Diamond usiwapuuze wanaokuandama sasa, hao sio shilawadu au Konde Gang. Chukua hoja zao

Diamond usiwapuuze wanaokuandama sasa, hao sio shilawadu au Konde Gang. Chukua hoja zao

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
DIAMOND USIWAPUUZE KINA KIGOGO NA WANAMTANDAO, HAO SIO KINA KONDE NA SHILAWADU

Na, Robert Heriel

Diamond hapaswi kupuuza hii movement ya Wanaharakati wa kimtandao na wanasiasa, asije akafikiri kundi hili nila Wale Wasanii wenzake ambao hata shule hawajaenda.

Diamond anapaswa Ajue kuwa Wanaharakati wa mtandaoni ni wasomi tena sio wakubahatisha, wana-exposure ya hali ya juu kumshinda hata yeye mwenyewe.

Kama ningeambuwa nimshauri Diamond kuhusiana na kile kinachoendelea mtandaoni ningemwambia aombe radhi hata ya kinafiki kwani yote anayotuhumiwa ni kweli.

Diamond anapaswa Ajue kuwa kundi hili ndilo lile lile lililokuwa linamshambulia Mwendazake bila kukoma mpaka dakika ya mwisho kabisa bila kujali athari zozote. Ikiwa kundi hili lilimudu kumkabili Mkuu. WA nchi lazima Diamond afikiri mara mbili mbili asifikiri Kama mtoto mdogo.

Simtishi Ila namtahadharisha ili achukue hatua zinazostahili. Nafikiri Diamond Kama atazichukua hoja za hawa wanamtandao akazifanyia kazi atakuwa msanii Bora zaidi kuliko akizipuuza.

Ni kweli kabisa Diamond hakuweza kuzungumzia uonevu na ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanyika miaka ya 2016 - 2019 zaidi ya yote alitoa kibao kisemacho ACHA NIKAE KIMYA.

Diamond asije akadhani hawa wanamtandao ni Wale kina Konde na shilawadu

Diamond lazima aangalie hili kundi linaloongozwa na #Kigigo_kigogo, na wenzake halijawahi kushindwa katika movement wazifanyazo.

Hilo kundi asilipuuze na Kama atalipuuza basi Ajue anafanya makosa makubwa yatakayo mgharimu pakubwa mno.

Diamond asilione kundi hilo Kama watafuta Kick Kama yeye na wenzake kwani kundi hilo halitegemei kick.

Management ya Diamond na washabiki wake ambao kimsingi nafahamu wengi wao wanafikiri kuwa kila anayemkosoa Diamond ni haters wabadilishe huo mtazamo.

Hakuna anayemchukia Diamond labda Wasanii wenzake huko.

Diamond unachopaswa kufanyia KAZI ni madai ya hao Wanaharakati wa mitandaoni.

Wanamtandao hawakatai Diamond kuwa CCM hiyo ni Haki yake Kama apendavyo, lakini tatizo ni diamond kushindwa kutetea maslahi na haki ya jamii yake pale zinaposiginwa.

Diamond Kama anaakili aichukue hii Kama changamoto na ajifunze ili wakati mwingine aweze kutetea maslahi na haki za jamii yake wakiwemo Wasanii.

Lakini Kama atashupaza shingo yake Nina uhakika Diamond huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho wake.

Diamond akileta mawazo ya mwendazake akidhani kila anayemshauri na kumkosoa ni hater basi anguko lake halipo mbali.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
 
Kabisa Mkuu ,nilitoa ushauri wangu Dayamondi akae mbali na mipasho na siasa kwenye mitandao ,atumie mtandao kupost kazi zake tu!! Kigogo ni mtu mbadi akili kubwa ile anajua mambo ambayo dayamond na crew yake wote hawatakuja kuyajua, umeshauri vyema.
 
Yaani aombe radhi kisa hakuisapoti chadema ila aliisapoti sisiemu, upuuzi kabisa! Ungewashquri hao unaowaita wasomi wanaharakati wa-mind their own eff business...

Wapi nimesema hayo?

Madai ya wanamtandao unayajua??

Hakuna ambaye anampangia mtu chama.
Uwe CCM uwe Upinzani uzalendo ni kutetea maslahi na haki za jamii yako.
Na hiyo ndio agenda.

Kama hujaelewa naomba nkupishe
 
Back
Top Bottom