Diamond v/s Kiba

Malisa Godlisten

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
201
Reaction score
1,540
Haya ni maoni ya rafiki yangu Benson Tembo ambayo nakubaliana nayo kwa 100%.
____________________________________

Ali Kiba na Diamond ni sawa na sukari na chumvi au chumvi na sukari, (vyovyote utakavyoamua kuiweka).Yaani namaanisha kuwa hawa watu wawili wana ladha zinazotofautiana ambazo zote ni tamu na muhimu kutegemeana tu na mazingira na wakati.

Wakati wa asubuhi ukihitaji kunywa chai, utahitaji sukari kwaajili ya kunogesha chai yako, ukiweka chumvi kwenye chai unaharibu na hautafurahia chai yako. Na katika mazingira hayo unaweza ukadhani kuwa chumvi haina maana.

Ngoja ufike wakati wa chakula cha mchana utakapohitaji kula ugali na nyama, hapo ndipo utakapouona umuhimu na utamu wa chumvi. Wakati huo hautahitaji sukari, kuweka sukari kwenye nyama ni kuharibu kabisa utamu wa nyama.

Kwahiyo kuipenda sukari hakukuzuii kuipenda chumvi kwasababu chumvi haiwezi kuwa mbadala wa sukari na wala sukari haiwezi kuwa mbadala wa chumvi. Kumbe pia, Ali Kiba hawezi kuwa mbadala wa Diamond na Diamond naye hawezi kuwa mbadala wa Ali Kiba kutokana na ukweli kwamba wote wawili wana ladha tamu lakini zenyekutofautiana vionjo.

Hivyo kuzipenda kazi za Diamond hakukuzuii kuzipenda kazi za Ali Kiba na kinyume chake. Kwa wapenzi wa muziki mzuri hawawezi kuwa Team Kiba au Team Mond, wao watasimama katikati wakisubiria muziki mzuri bila Kujali umetoka kwa nani.

[HASHTAG]#MyTAKE[/HASHTAG]:
Falsafa yangu ya maisha na ambayo haitabadilika siku zote ni kuwa SIAMINI KUPANDA NGAZI KWA KUMSHUSHA MWINGINE. Hilo siamini na siwezi kufanya hivyo. Napenda nyimbo za Kiba lakini pia napenda baadhi ya nyimbo za Diamond. Kwenye gari yangu na hata nyumbani nacheza nyimbo za Kiba na za Diamond.

Naamini katika ustawi wa wote wawili. Siamini kwamba ili mmoja anawiri inabidi mwingine afutike. No. Never. Kama ambavyo siamini kufilisi matajiri ndio kutafanya maskini kuwa matajiri, ndivyo ambavyo siamini kwamba kumshusha Kiba/Diamond ndio kutafanya mmoja wapo awe msanii mzuri. Maskini hawezi kuwa tajiri kwa kumchukia tajiri. Kumchukia Kiba hakumfanyi Diamond kuwa bora, wala kumchukia Diamond hakumfanyi Kiba kuwa bora.

Kwangu mimi wote ni wazuri, wote ni mahiri, wote wanafanya muziki mzuri. Imani yangu ni kuwa wote wanaweza kuendelea kufanya vizuri bila mmoja kulazimisha kumshusha mwezie.

Simba haihitaji kuishusha Yanga daraja ili iwe timu bora, wala Yanga haihitaji kuishusha Simba ili iwe timu bora. Never. Ushindani ni muhimu, lakini ushindani mzuri ni wenye staha, wenye ubunifu, wenye bidii. Sio huu ushindani unaoendelea huku mitandaoni wa matusi, kashfa, kejeli na mipasho. Huo si usishani, ni uhuni.

Watu wanaojitambua wanapenda muziki mzuri wa Kiba, lakini hawaachi kupenda muziki mzuri wa Diamond (and the vice versa). Ila kwa wasiojitambua ili wampende Kiba watamtukana Diamond, na ili wampende Diamond watamtukana Kiba.

Eti wanajiita timu Kiba na Team Diamond. Hivi kumbe TZ kuna watu wanamiliki timu? Kina Abramovich wanaomiliki Chelsea wasemeje, kama wewe una kasimu ka mchina na unatoa mapovu kwamba una timu?

Achana na timu za kijinga. Timu bora ni kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi yako, familia yako na taifa lako. Diamond akitoa wimbo mzuri burudika, enjoy. Kiba akitoa wimbo mzuri burudika, enjoy. Habari za timu waachie kina Haji Manara na Masau Bwire.!
 
umenielewa kweli?
Mbona maelezo yako yapo straight kabisa. Kwanini ulaumu babu tale!? Wakati tunaongelea music!?
Ali kiba na Diamond ni watu wawili tofauti. Kila mmoja anaradha yake ya music.
 
Ya siasa yamewashinda.. sasa mnakimbilia kutafuta kiki kupitia wanamuziki.. mie yangu macho na kucheka.. eeeeh
 
Tatizo ma miziki yetu yana ushirikina mwingi sana, ata sishangai vimbweka vinavyoonekana iwe social media au uraiani. Watu watafanya kazi za kukomoana kwa sababu hawajui nn wanatafuta, mfano diamond ame achieve mambo mengi mazuri kwenye muziki lkn hawezi kubaki salama na mafanikio yake kwa sababu mwanzo alivyoingia kwenye huo muziki, Je! Aliingiaje ingiaje? Muda ni rafiki mzuri kwenye kupata matokeo, vilevile muda siyo rafiki mzuri kwa sababu unakutupa mkono.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwaiyo unataka kusema tunguli za diamond zimeisha nguvu?
 
Shukran mleta uzi.
Tatzo smartphone zinatubomoa badala ya kutujenga.

Philips X2560
 
mimi naupenda nyimbo 'ukimwona' na 'kesho' sana.. lakini namkubali kiba zaidi ya diamond
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…