Naungana na wote waliotoa maoni tena ni mazuri na yana afya masikioni mwetu.
Kwaupande wangu (ni maoni tu) sio kama kuna ugomvi na kati ya redio na redio lah, sina neno moja la kitaalamu ambalo linatumika kwa nitakachokisema.
Kundi linaitwa Wasafi, Rekodi Lebo, inaitwa Wasafi, Redio inaitwa Wasafi, Televisheni inaitwa Wasafi. Nini maana yake? Jibu ni Wasafi ni Brand (bidhaa) Nijuavyo itakuwa nivigumu hilo neno Wasafi kutajwa kwenye redio stesheni nyingine hasa zilizosajiliwa kutoa burudani, wanaita muingiliano wa maslahi, nisawasawa wanaifanyia promosheni bidhaa ya Wasafi.
Mo Dewji akianzisha kituo cha redio, kwenye mazungumzo ya watangazaji wake hawawezi kutamka neno Mo Faya (hichi kinywaji cha Ali Kiba) au uvae T- shirt ya Vodacom uwe unafanyakazi Zantel. Au kipindi kilichodhaminiwa na Airtel kikiwahewani halafu kuna tangazo linalosomwa mwisho wa tangazo kuna namba za simu (0625 ******) hauwezi kusikia mtangazaji akitamka " wapigie kwenye Halotel.... atakuwa amefanya promosheni.