Diamond vs Ali Kiba

Diamond vs Ali Kiba

beingreal

Member
Joined
Aug 9, 2014
Posts
53
Reaction score
23
Mpo hapo eeee
By albertomsando
Ali Kiba; Diamond na Muziki:
Kila mwanadamu anapenda kufanikiwa katika jambo lolote analofanya. Mafanikio yanatokana na sababu nyingi lakini muhimu zaidi ni;
1. Kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
2. Kuona nafasi (opportunity) na kufanya maamuzi sahihi.

Diamond na Ali Kiba wote kwa pamoja wamefanya hayo yote na kufanikiwa. Ndio maana tunasikia kuhusu 'ugomvi' baina yao.

Binafsi niseme ni ugomvi wa kupikwa na hauna tija kwa muziki wa Tanzania. Na wale wote wanaofurahia au kushabikia hawana nia njema na ukuaji wa muziki wetu.

Ni mawazo ya kipuuzi kuamini kwamba Diamond atafanikiwa zaidi kama Ali Kiba hatafanikiwa. Au eti Ali Kiba atafanikiwa kama Diamond hatafanikiwa.

Tumefika mahali fikra zetu zimeganda. Hatutaki kushirikisha bongo zetu kuona mbali. Tabia hii iko kila mahali. Kwenye siasa, dini, michezo nk.

Kuna wanaoamini ili CCM ishinde lazima CHADEMA ife. Ili CHADEMA ishinde lazima CUF ife. Ili Yanga ishinde lazima Azam ife. Ili Ukristo ushinde lazima Uislamu ufe!!! NK

Na ni tabia hiyo hiyo wanaojiita TeamDiamond na TeamAliKiba wanaiendekeza. Hili ni la kukemea.

Kwa mtu yeyote anaependa maendeleo atakubaliana na mimi Diamond na Ali Kiba wote wanaweza kuwa maarufu na kupata mafanikio kwa PAMOJA na hakuna sababu ya mmoja kufeli ili mwingine afanikiwe.
Wote hawa wawili wana vipaji vya hali ya juu katika muziki. Wote wanao uwezo wa kuimba. Ila kila mmoja kwa aina yake.
Ushauri wangu kwa wote wawili ni kwamba nafasi ya mafanikio na umaarufu sio MOJA. Wala sio MBILI. Ni NYINGI sana. Hata wao wenyewe hawawezi kuzijaza. Kila mtu aendelee kufanya kazi kwa bidii na ubunifu.

Kwa Diamond niseme kwamba yaliyotokea Fiesta ni uonevu kwake. Lakini ni wakati yeye kuwa na busara na hekima na kuepusha mgogoro zaidi. Achukue kama changamoto katika kazi. Asiwape watu nafasi kutuharibia muziki na malengo ya kuukuza zaidi. Najua anaweza.

Kwa mashabiki tuhakikishe team zinabaki Liverpool na Real Madrid. Hizo teamDiamond na teamKiba zibaki kwenye kununua CD original, kuingia kwenye show, kuwapigia kura kwenye Awards, kuwashauri vizuri nk.
Ni jukumu letu kuutangaza muziki wetu kwa ulimwengu. Tutaweza tu endapo hatutawagawa wasanii wetu.
 
Last edited by a moderator:
Binadam.nawashangaaa sana. Hivi unawezaje kulumbana kwa ajili ya mtu fulani wakat na.wewe una maisha yako??
 
haya mambo hatuyapendi lakiniyanaletwa na itabidi tuyachangie...kwa mimi naona bado ni muendelezo ule ule na watu wanakwepa tatizo...hasa ninyi mnaomzunguka diamond tatizo ni kwamba anatunga mziki mzuri sawa, anajituma ....lakini kasahau KUHESHIMU mashabiki...huwa tunaona ninyi mnamzunguka na kujita timu zake MKITUKANA na KUDHARAU watu ...Na kuonesha bwembwe na DHARAU zisizo na msingi...kama hayo mambo ya kudharau hoteli(hukombeya) na Kukandia watu wanaotumia techno(ambapo pia mnaharibu biashara za watu).....hivi kwa mfano mnafikiri hao watu waliowekeza kujenga hoteli mbeya na ninyi mnakuja kuziponda kisa nininyi ni marufu wanaumia kiasi gani kibiasahara.....WATU MLIOMZUNGUKA DIAMOND MMUELEZE UKWELI KULIKO KUJIFICHA kwenye mgongo wa ALI...NA MKUMBUKE KUJITUMA SANA BILA DISPLINE(HESHIMA) NI KAZI BURE HUTADUMU KWENYE KITU UNACHOFANYA
 
hahahahahahahaha.......
 
Attachments

  • final_bstSnapshot_961621.jpg
    final_bstSnapshot_961621.jpg
    60.5 KB · Views: 226
Ni vizuri kuliangalia jambo hili kwa undani zaidi.
"music" nikazi inayotengemea Sana mashabiki(upenzi WA watu kwa kile ufanyacho) nikweli Diamond anafanya vema kwamaana ya jitihada na kuzing'amua fursa lakini hana uhusiano mzuri na wadau WA "music"(washabiki.nk). Kikubwa kinachomponza Ni dharau kwa watu muhim kwenye tasinia hiyo ya music.
mbona Kuna wasanii wengi wamefika hatua nzuri na hawaombewi kushuka kama diamond
 
Hivi huyu Albert Msando si ndio msaliti wa Chadema na Zitto wake?

Atie maji asubiri kunyolewa tu mwakani.
 
haya mambo hatuyapendi lakiniyanaletwa na itabidi tuyachangie...kwa mimi naona bado ni muendelezo ule ule na watu wanakwepa tatizo...hasa ninyi mnaomzunguka diamond tatizo ni kwamba anatunga mziki mzuri sawa, anajituma ....lakini kasahau KUHESHIMU mashabiki...huwa tunaona ninyi mnamzunguka na kujita timu zake MKITUKANA na KUDHARAU watu ...Na kuonesha bwembwe na DHARAU zisizo na msingi...kama hayo mambo ya kudharau hoteli(hukombeya) na Kukandia watu wanaotumia techno(ambapo pia mnaharibu biashara za watu).....hivi kwa mfano mnafikiri hao watu waliowekeza kujenga hoteli mbeya na ninyi mnakuja kuziponda kisa nininyi ni marufu wanaumia kiasi gani kibiasahara.....WATU MLIOMZUNGUKA DIAMOND MMUELEZE UKWELI KULIKO KUJIFICHA kwenye mgongo wa ALI...NA MKUMBUKE KUJITUMA SANA BILA DISPLINE(HESHIMA) NI KAZI BURE HUTADUMU KWENYE KITU UNACHOFANYA

Ni kweli watu wana zunguka wee bila kuleta chanzo cha tatizo nini siku zote mashabiki ndo kila kitu ulimi ni kiungo kidogo ila kina madhara makubwa sana sasa watu.hawataki shobo za kukashifu wao wana kuja na maneno ya chuki wivu ina maana ye ndo wa kwanza kufanikiwa by the way naona hata bado hajafka mbali kivile kama wanavotaka kuaminisha watu asipo badilika na kufuta kauli za kidharau atapotea huwezi kuwa msanii mkubwa bila kuwa na public support
 
nahitaji jibu la hili swali....

1.Kazi zao ni burudani kwetu,kila burudani lazima iwe na mashabiki.So kama ilivo kwa mpira wanamuziki pia wana fans wao waliowatunuku ktk fani iyo ya muziki! 2.Kama mashabiki wa wanamuziki hao hawavunji sheria yeyote kwanini wasiendeleze ushabiki wao,maadamu wana mudana vitu ivo waache washabikie. 3.siungi mkono chuki,matusi na umaamuma wa mashabiki wa viwango vilivopitiliza. 4.Sio lazima kila mtu awe shabiki.,ila wewe usio shabiki don't question y mtu kaamua kuwa shabiki wakati maisha yake anayamudu vizuri na ushabiki ni burudani kwake. 5.Hata sikumoja hatuwezi kuwa na mtazamo na hobby zinazofanana maishani, kiba Mungu akutie nguvu,akupe ubunifu na busara ya kazi!ova
 
Hivi huyu Albert Msando si ndio msaliti wa Chadema na Zitto wake?

Atie maji asubiri kunyolewa tu mwakani.

Kama mimi nimeamua kuwa shabiki wa burudani ya muziki,burudani halali,inayoingiza kipato halali kwa msanii na kuchangia pato la taifa,sio vibaya ata.Tena sio vibaya nikiamua kumtunuku Ally kiba,kwa kutoa muda na pesa zangu kufatilia kazi zake za sanaa,kumuunga mkono na kumpongeza inapobidi,ni sawa kabisaaa!Kwani hao wasanii hawana akili ya kuchambua na kujua mashabik wanaweza kuwagombanisha!!Ushabiki haupingiki
 
1.Kazi zao ni burudani kwetu,kila burudani lazima iwe na mashabiki.So kama ilivo kwa mpira wanamuziki pia wana fans wao waliowatunuku ktk fani iyo ya muziki! 2.Kama mashabiki wa wanamuziki hao hawavunji sheria yeyote kwanini wasiendeleze ushabiki wao,maadamu wana mudana vitu ivo waache washabikie. 3.siungi mkono chuki,matusi na umaamuma wa mashabiki wa viwango vilivopitiliza. 4.Sio lazima kila mtu awe shabiki.,ila wewe usio shabiki don't question y mtu kaamua kuwa shabiki wakati maisha yake anayamudu vizuri na ushabiki ni burudani kwake. 5.Hata sikumoja hatuwezi kuwa na mtazamo na hobby zinazofanana maishani, kiba Mungu akutie nguvu,akupe ubunifu na busara ya kazi!ova

Ni kweli ila je hivi wewe ukaumie yaan ubishane uwe tayar na lolote lile kisa diamond kadhalilishwa?? It doesnt make any sense....shabiki sawa kua shabiki ila haya mengine yamekujaje ya kua ugomvi kudandia vitu ambavyo havina mantiki kubishana kupigana kutukanana kisa kiba kamsema vibaya diamond??

Hata kama n huo ushabiki hivi mtu hawazi nina maisha yangu yananihitaji napiga kelele na kiba au diamond ambae tayar kishatoka na anaingiza mkwanja mzur tu?? Tatizo sisi tunapenda ushabiki maandazi yaan.kufata fata mkumbo jambo ambalo hua linatucost sana
 
Back
Top Bottom