Diamond: Sifikirii kuoa

Kutoka moyoni ? Wakati bimkubwa Wema
Isaac Sepetu akijiaminisha na kuhisi kuwa
amepata mume
ambaye ni baba bora, mwandani wake ,
Nasibu Abdul ‘ Diamond Platnumz ’ amefunguka
kuwa
kamwe hafikirii kuoa, Ijumaa lina
cha kukuhabarisha . Wema Isaac Sepetu akiwa
kwenye pozi la
kimahaba na mwandani wake, Nasibu Abdul ‘
Diamond Platnumz’ Kauli hiyo ya Diamond
inakuja wiki kadhaa baada ya Wema kuonekana
na pete ya ndoa kidoleni kisha kukiri kuvishwa
na ‘ kichaa ’ huyo wa Bongo Fleva ambaye
amerejea kutoka Marekani alikotwaa Tuzo ya
Msanii Bora wa Kiume Afrika
Mashariki zilizokwenda kwa jina la African Muzik
Magazine
( AFRIMMA) 2014 .
Hofu ya kuoa Akizungumza na gazeti hili kwenye
mahojiano maalum, Diamond alisema kuwa
anahofia kuoa kwa madai kwamba akifanya
hivyo anaweza kuanguka kimuziki kitu ambacho
hataki kimtokee maishani
mwake . Kumbe ! Jamaa huyo ambaye siku hizi
anajiita Dangote ( jina la tajiri wa Nigeria , Aliko
Dangote ) alitiririka kuwa zamani alikuwa na
wazo hilo la kuoa lakini akiwatazama
wanamuziki wenzake waliooa mwisho wa siku ,
makali yao hupungua na wengine kupotea kabisa
kwenye ramani ya muziki . Bofya hapa kumsikia
Diamond “Unajua unaweza kuona kama vile
nazungumza kitu cha utani lakini ndiyo ukweli
wenyewe . “Kuna wanamuziki wengi walikuwa
kwenye peak ( kileleni ) lakini walipooa tu ‘ kiki ’
yao ilishuka ghafla katika muziki na wengine
wamepotea kabisa . Nasibu Abdul ‘ Diamond
Platnumz ’ akiwa na
Mtangazaji wa Radio E- FM , Penniel
Mungilwa ‘Penny ’. “Ukifuatilia kwa umakini
wapo mastaa wengi duniani ambao umri
umekwenda sana lakini hawajaoa . Hata hapa
nyumbani kuna mifano hai. Nadhani hofu yao ni
kuona kuwa wakifanya hivyo
watashuka kimuziki, ” alisema Diamond . Ni
kweli kamvisha pete Wema ? Alipoulizwa kama
ni kweli amemvisha pete ya uchumba Wema ,
msanii huyo hakuwa tayari
kufafanua kwa kigezo kwamba pete ni urembo
kama urembo mwingine kwa mwanamke . Nje ya
boksi
Baada ya kusikia msimamo wa Diamond , gazeti
hili lilijiongeza na kutoka nje ya boksi ambapo
lilizungumza na baadhi ya wasanii waliooa
na wasiooa ambapo walieleza mambo
mazito . Jacqueline Wolper
Siri yafichuka Katika mazungumzo yao kwa
sharti la kutochorwa gazetini, wasanii hao
walidai kwamba Diamond anahofia kupoteza kiki
kwa warembo ambao wengi ndiyo mashabiki
wake wanaoamini nao wanaweza kupata zali la
kuolewa naye ndiyo maana humzingira na
kumuomba namba ya simu kila
anakokwenda . Msururu wa mademu Ilielezwa
kwamba kwa kuwa jamaa huyo hupenda
kuwa juu ndiyo maana alisharipotiwa kutoka
na msururu wa wanawake mastaa ambao
huchangia
jina lake kuendelea kuwa juu. Ilidaiwa kwamba
wakati anatafuta namna ya kuchomoka kimuziki
alidaiwa kutoka kimapenzi na warembo
waliokuwa na majina madogo kama Rehema
Fabian aliyepata umaarufu kupitia Shindano la
Miss Kiswahili . Jokate Mwegelo . Ilisemekana
kwamba baada ya hapo alidaiwa kuwa
na msururu wa wanawake mastaa kama
waigizaji Jacqueline Wolper Massawe na Aunt
Ezekiel
Grayson na Jokate Mwegelo . Baadaye jamaa
huyo alidaiwa kuruka na wasichana ambao
hawakuwa na kiki hivyo aliwamwaga ndani ya
muda mfupi kama Najma na Natasha. Baadaye
Diamond alitua kwa Wema hadi akafikia hatua
ya kumvisha pete ya uchumba mwaka
2012 ndani ya Ukumbi wa New Maisha uliopo
Masaki
jijini Dar . Kumbukumbu zinaonesha kwamba
muda mfupi baada ya kumvisha Wema pete ya
uchumba
walimwagana ambapo Diamond alitua
kwa Mtangazaji wa Radio E -FM , Penniel
Mungilwa ‘ Penny’ . Irine Uwoya Diamond
hakudumu na Penny kwa madai
kwamba mrembo huyo hakuwa na kiki kama
ilivyokuwa kwa Wema ambaye jina lake
halijawahi kushuka tangu alipovaa Krauni ya
Miss Tanzania 2006 /07.
Ilisemekana kwamba hata tuzo zilipungua
ndipo akampiga Penny chini na kurudi kwa
Wema ambaye
inasemekana ndiye anayemng ’ arisha . Hawa
wameoa, je , wameshuka ? Baadhi ya mastaa
waliooa ni pamoja na Mohamed Ahmed ‘ Z -Anto
’ , Nurdin Bilal ‘ Shetta ’ , Amini Mwinyimkuu,
Lawrence Marima ‘ Marlaw ’ , Amani Temba ‘
Mheshimiwa Temba ’ na wengineo .
 
Heee umerudi binamu au binam mwingineee

Yule yule binamu, kumbe wachawi kwa wachawi tunajuana eeh? Mwenzangu nimerudi nimeshindwa kuvumilia kabisa maana nimepigwa ban takatifu, yani apa mwili wote umejaa umbea nikasema walahi nikikaa kimya ntakufa warumi mie , nimerud binamu.
 
Yule yule binamu, kumbe wachawi kwa wachawi tunajuana eeh? Mwenzangu nimerudi nimeshindwa kuvumilia kabisa maana nimepigwa ban takatifu, yani apa mwili wote umejaa umbea nikasema walahi nikikaa kimya ntakufa warumi mie , nimerud binamu.

jobless wewe kweli mmbea uliyotukuka.
 
Wema hawezi kuolewa na Domo, anatumika tu!
 
Yule yule binamu, kumbe wachawi kwa wachawi tunajuana eeh? Mwenzangu nimerudi nimeshindwa kuvumilia kabisa maana nimepigwa ban takatifu, yani apa mwili wote umejaa umbea nikasema walahi nikikaa kimya ntakufa warumi mie , nimerud binamu.

Hhhaaa walah nimekariri mwandiko wako loo,mwaga umbeaa,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…