DIAMOND PLATNUMZ PUNGUZA KIKI

DIAMOND PLATNUMZ PUNGUZA KIKI

Mwishini mwa mwezi wa saba,dunia kama sio Tanzania,tulipata ujumbe kutoka kwa Diamond kwamba kutakua na Birthday party ya mwanae Latifa huko bondeni kwa Madiba!! Party itakua live kupitia channel ya Wasafi tv,bila kupoteza muda haraka nikalipa kifurushi cha miezi mitano,ili nifaidi uhondo!!

Pia akaja na wako kwamba atalipia watoto 30,gharama za kwenda kula bata la nguvu na mtoto mwenzao Latifa,nikasema kumbe mambo ni vipi moto!! Pia tukaambiwa kuna baadhi ya wasanii kama Madame Sepenga na Aunty Ezekiel watapata offer ya kwenda bondeni kwa gharama za Diamond!!

Sasa nauliza mbona kimya sana?? Sijaona picha za Sepenga na Aunty Ezekiel wakiwa bondeni,sijaona, watoto wakipewa tiketi za ndege za kwenda bondeni,au hii kitu ilifanyika kimya kimya??

Bado najiuliza kwa nini unapenda kutoa taarifa mapema,halafu inakuja onekana ni mtu uongo?? Bado tunafikiria fix yako ya kwenda kuimba wimbo maalum wa Welidi kapu,napo ulitupiga kamba!! Badilika punguza stunt utakuja kwama!!
TATIZO MNAPENDA VYA BURE!
 
We hata hujui unakurupukia tu.... mbona tar alitaja? Lawama kibao kumbe ufuatiliaji zero... haya subiria ukaripie kingine maana ni tar 17-19 mzee baba
 
Nakumbuka alijitangaza kuwa atashiriki kuimba katika ufunguzi Wa WORLD CUP, lakini Mimi binafsi sikumuona , sijui kama wenzangu mlibahatika kumuona, Mimi nilimuonak kavaa KIKUKU wanachovaa kina Dada na MAJUNYA mguuni !!
 
Na ww kulipia kifurushi cha miezi 5 then useme hapa ni kiki
 
kiki nyingi walisema amenunua nyumba kijiji mwananamala, eti atanunua helkopta kama a gwajima, haikuonekana, eti aajenga msikiti mkubwa tandale nalo hili sijui lipo?
 
Umbea ndio umekufanya ukalipia hicho kifurushi cha miezi mitano
 
Hayo yote sawa ila hii kiki ya kunyoa voooz na kutangaza daaah!!!! Kuna siku atatuonesha akiwa anapupu huyu mtu
 
mtoa mada acha ubwege, ule wimbo ulikuwa kwa ajili ya coca cola na sio FIFA world cup..
 
Back
Top Bottom