Diamond v/s Kiba

Diamond v/s Kiba

kwaiyo unataka kusema tunguli za diamond zimeisha nguvu?
SEDUCE MAMA IKO WAPI MTAANI HUKUU

BINADAMU WABAYA JAMANI,MMEMSHIKA MKONO KUPOFU ALI KIBA

MMEMUACHA NJIA PANDA HAJUI AFANYEJE

MNATAKIWA KILA SIKU MFANYE KAMA MLIVYO FANYA JMOS

WALAU HATA MPIGE KIDOGO HUKU MTAANI AMBAPO KILA KONA ZILIPENDWA
 
hakuna mziki wowote dunian usiousisha bifu za wasanii..inategemea ni bifu la aina gan
 
Haya ni maoni ya rafiki yangu Benson Tembo ambayo nakubaliana nayo kwa 100%.
____________________________________

Ali Kiba na Diamond ni sawa na sukari na chumvi au chumvi na sukari, (vyovyote utakavyoamua kuiweka).Yaani namaanisha kuwa hawa watu wawili wana ladha zinazotofautiana ambazo zote ni tamu na muhimu kutegemeana tu na mazingira na wakati.

Wakati wa asubuhi ukihitaji kunywa chai, utahitaji sukari kwaajili ya kunogesha chai yako, ukiweka chumvi kwenye chai unaharibu na hautafurahia chai yako. Na katika mazingira hayo unaweza ukadhani kuwa chumvi haina maana.

Ngoja ufike wakati wa chakula cha mchana utakapohitaji kula ugali na nyama, hapo ndipo utakapouona umuhimu na utamu wa chumvi. Wakati huo hautahitaji sukari, kuweka sukari kwenye nyama ni kuharibu kabisa utamu wa nyama.

Kwahiyo kuipenda sukari hakukuzuii kuipenda chumvi kwasababu chumvi haiwezi kuwa mbadala wa sukari na wala sukari haiwezi kuwa mbadala wa chumvi. Kumbe pia, Ali Kiba hawezi kuwa mbadala wa Diamond na Diamond naye hawezi kuwa mbadala wa Ali Kiba kutokana na ukweli kwamba wote wawili wana ladha tamu lakini zenyekutofautiana vionjo.

Hivyo kuzipenda kazi za Diamond hakukuzuii kuzipenda kazi za Ali Kiba na kinyume chake. Kwa wapenzi wa muziki mzuri hawawezi kuwa Team Kiba au Team Mond, wao watasimama katikati wakisubiria muziki mzuri bila Kujali umetoka kwa nani.

[HASHTAG]#MyTAKE[/HASHTAG]:
Falsafa yangu ya maisha na ambayo haitabadilika siku zote ni kuwa SIAMINI KUPANDA NGAZI KWA KUMSHUSHA MWINGINE. Hilo siamini na siwezi kufanya hivyo. Napenda nyimbo za Kiba lakini pia napenda baadhi ya nyimbo za Diamond. Kwenye gari yangu na hata nyumbani nacheza nyimbo za Kiba na za Diamond.

Naamini katika ustawi wa wote wawili. Siamini kwamba ili mmoja anawiri inabidi mwingine afutike. No. Never. Kama ambavyo siamini kufilisi matajiri ndio kutafanya maskini kuwa matajiri, ndivyo ambavyo siamini kwamba kumshusha Kiba/Diamond ndio kutafanya mmoja wapo awe msanii mzuri. Maskini hawezi kuwa tajiri kwa kumchukia tajiri. Kumchukia Kiba hakumfanyi Diamond kuwa bora, wala kumchukia Diamond hakumfanyi Kiba kuwa bora.

Kwangu mimi wote ni wazuri, wote ni mahiri, wote wanafanya muziki mzuri. Imani yangu ni kuwa wote wanaweza kuendelea kufanya vizuri bila mmoja kulazimisha kumshusha mwezie.

Simba haihitaji kuishusha Yanga daraja ili iwe timu bora, wala Yanga haihitaji kuishusha Simba ili iwe timu bora. Never. Ushindani ni muhimu, lakini ushindani mzuri ni wenye staha, wenye ubunifu, wenye bidii. Sio huu ushindani unaoendelea huku mitandaoni wa matusi, kashfa, kejeli na mipasho. Huo si usishani, ni uhuni.

Watu wanaojitambua wanapenda muziki mzuri wa Kiba, lakini hawaachi kupenda muziki mzuri wa Diamond (and the vice versa). Ila kwa wasiojitambua ili wampende Kiba watamtukana Diamond, na ili wampende Diamond watamtukana Kiba.

Eti wanajiita timu Kiba na Team Diamond. Hivi kumbe TZ kuna watu wanamiliki timu? Kina Abramovich wanaomiliki Chelsea wasemeje, kama wewe una kasimu ka mchina na unatoa mapovu kwamba una timu?

Achana na timu za kijinga. Timu bora ni kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi yako, familia yako na taifa lako. Diamond akitoa wimbo mzuri burudika, enjoy. Kiba akitoa wimbo mzuri burudika, enjoy. Habari za timu waachie kina Haji Manara na Masau Bwire.!

Mbona hata wewe una timu kwenye siasa.
vivyo hivyo
kwenye musiki kuna timu
kama ilivyo pia kwenye
mpira kila mtu ana timu.
Tatizo liko wapi?
 
Hii inawahusu wapenda good music nikiwa mmoja wapo bila kujali na kuweka timu zetu.

Mziki mzuri hauzuiliki kuusikiliza hata kama humpendi muimbaji wake
By
Classic
 
ni sawa na mzalendo wa kweli hatajali uchadema wala uccm

be genuine...usitukane watu wala wa vyama vingine
 
Mbona maelezo yako yapo straight kabisa. Kwanini ulaumu babu tale!? Wakati tunaongelea music!?
Ali kiba na Diamond ni watu wawili tofauti. Kila mmoja anaradha yake ya music.
Ukimtaja mondi ktk swala music huwezi kumwacha meneja wake kama tulivyowaya Kiba na mondi hatukosi kuzizungumzia timu ZAO ila wewe ushabiki ndio uliokusukuma kulaumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mimi naupenda nyimbo 'ukimwona' na 'kesho' sana.. lakini namkubali kiba zaidi ya diamond
Wewe jamaa utakuwa pacha wangu. Hizo ngoma 2 za Mond hunambii kitu! Na siamini kama ipo siku ntakuja kupenda nyimbo ya Mond zaidi ya hizo 2!

Napenda pia nyimbo za Kiba. Na zipo baadhi najua kabisa hapa Kiba kazingua, mf mpk leo sijaelewa Kiba alitaka kusema nini ktk MSINISEME, ule anaosema anapenda kula!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta uzi uko sahihi ktk suala LA umuhimu wa chumvi na Sukari lakini naona umesahau kwamba ktk matumizi ya sukar iwe kwenye Chai au kitu kingine chochote kinachoungwa kwa Sukari bado huwa Kuna viongeza ladha mfano kwenye Chai huwa tunaweka na majani,iriki au mdalasini nk,na kwenye chakula licha ya chumv Kuna ndimu,pilipili nk ili kutengeneza ladha ya ziada.vivyo hivyo ktk muziki wa wawili hawa uwepo wa team na upinzan ni kiongeza ladha muhimu kinachosisimua hata mapokeo ya kaz za wawili hawa,leo hii seduce me isingepokelewa kwa kishindo hiki kama isingekuwa maneno maneno ya timu hz mbili,lakini hata Wao pia wanatakiwa wawe na ubunifu wa kuhakikisha wanazitumia timu zao kufaidika kibiashara na sio kufaidika na matusi tu. Timu hizi ndizo zinazomfanya hata msanii mwenyewe Kuumiza kichwa Kuja na mziki mzuri zaidi ya mwenzie ili kuinyamazisha timu nyingine. Mimi ni timu diamond aisee [emoji3][emoji3][emoji3]
 
yaani mimi niwe ukawa halafu niipende ccm??Naanzaje kwa mfano???[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

natania wakuu
 
Haya ni maoni ya rafiki yangu Benson Tembo ambayo nakubaliana nayo kwa 100%.
____________________________________

Ali Kiba na Diamond ni sawa na sukari na chumvi au chumvi na sukari, (vyovyote utakavyoamua kuiweka).Yaani namaanisha kuwa hawa watu wawili wana ladha zinazotofautiana ambazo zote ni tamu na muhimu kutegemeana tu na mazingira na wakati.

Wakati wa asubuhi ukihitaji kunywa chai, utahitaji sukari kwaajili ya kunogesha chai yako, ukiweka chumvi kwenye chai unaharibu na hautafurahia chai yako. Na katika mazingira hayo unaweza ukadhani kuwa chumvi haina maana.

Ngoja ufike wakati wa chakula cha mchana utakapohitaji kula ugali na nyama, hapo ndipo utakapouona umuhimu na utamu wa chumvi. Wakati huo hautahitaji sukari, kuweka sukari kwenye nyama ni kuharibu kabisa utamu wa nyama.

Kwahiyo kuipenda sukari hakukuzuii kuipenda chumvi kwasababu chumvi haiwezi kuwa mbadala wa sukari na wala sukari haiwezi kuwa mbadala wa chumvi. Kumbe pia, Ali Kiba hawezi kuwa mbadala wa Diamond na Diamond naye hawezi kuwa mbadala wa Ali Kiba kutokana na ukweli kwamba wote wawili wana ladha tamu lakini zenyekutofautiana vionjo.

Hivyo kuzipenda kazi za Diamond hakukuzuii kuzipenda kazi za Ali Kiba na kinyume chake. Kwa wapenzi wa muziki mzuri hawawezi kuwa Team Kiba au Team Mond, wao watasimama katikati wakisubiria muziki mzuri bila Kujali umetoka kwa nani.

[HASHTAG]#MyTAKE[/HASHTAG]:
Falsafa yangu ya maisha na ambayo haitabadilika siku zote ni kuwa SIAMINI KUPANDA NGAZI KWA KUMSHUSHA MWINGINE. Hilo siamini na siwezi kufanya hivyo. Napenda nyimbo za Kiba lakini pia napenda baadhi ya nyimbo za Diamond. Kwenye gari yangu na hata nyumbani nacheza nyimbo za Kiba na za Diamond.

Naamini katika ustawi wa wote wawili. Siamini kwamba ili mmoja anawiri inabidi mwingine afutike. No. Never. Kama ambavyo siamini kufilisi matajiri ndio kutafanya maskini kuwa matajiri, ndivyo ambavyo siamini kwamba kumshusha Kiba/Diamond ndio kutafanya mmoja wapo awe msanii mzuri. Maskini hawezi kuwa tajiri kwa kumchukia tajiri. Kumchukia Kiba hakumfanyi Diamond kuwa bora, wala kumchukia Diamond hakumfanyi Kiba kuwa bora.

Kwangu mimi wote ni wazuri, wote ni mahiri, wote wanafanya muziki mzuri. Imani yangu ni kuwa wote wanaweza kuendelea kufanya vizuri bila mmoja kulazimisha kumshusha mwezie.

Simba haihitaji kuishusha Yanga daraja ili iwe timu bora, wala Yanga haihitaji kuishusha Simba ili iwe timu bora. Never. Ushindani ni muhimu, lakini ushindani mzuri ni wenye staha, wenye ubunifu, wenye bidii. Sio huu ushindani unaoendelea huku mitandaoni wa matusi, kashfa, kejeli na mipasho. Huo si usishani, ni uhuni.

Watu wanaojitambua wanapenda muziki mzuri wa Kiba, lakini hawaachi kupenda muziki mzuri wa Diamond (and the vice versa). Ila kwa wasiojitambua ili wampende Kiba watamtukana Diamond, na ili wampende Diamond watamtukana Kiba.

Eti wanajiita timu Kiba na Team Diamond. Hivi kumbe TZ kuna watu wanamiliki timu? Kina Abramovich wanaomiliki Chelsea wasemeje, kama wewe una kasimu ka mchina na unatoa mapovu kwamba una timu?

Achana na timu za kijinga. Timu bora ni kufanya kazi kwa bidii kwa maslahi yako, familia yako na taifa lako. Diamond akitoa wimbo mzuri burudika, enjoy. Kiba akitoa wimbo mzuri burudika, enjoy. Habari za timu waachie kina Haji Manara na Masau Bwire.!
Umeongea maneno mengi ila kuna vitu vya muhimu umeviacha.... inawezekana umeviacha kwa makusudi au kwa bahati mbaya..... ukiangalia wazi kabisa jambo ulilongea sina uhakika ni muhimu kwamba team zife ila kimantiki haiwezekani.... kwa sababu ili yawepo maendeleo ya kitu flani lazima kiwepo kitu ambacho kinapinga....(ili iwepo motion lazima iwepo na frictional force kwa Wanasayansi washaelewa...) na kitu ambacho kitaonyesha upinzani ni watu ambao wanasapoti kile kitu.... Nahisi itakuwa umesahau....NAKUOMBA UKITULIA UUFAFANUE KAULI HII "ili ufanikiwe unahitaji marafiki na ili ufanikiwe zaidi unahitaji...... " halafu tafakari....
Hivyo wazo la kusema timu zife ni njia moja wapo ya kuondoa mafanikio.... pia hadhi ya kitu.....
Jambo halisi nilokusudia ni hili..... Mtoa post bado umelalia sehemu moja umelalia kulaumu washabiki wakati wao sio kosa lao... mashabiki maisha yote wanangalia kile wanachokishabikia..... NAOMBA UVUTE PICHA URUDISHE KUMBU KUMBU NYUMA... kwa mfano leo tukiangalia Tanzania hakuna asiejua kwamba Kuna umoja wa UKAWA...ambao unaunganisha baadhi ya vyama.... vuta picha hapo mwanzo vyama hivi kabla ya kuungana vilikuwa vipi..? kila kiongozi akipanda jukwaani anakiponda chama chengine na wananchi walikuwa wapo vipi...? Je mbona walipoamua kuungana na wananchi nao wakapatana moja kwa moja....
Tukiachilia mbali kwenye mitandao... Mimi binafsi yangu nimeangalia.... nimesikilliza kazi zote ila sijawahi kuiona au kusikia kazi ya Ali kiba ikizungumza neno la kumdiss Diamond.... ila nikisikiliza kazi za Diamond anazungumza wazi kumdiss Ali kiba.... Kwa hali hiyo unahisi team zitakuwa ktk hali gani.... nimetoa mfano tuu japo kama kuna watu watakuja kusema nipo timu fulani nimelalia upande fulani... ila nimetoa mfano ulio wazi kabisa........
Naomba uangalie tn post yako kwa usahihi.... huku kwetu tuna msemo usemao.... "Usimharamishe kasa ukamhalalisha kaa"
Ni hayo tuuu...Shukran....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEDUCE MAMA IKO WAPI MTAANI HUKUU

BINADAMU WABAYA JAMANI,MMEMSHIKA MKONO KUPOFU ALI KIBA

MMEMUACHA NJIA PANDA HAJUI AFANYEJE

MNATAKIWA KILA SIKU MFANYE KAMA MLIVYO FANYA JMOS

WALAU HATA MPIGE KIDOGO HUKU MTAANI AMBAPO KILA KONA ZILIPENDWA
Ww ni mtu wa kupuuzwa kama CCM

Ngoma inayobamba kwenye media VS inayopigwa uswazi ipi zaidi?
 
Kwenye music industry kuna fursa kubwa kwa wote wawili kufanya vizuri bila mmoja kuhitaji kumshusha mwingine. Sasa hivi tunawaangalia Nigeria wameendelea sana kimuziki kiasi kwamba tunawaiga. Lakini ukiwaangalia siri ya mafanikio yao wana wanamuziki wengi sana wa kiwango cha Diamond na Kiba au hata zaidi... Kuanzia wakongwe kina P Square mpaka chipukizi kina Wizkid wote wanafanya vizuri kwenye soko la muziki, wanashirikiana na ndio maana muziki wao uko juu.
Tofauti kabisa na sisi ambapo tunao wawili tu na bado tunaendekeza malumbano na mashindano ya kijinga ya nani zaidi kwamba lazima mmoja amfunike mwenzake!
 
Wewe jamaa utakuwa pacha wangu. Hizo ngoma 2 za Mond hunambii kitu! Na siamini kama ipo siku ntakuja kupenda nyimbo ya Mond zaidi ya hizo 2!

Napenda pia nyimbo za Kiba. Na zipo baadhi najua kabisa hapa Kiba kazingua, mf mpk leo sijaelewa Kiba alitaka kusema nini ktk MSINISEME, ule anaosema anapenda kula!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ule si ndiyo type za kama nyimbo ya "zilipendwa" halafu kipindi kile kulikuwa hakuna team hivyo Kiba alikuwa anatamba tu,kwa sasa Kiba hawezi tena kutoa nyimbo kama ile.
 
yaani mimi niwe ukawa halafu niipende ccm??Naanzaje kwa mfano???[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

natania wakuu
Inawezekana,kama sasa hivi unaweza kuwapenda waliyokuwa wana ccm ni rahisi kuja kuipenda ccm yenyewe.
 
Lakini asili ya sukali ni tamu unaweza hata ukaila hivi hivi ila chumvi kuila hivi hivi ni shida labda utafute maembe mabichi.
 
Back
Top Bottom