Diamond umemkosea nini Majizo na E-FM mbona hawachezi nyimbo zenu?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam...
Ukiacha Clouds FM na East Africa radio ambao hawachezi nyimbo za Wasafi lakini kwa sasa wameongezeka E-fm nao hawachezi nyimbo za wasanii wawa safi...
Bado najiuliza hivi Diamond ana wakosea nini hawa watu ambacho kina wafanya wamchukie yeye na group lake?

Clouds Fm kupitia Kusaga walitangaza kuanaza upya na kusahau yote na hivi karibuni wataanza kupiga nyimbo zao..
Radio one wako tofauti kabisa na EA radio ...Radio one wanacheza nyimbo zote za Wasafi.
Bado najiuliza kwanini wamiliki wengi wa radio wanachukia challenge? Kwanini msanii akiendelea kidogo wana lazimisha kila mtu amuone mbaya?

Watangazaji wa E-FM wakiongozwa na Gerald hando wanamchukia sana Diamond hadi wanaonesha wazi....kwenye vipindi...
Gerald hando hutumia hadi ukurasa wake wa insta kumtukana Diamond as if Diamond alimchukulia mke wake.....
Hivi E-FM Diamond amewakosea nini? Mbona amekuwa akiwasupport sana?

Bado na jiuliza Diamond umemkosea nini Majizo?
 
Hii ishu ya kutocheza ngoma za wasafi nadhani kwanza lina pande mbili au zaidi!

1;Kibiashara!
Mmikiki wa chombo hawezi kuendelea kuzipa airtime zaidi nyimbo za wasanii ambao mwisho wa Siku kituo kikiandaa tamasha msanii au mameneja wake wanakaza msanii wake asitokee(hasa kwa hivi vituo vilijikita kiburudani zaidi)
Hii haiingii akilini .. ..

2;Wivu
Hapa kama ilivyo kawaida yetu Wabongo ukifika juu wanataka kukushusha na wanakuwekea mizengwe kibao kwa lengo la kutaka uendelee kua chini yao!

3; Msanii Binafsi
Kuota mapembe na kudharau wale walipmfikisha alipo licha ya kuwa anaweza akasema ni juhudi binafsi ndio zimemfikisha alipo ila ukweli unabaki pale pale Kuna watu (media) zilizomfikisha alipo!
 

Naomba nisaidie nielewe mkuu, media ikimfikisha juu msanii anatakiwa awe mtiifu mpaka lini? Na msanii kuota mapembe ndio uwa anakuaje mpka nyimbo zake zinaachwa kupigwa?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wiki iliyopita nilikuwa nasikiliza jahazi clouds fm walipiga nyimbo ya mboso hodari nilibaki mdomo wazi nikahisi labda jamaa wamebugi hivi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawala wasizigonge watu wanazifuata youtube [emoji1012][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] na wanazigongaaa wasafi tv na fm [emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
You nailed it all ... umegusa kila nyanja .. umeweka mapenzi kando nakuiacha akili ifanye kazi yake ipaswavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haiwezekani vituoe vyote vimechukie mtu m1 lazima atakuwa na matatizo tu,mbona kiba redio zote wanapiga? Tatizo la Domo baada ya kushika masimbi anataka aabudiwe....Aangalie wenzake mtoni mabilionea kweli wanamiliki mansions,magari kama yote,big bizness lakini wanaheshimu vyombo vya habari.
 
Diamond hana shida na mtu,naamini ukifatilia vizuri utagundua hao mameneja wake ndiyo wanakorofisha mambo.
Nafikiri una hisi lakini mimi sijasikia kama kuna ugomvi wowote kwa sasa kati ya mameneja wa diamond na EFM? hao mameneja wameanza kuwa wabaya na wagomvi baada ya Diamond kuanza kufanikiwa?
 
Ckuiz watu tunatumia technology sasa kuna app kibao zenye update za new song #hii haiwez mshusa mtu yeyote

Sent using Jamii Forums mobile app
Kibaya zaidi kila wanapo acha kucheza nyimbo zake ndio kwanza yeye na wasanii wake wanazidi kufanikiwa....Bado najiuliza Diamond ana wakosea nini?
 
Kimsingi radiuo nyingi kuanzia watangazaji na Madj ni mashabiki wa kiba na kwanini tusiseme hawa wamiliki wa radio wanapenda kuabudiwa na kuliliwa? nilishangazwa siku moja kumsikia Gerald hando akionesha chuki kubwakwa diamond.
Hivi kwanini mtu akifanikiwa anapachikwa jina ana dharau?
 
Nawala wasizigonge watu wanazifuata youtube [emoji1012][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] na wanazigongaaa wasafi tv na fm [emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji881][emoji4]

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kibaya zaidi watangazji wao wataziweka kwenye simu kama watangazaji wa Clouds
 
Wiki iliyopita nilikuwa nasikiliza jahazi clouds fm walipiga nyimbo ya mboso hodari nilibaki mdomo wazi nikahisi labda jamaa wamebugi hivi...

Sent using Jamii Forums mobile app
Kusaga kabla ya kumaliza mwaka 2018 alisema ana anza upya ana samehe kila jambo hataki tatizo na mtu sema shida iko kwa madj na watangazaji wake bado wana kinyongo lakini wamesha ruhusiwa kucheza nyimbo zao ......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…