GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 63,685
- 128,178
Kama kuna dhana ya Kipumbavu inayowamaliza Watanzania walio Wapumbavu ni hii ya kuamini mambo ya Nyota.Wadau habari zenu? Hili suala la diamond platnumz kuhusishwa na kupoka nyota za wasanii wenzake, hasa wale wanaofanya vizuri kwa kipindi fulani, limeshika kasi sasa.
Hivi karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali mitandaoni kuhusu kupokwa kwa nyota ya msanii Jay melody aliyetamba ni nyimbo kadhaa hapo nyuma.
Wadau wanadai Jay melody baada tu kufanya wimbo wa pamoja na diamond platnumz ndio basi tena, hasikiki tena. Hata akitoa wimbo sasa hivi haufiki mbali kama hapo awali.
Hata hivyo msanii Jay melody amekanusha vikali madai hayo ya kuibiwa nyota yake.
View attachment 3574166
Tunaacha kujituma, kuwa wabunifu na kuendana na hitaji la dunia la sasa ili tujikwamue Kiuchumi tunajikita kuamini mambo ya Nujumu (Nyota)
Acheni tu Rais Trump na Wazungu watudharau Waafrika na kwa Upumbavu huu tunastahili Kudharailika nao.