Diamond unarudia kosa lile lile

Diamond unarudia kosa lile lile

Kajamaa haka utandale bado upo kichwani lakini hongera kwa hatua mondi
 
Tumpe heko anajitahidi kufikia levo flani kivyake,hata hii video ikitoka utaona RR karelax anachana mashairi yake kiungwana taratibu. Angalia ndugu yetu anavyoahangaika, yaani km vile yuko jukwaa la fiesta na RR.
Mziki hatujasikia labda inawezekana ni tangazo tu la kinywaji Be llaire.
 
Diamomd Mimi ni shabiki Wako Tena shabiki wako mkubwa! Nafurahishwa na Juhudi zako nafurahishwa na Utendaji kazi wako! Juhudi zako za kufanya Collabo na wasanii wakubwaa inanitia moyo na kunifurahisha kuona kuwa ni kijana mchapakazi

Nimeshtushwa Leo nilipo amka na kuona kwenye Mitandao ya kijamii video zako za video shooting na Rickross zimesambaaa sana! picha mlizo piga wakati wa kushoot video zimesambaa sanaa! Kwanini Diamond Kwanini unarudia kosa lile lile ulilo Fanya kwa Neyo? Hadi wimbo wako wa Marry you ukavujaa na ukakosa mvuto kwa watu? ule ni wimbo mkubwa sana kama ungeutoa kama ulivyo Toa HALLELUJAH! Japo video zako na Rickross ume mute lakini unatoa mwanya wa watu kutokuwa na attention na Wimbo wako

Vile Rickross kukupost tuu ilikuwa inatosha kilicho fuata ilikuwa ni wewe kuja kuachia official video ukiwa na yeye na sio hizi clipp! watu washaona umevaaje kwenye video rickross kavaaje na mengine mengi! sasa yote hiyo ya nini Jamani?

kwanini unarudia kosa lile lile ulilolifanya kwa Neyo? ur Big star huhitaji hizi clip kuja kuboost mziki wako kwa sasa wala wewe kufanya collabo na Rick rosse sio ajabu,Alishafanya na Kina P squre na ulifanya collabo na psqure ajabu nini wewe kufanya na Rickrosee?
mkuu mbona Rick Ross ndo alianza kupost hadi wimbo tena alikuwa studio ww hukuiona? hata ivyo Sallam ndo kiherere sn hii ilitakiwa iwe km suprise backage ila sio mbaya
 
Si mtoe video zenu ziwe surprise, acheni kuwapangia watu kazi zao.
 
Si mtoe video zenu ziwe surprise, acheni kuwapangia watu kazi zao.
tunaongea kama mashabiki ambao ndo tunamuweka mjini huyo Pimbi...mashabiki wa mpira wanapanga mpaka sub za wachezaji na ilhali wenyewe wapo ulaya huko na hata akili zao hawajui kama wana mashabiki Tanzania.
 
tunaongea kama mashabiki ambao ndo tunamuweka mjini huyo Pimbi...mashabiki wa mpira wanapanga mpaka sub za wachezaji na ilhali wenyewe wapo ulaya huko na hata akili zao hawajui kama wana mashabiki Tanzania.


Diamond ni [HASHTAG]#selfmade[/HASHTAG], we unamshabikia kwa vile kazi zake nzuri. Unamuweka mjini mtu unayemlipia kodi ya nyumba, lakini watu wengine wote wako mjini kwa kazi zao na mzunguko wa maisha. Ni sawa leo useme unamuweka mjini konda wa daladala kwa vile unalipa nauli, hiyo haimake sense.
 
Back
Top Bottom