sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Baada ya kununua helicopter yake ya kifahari, Diamond Platnumz ndio anakuwa mtanzania wa kwanza kumiliki helicopter ya kifahari.
Wapo matajiri wengine waliwahi miliki helicopter za kuungaunga ila tajiri huyu mdogo sana kiumri mzaliwa wa Tandale anamiliki helicopter ya kifahari.
Helicopter hii ni maandalizi ya ujio wa ndege yake binafsi ya kifahari sana ambayo ni suala la muda itakuja kuwapa watu kisukari cha kupanda na kushuka.
Salute sana Diamond unatuheshimisha watoto wa uswazi.