Super bilionea toka Mombasa, Imran Kholsa, ameendelea kuthibitisha kuwa pesa kwake si tatizo, akigeuza harusi ya mtoto wake kuwa tukio la mwaka
Ni baada ya kutenga kiasi cha dola 1,350,000 (sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 3) kwajili ya Diamond Platnumz na Nandy kutoa burudani kwenye harusi ya kifahari ya mtoto wake, Zakir. Hafla hiyo ilifanyika jijini Mombasa na kuhudhuriwa na viongozi mashuhuri, akiwemo Rais wa Kenya na Gavana wa Mombasa.
Hili linaweza kuwa jipya kwako... Hata visivyo na uhai kwenye ulimwengu wa roho vina yoho.. Kimojawapo ni pesa ama fedha, ukipenda ziite shekeli.. Ni wazi umeshawahi kusikia watu wakisema.. Fulani bwana pesa imemkubali.. Ama Fulani bwana pesa imemkataa! Licha ya pesa kuitana na kualikana...
Super bilionea toka Mombasa, Imran Kholsa, ameendelea kuthibitisha kuwa pesa kwake si tatizo, akigeuza harusi ya mtoto wake kuwa tukio la mwaka
baada ya kutenga kiasi cha dola 1,350,000 (sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 3) kwajili ya Diamond Platnumz na Nandy kutoa burudani kwenye harusi ya kifahari ya mtoto wake, Zakir. Hafla hiyo ilifanyika jijini Mombasa na kuhudhuriwa na viongozi mashuhuri, akiwemo Rais wa Kenya na Gavana wa Mombasa.
Ajabu sasa japo siwaonei kijicho chochote unakuta ndoa kama hii inafungwa baada ya siku chache inasambaratika.Nimeshawahi ona harusi moja Dar miaka30 iliyopita watoto wa vigogo wawili walioana nawahifadhi majina yao.
Pamoja na bia za Breweries zilikuja bia za Steller artois kwa meli maalum.Barabara zilifungwa mitaa miwili.
Ile ndoa ilidumu kwa miezi mitatu.
Hata mimi ningekuwa na ukwasi ningefanya hivi ila sababu mungu hajanipa ukwasi huo kanipa ya ugali na kusumbua mtaani kidogo nikifanya nafanya kwa urefu wa kamba yangu kikubwa kuwaombea maharusi maisha mema.
Na hawa tuwaombee maisha mema ya ndoa. Wapo watu watasema ohh freemason umasikini wako usimuambukize mtoto wa mwenzio.