Brothers Karamazov
Senior Member
- Jul 13, 2023
- 152
- 393
Sikusudii mjadala wa 'Team' za washabiki.
Kwa kawaida wanamuziki wote wakubwa duniani, huwa wanalo kundi fulani la kijamii ambalo huko hukubalika zaidi. Walalahoi na waduni kielimu-Uswahilini huwa na aina yao ya wanamuziki ambao huwahusudu, vivyo hivyo jamii za wasomi na 'mabwenyenye'-ushuani.
Nenda Congo, Jb Mpiana anakubalika sana na Wasomi na matajiri huku Werason akikubalika na 'Walalahoi'. Mfano UB40 hupendwa zaidi na 'wapenda Reggae wa Ushuani' kuliko 'wale wa uswahilini'.
Turudi kwetu. Diamond na WCB wameshajitanabaisha kuwa wao 'uswahilini' ndio nyumbani-sikiliza mashairi na mahadhi ya Muziki wa wanamuziki wote wa WCB. Alikiba, ukifanya tathmini utakuta anasikilizwa zaidi Masaki kuliko Diamond.
Ili uwe mwanamuziki mkubwa na endelevu, ni lazima ujitanabaishe/ujifungamanishe na tabaka jamii fulani.
Harmonize, mnamuweka kwenye kundi lipi kiufuasi?
cc: @luambomakiadi @kingkongIII @theboywonder GENTAMYCINE et al.