Diamond: Tayari nimeshanunua ndege binafsi (private jet)

Diamond: Tayari nimeshanunua ndege binafsi (private jet)

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Star wa muziki kutoka Tandale haishiwi surprises, kutoka Tandale mpaka kumiliki ndinga za maana kama Rolls royce, escalede mbili na gari yake yenye hadhi ya chini ikiwa ni v8 hizi za mawaziri na wabunge sasa kaja na jipya lengine ambalo kama ni kweli basi si kwamba kapiga hatua bali kachana msamba.

Akiwa anahojiwa kwenye Interview kituo cha DW Africa nchini ujerumani, Diamond alikuwa akizungumzia namna msanii anavyotakiwa kuishi au kuwa ili kupata ile heshima unayostahili na kuingiza mkwanja wa kutosha (msanii unavyotakiwa kujiwekeza mwenyewe)

"Mfano kwa mtu kama mimi ambaye nimetokea mtaani, kwasasa nanunua gari la kifahari lenye thamani hadi tsh. Bilioni 2.3/=... Kwahiyo itabidi ufanye hivyo kwani usipofanya hivyo hawatakuona wewe ni wa thamani (watakuchukulia poa). Na sasa tayari nimeshanunua ndege binafsi (private jet)" - Diamond Platnumz
 
Safi sana.

F4BAC5CF-7371-438A-8832-53B48EA476E6.jpeg
 
Sasa kama ni hii mbona inaonekana kama mbovu au ndio design yake,au atakuwa amenunua used anasubiria kuifanyia matengenezo ndio aje nayo huku...?
roho ya kimasikini hii, ni kama mashabiki wa simba walianza kusema Yanga hawana pesa ya kumsajili Azizi Ki, wakaja kusema picha aliyopiga ya usajili ni edit, haya sasa kafika Yanga wanasema ni mchezaji wa kawaida 😂😂
 
Dalili za kuanza kufulia kumiliki jet sio pole pole maana kupaki Hela kuwa hewani Hela Kila kitu pesa kama baadhi ya nchi nyingi zimeshindwa labda ndugu Mondi anaweza tuonesha mfano

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
roho ya kimasikini hii, ni kama mashabiki wa simba walianza kusema Yanga hawana pesa ya kumsajili Azizi Ki, wakaja kusema picha aliyopiga ya usajili ni edit, haya sasa kafika Yanga wanasema ni mchezaji wa kawaida 😂😂
Jibu swali mkuu,ni mpya au ya mkononi,kununua kitu used sio kwamba ni makosa,ni mipango tu ...?
 
Jibu swali mkuu,ni mpya au ya mkononi,kununua kitu used sio kwamba ni makosa,ni mipango tu ...?
Kwenye ndege hata kama anatumia iliyotumika hapa hakuna msanii wa bongo wa kujaribu kumuiga!!

Hebu jiulize tu ni msanii gani hapa bongo anaendesha hata gari ambayo thamani yake imefikia angalau milioni 575 (robo ya bei ya Rolls royce ya Diamond)
 
Back
Top Bottom