Ukitaka kujua ni jinsi gani uwezo wa mtu au wa watu kufikiri ni wa chini kabisa ni kuchangia au kushabikia kitu kidogo sana ambacho siyo significant katika context (muktadha) wa jambo linalojadiliwa.
Katika hoja hii muktadha ni kujua jinsia ya mtoto. Mimi siyo mzuri katika fani ya utabibu, nilitaraji ma great thinker watusaidie kuainisha njia za kuweza kutambua jinsia ili nasi tufaidike. Ninachoshuhudia katika uzi huu ni matusi na kejeli kupitiliza. Wenye ufahamu wa tiba tafadhali tujuzeni wengine tunapata shule hapa.