuwaombea maharusi maisha mema.

Na hawa tuwaombee maisha mema ya ndoa. Wapo watu watasema ohh freemason umasikini wako usimuambukize mtoto wa mwenzio.
 
Kila Mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

cc
Willy Paul
 
Why 2b wakati hata angetoa offer ya 200m wangekubali
 
Back
Top Bottom