Diamond Platnumz: Tangu niwe na Zari sijatongoza msichana mwingine

Diamond Platnumz: Tangu niwe na Zari sijatongoza msichana mwingine

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Mond.jpg

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa tangu amtongoze mzazi mwenzie, Zari mwaka 2014 ndio ilikuwa mara yake ya mwisho kufanya hivyo hajawahi tena kutongoza mwanamke mwingine.

Diamond Platnumz amesema kuwa hawajahi kutongoza mwanamke mwingine kwa sababu yupo na Zari tofauti na kipindi cha nyuma kabla ya kuwa maarufu.

Akijibu swali kwenye mahojiano yake na Kituo cha Radio cha Kiss FM cha nchini Rwanda, swali lililohoji kuwa alishawahi kukataliwa na mwanamke kabla ya umaarufu wake? Diamond alijibu kwa kusema ‘ndio tena wengi tu kwanini isitokee“.

Na alipoulizwa ni lini mara yake ya mwisho kukataliwa na mwanamke au kusikia neno hapana kutoka kwa mwanamke Diamond Platnumz amesema “tangu nimtongoze Zari, hadi sasa sijawahi kutongoza msichana mwingine“.

Diamond Platnumz wikiendi iliyopita alikuwa nchini Rwanda ambapo akiwa huko alitembelea kituo cha Jordan Foundation kinacholea watoto wenye ulemavu wa macho (Vipofu).

Chanzo: Bongo5
 
hujawai kutembea na mwanamke bila kumtongoza??

anamaanisha wanajigonga tu wenyewe... ila hawatongozi kama zamani

Kuna movie inaitwa Love dont cost a thing.. ya nick canon...

mbinu aliyoitumia kupata wadada ndio mbinu ya diamond...

hujui akili za wanawake wewe...

wanawake wanapenda mashindano.. so ukitoka na mzuri na wanayemkubali sana.. unakuta na wao wanakupa tu ili washindane na mwenzao... so wanashindana na zari kutaka kumpora bwana... ndio diamond anawafaudu tu

Hamisa ilikuwaje?
 
kwa sisi wahenga ambao tunaenda club zinazopiga oldies, kuna ngoma ya Shaggy inaitwa it was not me, Hahahaha! ukiwa Player hata ukikutwa eneo la tukio unatakiwa kukataa kwamba huhusiki[emoji63]
 
hujawai kutembea na mwanamke bila kumtongoza??

anamaanisha wanajigonga tu wenyewe... ila hawatongozi kama zamani

Nani wa kutoa huo usibitisho kama hakutongoza? hizo ni sifa zake za kutaka kuendelea kumpumbaza mwanamke wa Uganda the lady boss kwa kumdiss hamisa aonekane kicheche mbele ya zali

kimpira diamond anacheza mind game kwa zali.
 
Ana mtoto lakin kumtenga huko kubaya vingine kama mwanaume ni kukaa kimya tu akikuwa mtoto wake yule atajisikiaje kwa hayo manyanyaso? wengi tunachakaza mademu bila kupiga saund ila kujisifia ni mwiko.
Hasira za nini?
 
Hasira za nini?

Mm hatar sana kwa hiyo hapo umeona hasira? ili iweje? huyo anamchezea mchezo zali sisi wanume wazinzi tunajua maana ya hiyo kauli yake mdogo wangu hamisa hawezi kumvua nguo mond bila makubaliano ya faragha.
 
hujawai kutembea na mwanamke bila kumtongoza??

anamaanisha wanajigonga tu wenyewe... ila hawatongozi kama zamani
Wanajitongozesha afanyaje sasa.Hana haja ya kutongoza yeye ni almasi wanakuja wenyewe.
 
Kwahiyo kina mabutu walijileta na kujitongozesha wenyewe chibuu utajafia vifuani wakijileta fumuuuaaa nikupita nao tu shobo dundo
 
Tafsiri ni kwamba wanajileta wenyewe mdomoni mwa simba.
 
Back
Top Bottom