Diamond Platnumz, tusamehe Watanzania tumezoea kuitwa 'Kichwa cha mwendawazimu'

Fukara

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2013
Posts
1,625
Reaction score
928
Wasalam wanaJF wenzangu,

Kwanza naomba ni declare interest kuwa mimi ni shabiki wa maendeleo katika nyanja zote. Lakini kwa leo nitazungumzia muziki wetu hapa nchini (Bongoflava). Lakini point yangu nitaielekeza haswa kwa mafahali wawili, yaani Diamond na Slikiba.
na nitachukua reference ya show ya Kiboko Yao iliyodhaminiwa na kampuni ya simu ya Tigo, iliyofanyika jumamosi iliyopita kwenye viwanja vya leaders.

Ni ukweli usiofichika kwamba wasanii wote waliotumbuiza walijitaidi kwa kiwango kikubwa sana, hongera sana kwani kuna changes kubwa sana. Lakini kuna jambo halikuwa sawa katika show ile, alo ni kurushwa makopo stejini wakati Diamond akitumbuiza na hapo ndio hoja yangu inapojengeka.

Bila kuwachosha sana, Diamond ametuwakilisha Watanzania kwenye shoo nyingi za kimataifa, ni nyingi siwezi kuzitaja zote, mbona Wanigeria, Marekani, Canada, Germany, Rwanda, Burundi etc hawakumrushia makopo? Kwanini itokee nyumbani Tanzania? Ni wivu au chuki kiasi gani juu ya msanii huyu mwenye kuheshimika Afrika kwa sasa? Amewakosea Watanzania?

Natambua Watanzania wengi hatupendi kuona mtu anaendelea, tumezoea majungu, fitina, chuki, umbea, na wivu. Jamani tubadilikeni. Maskini ya mungu Diamond huna ugomvi nae unamchukia kwanini? Au alikikiba hata hujawai kumuona unamchukia kakukosea nini?

Nimetafakari nikagundua ndio mana tuko nyuma in everything. Nenda Kenya and see how Jaguar anathaminiwa nchini mwao, Go Uganda and see how Jose Chamilione is respected. Hivi vitu vya team ujinga in negative way ni ushamba uliopita kiwango, inatakiwa team in constructive way.

Tunaomba Alikiba na Daimond washirikiane kuendeleza muziki wetu na kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Samahanini kwa kuwachosha. Asanteni kwa kunisoma.

Nawasilisha
 
ndio tulivyo na tamaa ya kushindwa kwetu....
 
Ali Kiba yupo nyuma ya wale wahuni waliorusha makopo pale Leaders ni wahuni wa Kariakoo kwenye vijiwe wa Kiba na nilisikia akihojiwa clouds hakuonyesha kulaani kitendo kile au kutoa kauli ya kutokukubaliana na kitendo
Ushauri kwa Kiba afanye kazi ili afaidike na kipaji chake kama ilivyo kwa Nasib maana sasa anafaidika na kipaji chake kwa kufanya excellent performance
 
Diamondi ni kijana anayejitambua, kama mafanikio kweli anayo,
Wenye akili zetu timamu tunamkubali.

Hao warusha makopo ungejaribu kuleta picha ya mmojawapo hapa jamvini ili tumlinganishe.

watoto wa kariakoo na jangwani wahuni wachache waliokodiwa ndo waleta vurugu..
 
Ali Kiba yupo nyuma ya wale wahuni waliorusha makopo pale Leaders ni wahuni wa Kariakoo kwenye vijiwe wa Kiba na nilisikia akihojiwa clouds hakuonyesha kulaani kitendo kile au kutoa kauli ya kutokukubaliana na kitendo
Ushauri kwa Kiba afanye kazi ili afaidike na kipaji chake kama ilivyo kwa Nasib maana sasa anafaidika na kipaji chake kwa kufanya excellent performance

nmecheka sana " kwani kulaani lazima jaman sio kosa kisheria. daimond anafanya vizur sana tatizo nyota. maringo na dharau ndio maana vijana wahun wanamchukia yawezekana kiba hahusiki pia kumbuka kuna maadui wengi ambao dai aliokuwa nayo kwenye mahusiano walivyo achana ndo kuwadhalilisha pia hili mliangalie
 
Kwenye biashara ya muziki kuna kitu wadau wanaita 'beef, well done '. Kuna wanaonufaika na hii beef ya Diamond against Ali Kiba, kuna wafanyabiashara wameanza kuandaa maonyesho kama aya ambayo ukiangalia kwa makini walengwa ni awa jamaa wawili ili waitangaze bidhaa yao (kumbukeni tigo awa awa walishawahi kuandaa mpambano wa wanaume halisi vs family), kuna maadui wa awa jamaa wawili ambao wanawatumia kama silaha bila wao kujua kulipa visasi vyao, kuna mashabiki ambao uwa wanapenda tu vurugu so wakipata vivuli vya kujifichia kama hivi wanafurahi sana(ata ukiangalia umu wengi si mashabiki wa dhati wa awa watu).

Ningepata nafasi ya kuwashauri ningewapa ushauri kama huu niliotoa hapa fungua https://www.jamiiforums.com/celebri...ma-nature-na-inspekta-harun-wa-zama-hizi.html kwani kiukweli hii beef inawaathiri wote wawili kwa namna moja au nyingine, kwani ata mahusiano yao na wadau wengine yanaanza kuvunjika mfano nilisikia Kiba alimzuia Dullah wa Planet Bongo kumsalimu, ambaye inafahamika Dullah ni rafiki wa Diamond mkubwa sasa hii inaweza kumuathiri ata kikazi pia niliona sehemu Diva wa Clouds anatoa maneno makali kuhusu Diamond sikuelewa kwa nini lakini inaonyesha ni aya aya mamigogogro. Pia inawaathiri ata kwenye concentration mfano badala ya kuangaika na mambo yatayokuza muziki wao wanaweza kujikuta wanatumia muda mwingi kwenye kupanga mashambulizi kitu ambacho ata muziki wenyewe kitaurudisha nyuma.

All in all, unapoingia kwenye vita kuna kushinda au kushindwa so lazima ujiandae kwa yote ayo ata kama unajiamini kiasi gani.
 
umetiririka point sana mkuu well done
 
Nawaonea huruma tu maana hta maandiko matakatifu yamesema ahukumuye atahukumiwa sambamba na yale yaliyomtoka kuanzia kichwan mpka kinywan mwake, na kwa stail hii tanzania bila maskin itakuwa ngumu
 
Hata nchi zilizoendelea umaskin upo
 
Mbna akipiga shows zingine bila Kiba kuwepo hazomewi??? Isingekua ndio kazi/ajira yake ningemshauri aache kupiga show za ivo aisee
 
Back
Top Bottom