Diamond tena; Youtube wampa zawadi ya ''Gold Play' Button'' kwa kufikisha subscribers milioni moja

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
oiPbymr.png

Kuna jitihada kubwa sana Youtube hufanya ili kutambua bidii na ushawishi ambao wamiliki wa account za youtube wanao, Moja wapo za jitihana hizi ni kuwatunuku zawadi ya “gold play button” watu waliofikisha subsribers zaidi ya milioni moja kwenye channel zao, Kupata subscribers milioni moja sio shughuli ya lele mama na inahitaji uwe zaidi ya competent ili upewe hii gold play ya youtube
6QXNLtg.png

Kuna wengi waliodhani kijana hatoweza na bado wapo wap*mb*vu wengine wasiomtakia mema lakini kijana anaendelea kutia mchanga vitumbua vya hao watu, Kwakweli kijana anatuwakilisha vyema nchi yetu na wengi huwa hatushangai akipendekezwa kuwa rasilimali ya taifa.

Iwe kuchukiwa na wasiompenda, kuitwa majina mabaya, kubanwa na media ama habari za kumchafua huyu dogo hakati tama hadi wengi kumdhania sio mtu wa hii Tanzania, Pindi inapotokea akidhaniwa hawezi kufanya kitu fulani ama akikatazwa kukifanya kwake ni kama unatia mafuta kwenye petroli maana atapambana hadi atekeleze ambayo huwa tunaona hayawezekani kwa wasanii wengi wa Tanzania.

Achilia mbali umaarufu wake ambao nao umechangia kupata hio zawadi ya subscribers milioni 1, Huyu kijana ni mtu anaeweza kuchanganyika na na jamii kwa kutokua na dharau tulizozizoe pindi mtu akiwa star, Kijana kachangamka sana (haboi) na wala hana shobo za kudharau watu kama baadhi ya wapinzani wake.

Yote kwa yote kijana tunampongeza na aendelee kuchapa mzigo na asije kukata tamaa kwajili ya watu ama vitu visvyo na msingi (mfano kelele za teams)

Kama una mawazo aa nyongeza ya ziada ungependa kuongezea karibu sana.
 
Hata Eric Omondi anayo, kazi ni kwako na wewe kafungue Channel tafuta Views hata wa kununua.
 
Mimi ni mmoja wa mshabiki wake!! Nina moja la kushauri hapa!! Hebu Mwambie ajitahidi kufanya kazi zake nje ya majukwaa ya kisiasa! Hilo linampunguzia credit kubwa sana! Mfano kama leo angekuwa neutro bila kufungamana na chama chochote cha siasa basi angekuwa anatunukiwa diamond button kwa kuwa na subscribers 2m+!! Ila kiukweli kiba hana mashabiki wengi wanaopenda kazi zake toka moyoni ila tu wanasupport kwa kuw hawapendi msimamo wa mondi kisiasa!
 
Mkuu vipi kuhusu wewe unapambanaje na maisha na umeshafika level gani? au wewe kila ukiamka unasifia wanaume wenzako tu huku wewe mwenyewe ukibaki palepale ulipo!?
Nauliza tu!
 
Eti kumchafua??
anakichafua mwenyewe kwa mapicha ya hovyo halafu mnasingizia Watu!

Media zinambania!
Mbona zikimpendelea hamsemi?
 
Hata Eric Omondi anayo, kazi ni kwako na wewe kafungue Channel tafuta Views hata wa kununua.
Mimi ni mmoja wa mshabiki wake!! Nina moja la kushauri hapa!! Hebu Mwambie ajitahidi kufanya kazi zake nje ya majukwaa ya kisiasa! Hilo linampunguzia credit kubwa sana! Mfano kama leo angekuwa neutro bila kufungamana na chama chochote cha siasa basi angekuwa anatunukiwa diamond button kwa kuwa na subscribers 2m+!! Ila kiukweli kiba hana mashabiki wengi wanaopenda kazi zake toka moyoni ila tu wanasupport kwa kuw hawapendi msimamo wa mondi kisiasa!

Inabid ujue ya kwamba Diamond platnumz ni brand

Kuna vitu kwenye biashara huwa vinaweza kuzulika na kuvicontoll kama wafanyakazi, mapromoter, manager, n.k

Lakini Kuna vitu ambayo huwezi kuviepuka wala kuvikwepa kwenye shughuli zozote zinazouingizia pesa, Haya mazingira ni

1.Siasa(politics)
2.Hali y uchumi (Economy)
3.Jamii na tamaduni(society & culture)
4.Teknolojia (Technology)
5.Sheria (Legal issues)
6.Environmernt - (Mazingira)

Hapo kwenye siasa Diamond hawezi kuzuia wala kuzikimbia na endapo akienda kinyume brand yake itaharibiwa na wana siasa
 
Mkuu vipi kuhusu wewe unapambanaje na maisha na umeshafika level gani? au wewe kila ukiamka unasifia wanaume wenzako tu huku wewe mwenyewe ukibaki palepale ulipo!?
Nauliza tu!
Maisha yangu yako poa kabisa, Jamii forums ilituwekea haya majukwaa kwa ajili ya kuposti, kusoma posti na kutoa mawazo ya ziada kwa maada husika, waombe moderators wakufungulie jukwaa la kuhoji maisha ya wanajukwa maana humu sio sehemu ya kuhoji maisha yangu
 
Mimi ni mmoja wa mshabiki wake!! Nina moja la kushauri hapa!! Hebu Mwambie ajitahidi kufanya kazi zake nje ya majukwaa ya kisiasa! Hilo linampunguzia credit kubwa sana! Mfano kama leo angekuwa neutro bila kufungamana na chama chochote cha siasa basi angekuwa anatunukiwa diamond button kwa kuwa na subscribers 2m+!! Ila kiukweli kiba hana mashabiki wengi wanaopenda kazi zake toka moyoni ila tu wanasupport kwa kuw hawapendi msimamo wa mondi kisiasa!

Mkuu kupata Diamond play button sio mchezo ni mpaka kufikisha subscribers 10m+
 
Mimi ni mmoja wa mshabiki wake!! Nina moja la kushauri hapa!! Hebu Mwambie ajitahidi kufanya kazi zake nje ya majukwaa ya kisiasa! Hilo linampunguzia credit kubwa sana! Mfano kama leo angekuwa neutro bila kufungamana na chama chochote cha siasa basi angekuwa anatunukiwa diamond button kwa kuwa na subscribers 2m+!! Ila kiukweli kiba hana mashabiki wengi wanaopenda kazi zake toka moyoni ila tu wanasupport kwa kuw hawapendi msimamo wa mondi kisiasa!
We ngengemkeni nambie msanii gani asofanya siasa hapa bongo. Hata akina Jay Z, Didy na wale wakubwa Ulaya unaowajua wanafanya siasa wakati wa uchaguzi mkuu. Sasa Diamond kufanya siasa wakati wa uchaguzi mkuu ushaanza kujifanya mnajimu. Kwani kaanza juzi hizo siasa! Mbona bado anaendelea vyema kutusua? Kama ipo ipo tu mkuu wewe pambana na hali yako. Angekuwa anawakampenia UKAWA hata usingekuja humu kuhorojoka.
 
King kiba yeye alishapata 5million gold play button sema tu hapend show off!
 
Mimi ni mmoja wa mshabiki wake!! Nina moja la kushauri hapa!! Hebu Mwambie ajitahidi kufanya kazi zake nje ya majukwaa ya kisiasa! Hilo linampunguzia credit kubwa sana! Mfano kama leo angekuwa neutro bila kufungamana na chama chochote cha siasa basi angekuwa anatunukiwa diamond button kwa kuwa na subscribers 2m+!! Ila kiukweli kiba hana mashabiki wengi wanaopenda kazi zake toka moyoni ila tu wanasupport kwa kuw hawapendi msimamo wa mondi kisiasa!
Mkuu kwani ALI KIBA ni kada wa chama gani?
 
Maisha yangu yako poa kabisa, Jamii forums ilituwekea haya majukwaa kwa ajili ya kuposti, kusoma posti na kutoa mawazo ya ziada kwa maada husika, waombe moderators wakufungulie jukwaa la kuhoji maisha ya wanajukwa maana humu sio sehemu ya kuhoji maisha yangu
Hahahaha! unachokikataa wewe ndicho unachokifanya kwasasa!! sasa wewe mbona unahoji maisha ya wenzako mkuu? tena mpaka unawaita wapumbavu? anyway nadhani unachokifanya ndio level yako ilipofikia,keep it up!
 
Hata harmorapa ana subscribers zaidi ya milioni moja sema tu hataki tuzo zao.
 
Tafadhar tupeni faida kidogo tusiojua hiyo Button"Gold play"ni ipi na ina faida gani?
 
Back
Top Bottom